Lukuvi: Tunakuja na bei elekezi kwa viwanja

Kama ndiyo hivyo basi hata Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Mifugo naye atoe bei elekezi na Mawaziri wengine wafuate mbona mishahara tuliyo nayo itakuwa ni mikubwa Sana hata tutaomba ipunguzwe kwani savings itakuwa kubwa mno mabenk yatajaa pesa!!!
Jamani hivi Waziri anayeangalia riba zinazotolewa na mabanki sio Waziri wa Fedha? Tutaomba riba ziangaliwe upya!
 
ujamaa wa dizaini hii utaporomosha sana uchumi. angesema kwa vinavyopimwa na serikali ningemuelewa.
 
The value of land has been increasing every time and every minutes especially in big cities like Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and so on...! This lead to poor people can't afford it.
 
Bravo! Bravo! Bravo!.
Imekuja imechelewa, lakini huu ndiyo ukweli. Miji imekuwa haiendelei kutokana na huu utapeli wa kwenye ardhi.
Hiyo ni spirit nzuri. Mungu ibariki Tanzania yangu.
huyu jamaa hayuko serious nijuzi tu alinukuliwa akisema mafisa ardhi wanahujumu miradi ya viwanja kwa kujiuzia wenyewe Kisha kuviuza kwa bei kubwa kwa Wananchi hivyo Wizara imeamua kuandaa Mkakati wa Makampuni binafsi kufanya kazi ya upimaji ardhi.
 
Hili nalo ni LA kukurupuka et mtu shamba Lake akitaka kupima akabidh halmashaur ndo wapime na kumilikisha
 
The value of land has been increasing every time and every minutes especially in big cities like Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and so on...! This lead to poor people can't afford it.
they can go to hell, if thet can't get rich
 
Kwakweli kwa Bunge kutokuwa Live wananchi tunabaki gizani sana.Sasa hoja kama hizo zinajibiwa na wananchi hatuzisikii kabisa na hata ikiandikwa kwenye magazeti ni kwa kifupi sana.Sikui serikali yetu inatufikiria nini sisi wananchi.
 
Ni wazo zuri,ila kama kijana hana akili ay kujenga hata umpe bure hajengi na atakiuza tu.
Watu walipewa mwabepande na wakauza.Kila mtu anataka kukaa City Center,Tabata,Sinza,Mikocheni,Oysterbay,Mwenge
Ukimuambia aende Chanika hataki,kila mtu anapana hapo hapo,sasa aache tu mbanweee mpaka mtie akili,wa kutoka mikoani mbio wanaongoza kujenga Dar ila waliopo kwa vile akili zimelala na Jiji wao wanasubiri siku Dunia itakapogeuzwa matajiri wawe masikini na wao wawe matajiri.
Viwanja bado rahisi wala sio ghali,na hata kama akisema atoe bei elekezi bei inaangalia vitu vingi na hili wataalam watamshauri
The selection criteria are set by the interested party based on his/her needs and can vary from one buyer to the other.Among others;size,cost;accessibility,lease;neighborhood are among key ones
 
Waanze na viwanja vya serikali vinavyosimamiwa na manispaa, waende kwenye nyumba za serikali kupitia mashirika yake-sitaki kuamini kwamba Mtanzania wa kawaida anaweza kununua nyumba kwa zaidi ya M50! Lukuvi na serikali watuondolee huu usaniii!
weee ukome kutuita WATANZANIA WAKAWAIDA hakuna mtanzania wa kwaida hii kauli mm sipendi kuisikia.
 
wewe ut
We acha ubwanyenye serikali Ya gani ni makini ili kuwakumboa watanzania wa kawaida. Viwanja havinunuliki kwa mantiki Ya maisha ya kawaida ya mtanzania.ni kipindi kifupi tu hii issue Ya viwanja Na Nyumba vimepaa kupita maelezo na kwa uhalisia uwezo ulibaki kwa mafisadi na Watu wa kuja kama wahindi wakati wazawa wa kawaida wakikosa uwezo wa kumiliki ardhi yao. Serikali kwa kufanya hivyo itasaidia wengi ambao tulishakata tamaa Ya kumiliki ardhi.
wewe utakataje tamaa ya kumiliki ardhi mzee? Au unataka kiwanja cha mbezi beach uuziwe kwa laki tano? hiyo haiwezekani ila vya laki tano vipo sema sio huko unakotaka ww.Jaman msipende slope kwa expense ya watu wengine kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake jikune unapofika!
 
Waanze na viwanja vya serikali vinavyosimamiwa na manispaa, waende kwenye nyumba za serikali kupitia mashirika yake-sitaki kuamini kwamba Mtanzania wa kawaida anaweza kununua nyumba kwa zaidi ya M50! Lukuvi na serikali watuondolee huu usaniii!
Mnnnnnh?
 
Hakuna kiwanja ambacho hakinunuliki labda kiwe hakiendani na bei hiyo! We uliyeshindwa kununua kiwanja una shilingi ngapi na unataka ununue wapi?! Nilionya kuwa taifa linarudi kwenye ujamaa kiaina.! Huu ni mfumo wa hovyo kabisa!
Mkuu kuwa na huruma na watz wenzako basi, wanaonunua viwanja vya kupima ni watu wa level flani tu kama hali isiposimamiwa vizuri wengi wataendelea kujenga sehemu zisizopimwa, ukiwa na uwezo wa kununua wewe kuna wengine kibao wanatamani wanunue viwanja. Usihofu lakini taifa halirudi kwenye ujamaa kiaina ila angalau kuwe na utaratibu flani japokuwa haina maana kwamba viwanja vyote vitakuwa bei ya chini, vitakuwepo vya level yenu pia na vya level ya wengine. Thamani ya ardhi haipo juu kivile, mfano serikali (halmashauri) inalipa fidia kiduchu mfano ekari moja mtu anaweza akalipwa laki 6 alafu yenyewe inapima viwanja wanatoa viwanja kuanzia vitatu vinauzwa milioni 6 kila kimoja (sasa hapa huoni kwamba kuna watu wanaachwa automatically, hayo makampuni sawa kwa kuwa yametumia fursa iliyopo kufanya biashara kutokana na uzembe wa serikali hivyo ukiwa na hela unajilipua kununua lakini mpaka vinavyopimwa na serikali navyo ni majanja)
 
hii safi sana aisee..viwanja ni kweli havinunuliki kwa walio wengi..pia waziri anatakiwa akaze sana kusafisha wizara hiyo..ina maudhi kinoma..imejaa watu sijui wakoje..
 
hata kama tukirudi kwenye ujamaa lakini kama lengo ni maslahi na manufaa kwa wengi bora tuende tuu,wengine wanapinga tuu utadhani na wao ni ma-bourgeoisie kumbe choka mbaya tuu kama sisi,halaf badae wanaanza kulalamika ooh! keki ya taifa wanakula wachache.kama serikali ina mpango wa kuwawezesha masikini kuafford kununua viwanja wewe mtoto uliyetokea maisha duni unapinga ili kutetea masilahi ya nani hasa? kumbuka Watanzania wengi ni masikini so mwisho wa siku serikali ni wajibu wao kuwawezesha masikin ambao ndo wengi.wengi wanashindwa kujenga kwa sababu ya bei ya viwanja kuwa ghali au inabidi wajenge nje sana ya mji kitu ambacho kinaleta adha nyingine tena,na ndo matatizo ya uvamiz wa viwanja yanapoongezeka then watu kubomolewa nyumba zao halaf lawama zoote tunazirudisha tena serikalini.
 
Naunga mkono hoja.
Lukuvi akiongea huvyo jua ndiyo imeshatoka. Tutabaku kumkumbusha tu bungeni. Siku hizi style ya mawaziri wanapobanwa bungeni ni kukubaliana na hoja haraka haraka ili kuua mjadala au kuahidi kitu halafu hakuna utekelezaji.
 
Back
Top Bottom