Maajabu Ya Marais Ikulu ya Marekani "The White House"

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Pengine Kuna watu wanasikia Mengi kuhusu Makao makuu ya kiserikali ya Nchi ya Marekani, Washington DC lakini wasijue Nini chanzo Cha jina la huo Mji ambamo Imejengwa ikulu ya Nchi hiyo The White House.

George Washington alikua Ni Kiongozi muasisi wa Taifa la Marekani, The United States tangu Uhuru mwaka 1789 ambapo alikaa madarakani mpaka 1797 alipoondoka madarakani.

Rais George Washington ndie Kiongozi mwenye kukumbukwa katika Taifa Hilo kuliko mtu yeyote ingawaje Jamii ya watu weusi Nchini Marekani humkumbuka Rais John F. Kennedy Kama mkombozi wa Haki zao lakini kwa ujumla Taifa la Marekani humtabaruku Washington Kama baba wa Taifa Hilo na ndio maana Makao makuu ya Nchi hiyo huitwa kwa Jina lake "Washington".

Moja ya kumbukumbu aliyoicha vichwani mwa watu Ni pale alipojitolea Vipande vyake vya Madini ya fedha ili Nchi itengeneze sarafu yake baada ya Kuufurusha ukoloni wa Kiingereza Nchini humo.

Mbali na Mambo haya ya kushangaza aliyoyafanya Washington Marais wengi wa Marekani waliofuata walikuja na upekee wao ndani na nje ya White House yaliyovuta hisia za watu.

Ukija huku Nchini kwetu utasikia watu wakisema Rais Jakaya Kikwete alikula Sana Bata kwa kusafiri Sana duniani lakini hakumfikia Rais wa Tano wa Marekani James Monroe, huyu bwana alisafiri na kutembelea kila Sehemu ya majimbo yote ya Marekani ambayo Ni moja ya Nchi kubwa katika Bara hilo la Amerika ya kaskazini.

Watu wengi siku Hizi hujiona Fahari pale wanapopiga "serfie" na kutupia Mtandaoni na kujiona wametoboa maisha lakini aliefurahia hili Jambo kwa Mara ya kwanza Kama Rais alikua Rais wa Sita wa Marekani John Adams (1825-1829) ndiye alikua Rais wa kwanza wa Nchi hiyo kupigwa picha.

Ni Jambo la Heri Sana Kushangilia pindi mtu anaposhinda Uchaguzi lakini hatupaswi kusahau kua Kuna maisha baada ya Ushindi huo, William Harrison alichaguliwa kua Rais wa 9 wa Marekani 1841 lakini alidumu katika kiti hicho kwa siku 32 tu akafariki baada ya kuugua Ugonjwa wa pumu usemi usemwao Usiyoyajua Ni sawa na Usiku wa Giza ukatimia kwake.

Unaweza kushangaza inawezekana Vipi kwa Afrika lakini sio kwa Marekani bwana, Rais wa 15 James Buchnan alikua hajaoa mpaka alipoingia White House.

Kiongozi Bora sio lazima awe na elimu ya Shahada au Uhadhiri mbona Andrew Johnson alikua hajui kusoma Wala Kuandika mpaka alopofikia umri wa miaka 17 lakini Baadae alichaguliwa kua Rais wa Taifa kubwa la Marekani na kutinga ndani ya White House.

Umewahi kusikia kua mapenzi sio ubondia na ukaamini? Na ndivyo ilivyo kwani mke wa Rais wa 19 wa Marekani James Polk alikua Ni mkali Sana alipiga Marufuku kucheza karata na muziki ndani ya ikulu ya Marekani "The White House" mpaka alipomaliza mda wake 1849
Kila mmoja ana talanta yake japo muda mwingine talanta ya mtu huweza kuonekana Kama miujiza au ushirikina.

James Garfield Rais wa 20 wa Marekani alikua na uwezo wa kutumia mikono yake yote miwili muda alowashangaza watu kwa Kuandika kigiriki mkono wa kwanza huku mkono wa Pili ukiandika kilatini kwa wakati mmoja.

Harry Truman hakururahia maisha ya kuishi kwa muda mrefu Sana katika ikulu kwani aliishi nje ya ikulu kwa muda ili kupisha marekebisho na ndiye rais Alie ruhusu Matumizi ya bomu la nyuklia katika Vita ya Pili ya dunia huko Nagasaki na Hiroshima 1945 ambapo watu wengi walipotezaaisha Hilo Japan.

Watanzania walimshangaa San Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na Kashfa za rushwa, lakini Rais wa 39 Wa Marekani Richard Nickson yeye alijiuzulu kwa Matumizi mabaya ya Ofisi "The Watergate Scandal"
Visa Ni vingi vyenye kusisimua kuhusu Marais waliowahi kukanyaga ikulu ya Marekani "The White House" lakini hivi Ni baadhi tu visa hivyo.

Peter Mwaihola
1671428697122.jpg
 
Back
Top Bottom