M4C-OPD: Tundu Lissu, John Heche na Deo Munishi - Kutoka Singida

We kalale!!ndo maana mmebaki misukule ya lumumba na wa mwisho kwa maendeleo!!!You have to think big!!!Badilikeni wana Singinda!!!Amkeni usingizini!!kumeshakucha eti!!!
Bora uwe maskini wa kipato kuliko kuwa maskini wa fikra na mtumwa wa wachagga
 
Lissu alitumia muda wake wa dakika kumi na tano kuelezea madhila yanayosababishwa na wananchi kutosikiliza maneno ya muasisi wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa kwenye maandishi ya kitabu alichokiandika mwaka 1993 cha Uongozi na Hatima ya Taifa letu.
Tundu Lissu alisema kuwa baadhi ya maneno muhimu sana kwenye kitabu hicho ni yale aliyowaasa watanzania kuipiga chini ccm kwani kuendelea kwake kudumu madarakani kutaisababisha nchi yetu huko mbeleni kuwa gizani.
Alizungumzia matatizo ya udini yanavyolisonga taifa hili kwa sasa huku serikali ikishindwa kutoa kauli yeyote.
Amehoji kwa nini serikali imeshindwa kutoa kauli juu ya uchomaji wa makanisa na mauaji ya padre huko zanzibar pamoja na umwagiaji wa tindikali kwa shehe hukohuko Zanzibar.
Mheshimiwa Tundu Lissu aliwaambia mamia ya wanasingida waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira wa shule ya msingi mkombozi kuwa ccm ndio wamekuwa hodari wa kuwagawa watanzania kwa misingi hii ya udini kwa kasi ya ajabu.Anaendelea kusema kuwa Lowassa anapita kuwahonga viongozi wa dini ya kikiristo huku akiwaambia kuwa uchaguzi unaokuja anayestahili kuchaguliwa kuwa rais mwakani ni mkiristo kwa kuwa huu sasa ni wakati wetu wakati huo huo viongozi wa ccm wa dini ya kiislamu nao wanapita misikitini wakiwaambia waumini wao kuwa wasikubali kumchagua kiongozi yeyote ambaye si muislamu kwa kuwa nchi hii kuna mfumo kristo.Sasa mheshimiwa Lissu anasema kama huo si udini ni nini?
Alizungumzia pia namna ambavyo maccm wamechochea mauaji yaliyotokea huko kiteto.Anasema maccm wafugaji wanawasukuma wafugaji wakawavamie wakulima na maccm wakulima nao wanawachochea wakulima wakawauwe wafugaji na hayo ndo yamepelekea mauaji ya zaidi ya watu kumi huko kiteto wiki zilizopita.
Mwisho akawaomba watanzania tubadilike na tusikubali kugawanywa kwa misingi yeyote ile,tumchague rais muadilifu ambaye si mwizi bila kujali dini,kabila lake ama sehemu atokako.
Ujumbe mwingine muhimu uliotolewa na wazungumzaji waliotangulia ni kuwa hakuna mtu maarufu kuliko taasisi hii.
Awali Katibu wa Bavicha Taifa Bwana Munisi alisema ikiwa rais anawafahamu wauza madawa ya kulevya lakini hawataji ina maana anashirikiana nao?

Asante kwa kujazia zaidi alichomimiba Lissu na sikua nimekidaka
 
Kauli za mfa maji. Mipango yenu ya kuiua ifikipo 2015 imedoda ehe!
 
Bora uwe maskini wa kipato kuliko kuwa maskini wa fikra na mtumwa wa wachagga

Umenena vema ndugu. Umasikini wako wa kidmfikra ni janga kwa taifa.

Umasikini huo ndio unaokufanya ufikiri kikabila kabila.

Wachaga wanakunyima usungizi ehee!
 
huyo jamaa ni kilaza sijapata kuona. Lissu sijui ni mwanasheria wa namna gani? Jamaa nadhani anaelekea kuwa Chizi kwani hanaga point za msingi za kuongea wala kujenga Taifa ila anafundisha watu Matusi, Kulalamika, Kulaumu, Kusema hovyo, nk.... afu eti kuna watu huyu jamaa ndo roll model wao utaiga nn toka kwa Kilaza huyu?
Mkuu OPD ndo kwanza Ina siku ya nne. Ikifika wiki ya pili nadhani utakuwa marehemu kwa shinikizo la damu.
 
huyo jamaa ni kilaza sijapata kuona. Lissu sijui ni mwanasheria wa namna gani? Jamaa nadhani anaelekea kuwa Chizi kwani hanaga point za msingi za kuongea wala kujenga Taifa ila anafundisha watu Matusi, Kulalamika, Kulaumu, Kusema hovyo, nk.... afu eti kuna watu huyu jamaa ndo roll model wao utaiga nn toka kwa Kilaza huyu?
Je tutaiga nini toka kwako Ndimu Mkatashombo, mtu asiye na akili angeweza kushinda kesi hata moja anazosimamia? Je angeweza kupata ubunge huko singida (ama unataka kutuambia waliomchagua hawana akili zaidi ndio maana wakamchagua asiye na akili)? Wewe kama ungekuwa na akili hata post uliyoiandika ungeiandika kwa akili lakini kwa usivyo na akili umeiandika ki-ukosa akili.
 
Back
Top Bottom