M23 Washambulia tena Mji wa Sake

Pk akidondoshwa CONGO DR itapata kutulia. Shida sio WATUTSI kwa sababu hata BURUNDI watutsi wapo na kwa kiasi fulani amani ipo. Japo watutsi wana kasumba zao za kujiona wao ni wateule kuliko wengine. Nimeishi nao hawa jamaa wana kakujisikia mno. Hilo nalo ni tatizo.
 
Hao waasi wakubaliwe kuingizwa jesheni... Nadhan tutatatua mgogoro kwa kiasi chake
Hii haiwezekani kabisa. Hata PK jeshi lake top officers wahutu ni wachache mno. Na siku zijazo hata junior staffs jeshini kutakosekana mhutu hata mmoja. Mark my words.
Kuruhusu banyamulenge kwenye jeshi la FARDC ni sawa na kumruhusu KINANA kuwa KATIBU MKUU CHADEMA
 
Kipindi cha mobutu waliishi namna gani?

Aliwakandamiza kidikteta, ila sasa wameonja damu na wamejua kupigana, hata Mobutu afufuke leo na awe nguvu alizokua nazo, hawezi kuwadhibiti.
Wananchi kwenye nchi yoyote ukiwakandamiza hakikisha unaishi milele, usiache waje kujua kuwa na wao wana uwezo.
 
Aliwakandamiza kidikteta, ila sasa wameonja damu na wamejua kupigana, hata Mobutu afufuke leo na awe nguvu alizokua nazo, hawezi kuwadhibiti.
Wananchi kwenye nchi yoyote ukiwakandamiza hakikisha unaishi milele, usiache waje kujua kuwa na wao wana uwezo.
Aliwadhibiti wao tu au na wacongo wengine?.
Hoja yangu hapa ni kuwa ni kuwa watii sheria na taratibu za Congo.
 
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mji wa Sake uliopo km 23 magharibi mwa Goma ambai ni mji mkuu wa Kivu ya kaskazini, umeshambuliwa tena.

Ikumbukwe wiki iliyopita waliuzingira na kukaribia kuuteka lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya serikali na washirika wake.

Wakati huo huo msafara wa silaha mzito pamoja na mitambo ya maroketi ya kutungulua ndege kutoka Rwanda imeonekena ikielekea uwanja wa mapambano upande wa m23. Wachunguzi wa umoja wa mataifa umethinitisha kundi la m23 kutumia mitambo ya SAM(surface to Air Missiles)
Baada ya m23 kushambuliwa sana na ndege za serilali, Rwanda imelazimika kutoa mitambo hiyo ili kuwawezesha m23 kukabiliana na ndege ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu na kusababisha hasara kubwa kwa m23. SAM ni mitambo yenye rada ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kutungua ndege za adui.

Hii ni ushahidi tosha kuwa Rwanda inahusika sana katika vita hii moja kwani hakuna kundi la waasi laweza kumiliki mitambo hiyo. Lakini pia ili.mitambo huyo ifike kivu lazima ifate barabara kutoka Rwanda kuingia uganda ndio ifike DRC

Wakati ambapo mji wa Sake uko mikononi mwa majeshi ya serikali, m23 wanasenekena wako upande wa milima inayouzunguka.

Wakongomani wasubiri kwa hamu kusikia majeshi ya serikali na washirika wake wanakomboa maeneo yote yanayoshikiliwa na waasi kama sasha,kiwanja,Kitchanga, Rutshuru,Rubaya pamoja na Bunagana ngome kuu ya m23.

Ni jambo linalowezekana ila linahitaji uwekezaji mkubwa wa nguvu na teknolojia ya kisasa ya zana za mapigano kwani Rwanda na Uganda wameingia vitani upabde waasi wazimawazima bila kubakisha kitu nyuma.

Maswali kadhaa ya kujiuliza.
1. Inakuwaje adui anaingiza nchini kwako zana za kisasa bila kupata wakati mgumu na hasara? Wapi intelijensia ya nchi?

2. Kwa nini majeshi ya serikali na washirika wake hayateki maeneo ya waasi badala yake nguvu kubwa ni kukilinda na kujibu mashambulizi tu?

Natamani vita iishe ili maisha ya raia wa Kongo yaendelee
Vita ya maslahi hii.

Tuwaombee raia
 
20240216_172242.jpg
 
Back
Top Bottom