Maajabu: Maiti yagoma kuzikwa ili ivishwe viatu vipya

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
2,126
3,022
Waombolezaji waliofika katika boma moja eneo la Kilingili, Vihiga nchini Kenya wameachwa midomo wazi baada ya mwili wa marehemu kukataa kuingia ndani ya jeneza hadi ulipovishwa viatu vipya alivyokuwa amenunua.

Duru zinaarifu kwamba jeneza lililetwa kisha jamaa na marafiki wa mwenda zake walimkaribia na kuubeba mwili wake kwa makini kuuweka ndani ya jeneza.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Taifa Leo walishtuka baada ya mwili huo kuanza kufura na jeneza kuonekana kuwa dogo.

Inasemekana kwamba waliotwikwa jukumu hilo waliamua kulipanua jeneza lakini walipojaribu kuuweka mwili huo ndani ya sanduku safari hii ulirefuka.

“Lazima kuna mtu marehemu hamtaki hapa. Haya mambo hayawezi kufanyika bila sababu,” jamaa mmoja alisikika akisema.

Waombolezaji walipoarifiwa kuhusu kisa hicho walibaki wamepatwa na mshtuko. “Kama amekataa kuingia jenezani hata kaburini basi pia atakataa. Lazima kuna mchawi hapa,” mwombolezaji mmoja alisika akisema.

Penyenye za kijijini zilisema kwamba ilibidi wazee wa kijijini waliitwa kutegua kitendawili hicho.

“Watu wote watoke nje,” wazee waliamuru. Inaarifiwa kwamba wazee walipoachwa chumbani humo walianza kumtandika viboko marehemu. “Usipokubali kuingia ndani ya jeneza tutakutupa kama mbwa. Ingia humu mara moja,” sauti ya mzee mmoja ilisikika ikiamuru kutoka chumbani.

Semasema zinaarifu kwamba baada ya dakika tano za adhabu kali mlango ulifunguliwa na wazee hao wakamwita mke wa marehemu.

“Nimesikia sauti ya marehemu ikiniambia kwamba avishwe viatu vyake alivyonunua juzi,” mke wa marehemu alisema.

Viatu hivyo vililetwa haraka na mwenda zake akavishwa na baada ya hapo waliokuwa wakiutia mwili wake ndani ya jeneza waliitwa kuendelea na shughuli hiyo.

Duru zinasema kila mmoja katika mazishi hayo alibaki mdomo wazi kwani mwili uliingia jenezani bila tatizo lolote. “Marehemu hakutaka kuacha viatu vyake nyuma,” muombolezaji mmoja alisikika akisema.
 
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
Watu wote watoke nje,” wazee waliamuru. Inaarifiwa kwamba wazee walipoachwa chumbani humo walianza kumtandika viboko marehemu. “Usipokubali kuingia ndani ya jeneza tutakutupa kama mbwa. Ingia humu mara moja,” sauti ya mzee mmoja ilisikika ikiamuru kutoka chumbani.
 
Me nikioanaga tu habari imetoka Kenya au Nigeria najua itakuwa..tea of milk
IMG_20210806_133727.jpg
 
MHU. :9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

MHU. :9:6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
 
Waombolezaji waliofika katika boma moja eneo la Kilingili, Vihiga nchini Kenya wameachwa midomo wazi baada ya mwili wa marehemu kukataa kuingia ndani ya jeneza hadi ulipovishwa viatu vipya alivyokuwa amenunua.

Duru zinaarifu kwamba jeneza lililetwa kisha jamaa na marafiki wa mwenda zake walimkaribia na kuubeba mwili wake kwa makini kuuweka ndani ya jeneza.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Taifa Leo walishtuka baada ya mwili huo kuanza kufura na jeneza kuonekana kuwa dogo.

Inasemekana kwamba waliotwikwa jukumu hilo waliamua kulipanua jeneza lakini walipojaribu kuuweka mwili huo ndani ya sanduku safari hii ulirefuka.

“Lazima kuna mtu marehemu hamtaki hapa. Haya mambo hayawezi kufanyika bila sababu,” jamaa mmoja alisikika akisema.

Waombolezaji walipoarifiwa kuhusu kisa hicho walibaki wamepatwa na mshtuko. “Kama amekataa kuingia jenezani hata kaburini basi pia atakataa. Lazima kuna mchawi hapa,” mwombolezaji mmoja alisika akisema.

Penyenye za kijijini zilisema kwamba ilibidi wazee wa kijijini waliitwa kutegua kitendawili hicho.

“Watu wote watoke nje,” wazee waliamuru. Inaarifiwa kwamba wazee walipoachwa chumbani humo walianza kumtandika viboko marehemu. “Usipokubali kuingia ndani ya jeneza tutakutupa kama mbwa. Ingia humu mara moja,” sauti ya mzee mmoja ilisikika ikiamuru kutoka chumbani.

Semasema zinaarifu kwamba baada ya dakika tano za adhabu kali mlango ulifunguliwa na wazee hao wakamwita mke wa marehemu.

“Nimesikia sauti ya marehemu ikiniambia kwamba avishwe viatu vyake alivyonunua juzi,” mke wa marehemu alisema.

Viatu hivyo vililetwa haraka na mwenda zake akavishwa na baada ya hapo waliokuwa wakiutia mwili wake ndani ya jeneza waliitwa kuendelea na shughuli hiyo.

Duru zinasema kila mmoja katika mazishi hayo alibaki mdomo wazi kwani mwili uliingia jenezani bila tatizo lolote. “Marehemu hakutaka kuacha viatu vyake nyuma,” muombolezaji mmoja alisikika akisema.
Huyu bila shaka alikuwa mwanachama wa UWABATA
 
MHU. :9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

MHU. :9:6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Tembea uone na kuamini, usiishie kusoma
 
Back
Top Bottom