STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Ndugu zangu wanaJF, Imekuwa ni wimbo/jadi kwa CCM kipindi cha uchaguzi kuhubiri eti wapinzani wakichukua nchi wataleta Vita, Udini, Watavuruga amani iliyoko nchini. Je ni kweli kwamba wapinzani wataleta haya ambayo CCM wanayahubiri? HAPANA.
Mimi kwa upande wangu naamini hakuna chama cha upinzani kitakacholeta ugomvi wa aina yeyote kwani viongozi wa Upinzani wana utashi wa kisiasa kama ambavyo tumeona wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi wa mwaka huu.
Ni jambo la kushangaza kuona CCM na serikali yake wamekuwa na desturi ya kuwalazimisha waTZ kuwa na ugomvi usio na msingi wowote hata pale ambapo wananchi kwa hiari yao wamemchagua kiongozi fulani imekuwa ni desturi kwa CCM kuwalazimisha watawaliwe na fisadi wanayemtaka. Hi ilionekana wakati wa kampeni na kutangangaza matokeo pale wanapopeleka askari kwa ajili ya kuwapiga wananchi ili wamtangaze mgombea wao aliyeshindwa.
Mfano hayo yalitaka kutoke mwanza, ubungo, kawe, karatu, arusha, mbeya, musoma etc.
Lakini CCM wakaenda mbali zaidi kwa kufanya hujuma na kutofuata utaratibu katika uchaguzi wa Mameya na wenyeviti wa halimashari, tumeona Zengwe likitokea mwanza, arusha, mbeya mjini, moshi, kigoma, ukerewe, mbulu hii yote ikiwa ni kuhakikisha madiwani wa CDM wasishiriki mchakato wa kuchagua mwenyeki/Meya wao. Hii ni dalili za kuwataka hata watu ambao hawataki fujo unawalazimisha kufanya vurugu na hatimaye kuleta uvunjifu wa amani. Huwezi kumpiga mbunge aliyechaguliwa na wananchi mpaka anazimia halafu unasema unadumisha amani hata siku moja hii haikubaliki.
Nafikiri wananchi sasa wataelewa kuwa wanaoleta vurugu, umaskini, ujinga ufisadi nchi sasa wako hadharani na dawa yao ni kuwang'oa wote, wakibakia ni wachache mno kiasi kwamba hawawezi kufanya kitu kama ambavyo Karatu na moshi wamefanya. Ni kuwaondoa wote.
MUNGI IBARIKI TZ NA WATU WAKE.