Kikao kijacho cha mahakama lazima nikutoe kwa dhamana. Mapumziko yetu China. Nikupe pole kwa kutenganishwa na sisi kwa siku zote hizo. Mzee wako tutapita kumsalimia. Hii itakusaidia kuwaepuka paparazi wa bongo kwa muda mpaka wazoee kuwa kwako nje ya gereaza. Pole honey kwa yooote. Maisha ni hatua.
Mimi sioni kama kuna ukiukwaji wa sheria uliofanywa na Mkurugenzi wa Mashtaka, mshtakiwa hufunguliwa shtaka kulingana na ushahidi uliopo, kama DPP hana ushahidi unaoweza kuthibitisha kwamba Lulu ameua kwa makusudi na aliua bila ya kukusudia kuna haja gani ya kuendelea kumshtaki Lulu kwa mauaji ya kukusudia. Ukiangalia jinsi tukio lenyewe lilivyotokea ni wazi kwamba kuna ugumu kwa DPP kuweza kuthibitisha mauaji ya kukusudia. Ni mamlaka yake na nakubaliana nae kwa kitendo hichi cha kubadilisha shtaka. Hakuna mamlaka yoyote ya Mahkama yaliyoingiliwa hapo.
Mkuu, "mustakabali" nadhani maana yake ni "future," sio? Kama ndivyo badi sidhani kama unaweza hata kusema "ameepuka future ya kunyongwa" kwa sababu hakuna anaejua kwamba asingefutiwa mashitaka angekutana na future ya kunyongwa.Ameepuka mustakabali wa kunyongwa.
Sijui kama kuna kutanabahisha tofauti ya mustakabali na adhabu katika uandishi wetu.
mpaka alipata ugonjwa wa nyonga akakimbilia apollo! chezeiya ukame weye??!! sasa atapona kabisaaaaaaa katoto kakitoka!Wamwache mtoto akanyweshee jangwa. Jangwa limezidiwa na ukame town.
Mimi sioni kama kuna ukiukwaji wa sheria uliofanywa na Mkurugenzi wa Mashtaka, mshtakiwa hufunguliwa shtaka kulingana na ushahidi uliopo, kama DPP hana ushahidi unaoweza kuthibitisha kwamba Lulu ameua kwa makusudi na aliua bila ya kukusudia kuna haja gani ya kuendelea kumshtaki Lulu kwa mauaji ya kukusudia. Ukiangalia jinsi tukio lenyewe lilivyotokea ni wazi kwamba kuna ugumu kwa DPP kuweza kuthibitisha mauaji ya kukusudia. Ni mamlaka yake na nakubaliana nae kwa kitendo hichi cha kubadilisha shtaka. Hakuna mamlaka yoyote ya Mahkama yaliyoingiliwa hapo.
Mkuu, "mustakabali" nadhani maana yake ni "future," sio? Kama ndivyo badi sidhani kama unaweza hata kusema "ameepuka future ya kunyongwa" kwa sababu hakuna anaejua kwamba asingefutiwa mashitaka angekutana na future ya kunyongwa.
Lulu ameepuka uwezekano wa kuhukumiwa kunyongwa. Simple as that.
Na sidhani kama mwandishi wa kawaida wa gazeti kama la MWANANCHI anaelewa tofauti yake, au whether wanajali.