Lugha moja itawale ulimwengu?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Nawaza kuwa ingekuwa vema kukawa na lugha moja ambayo itakuwa ndiyo Lugha rasmi ya ulimwengu wote.
Kuwepo kwa Lugha moja rasmi ya ulimwengu, kungeleta faida zifuatazo:-

Kurahisisha mawasiliano.
Kujenga umoja wa kimataifa.
Kufanikisha ueneaji wa tekinolojia ulimwenguni.
Kupunguza dhana ya ukabila na ubaguzi wa kimataifa.
 
Ni wazo zuri makyao. Lakini nani atakubali kuacha lugha yake akumbatie ya mwenzie?
Pia ingekuwa vema ukitoa mapendekezo ya namna ya kuanzisha hiyo lugha na namna ya kumfikishia kila binadamu wa kila sehemu. Mfano, tukichukua kichagga kiwe lugha hiyo, tunaanzia wapi?
 
Exaud if thats a dream you better wake up and face the reality, that won't happen!..
Yaani dunia nzima itawalliwe na lugha moja tu?
BTW, wewe kwa mawazo yako ungependa lugha gani itawale?
 
Lugha moja kutawala dunia ni kitu kinachowezekana kabisa kwa msingi wa kutawala tu, lakini misingi ya kuzungumzwa na kutumiwa na watu wote aah' hiyo habari haipo, kwani lugha hujiegemeza na tamaduni ya watu na n.k, je tutafanya tamaduni moja, kabila au jamii kuwa moja, rangi ya watu iwe moja, mtazamo mmoja na hata makazi yawe ya aina moja! hata Muumba wetu katwambia nimekuumbeni mataifa, rangi lugha na maumbile tofauti ili mpate kutambuana,
 
Hili lilishajaribiwa na lugha ya Esperanto ambayo ilishindwa vibaya sana, it is not practical at all.Ukitaka kujifunza how impractical this is study the fall of Esperanto.
 
Sidhani hoja ni zuri. Kwanza hakuna dokezo ya kwamba dunia inaelekea kuwa na lugha moja pekee pili sidhani ya kwamba ni shabaha inayofaa.

1. Lugha zinaendelea kubadilikabadilika. Lugha iliyoenea kushinda zote wakati wa karne ya 19 na 20 ni Kiingereza - itaendelea kama lugha moja kwa muda gani? Tayari tofauti ziko kati ya Kiingereza cha Uingereza, Marekani, Uhindi n.k. Tukumbuke historia ya [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/Kilatini"]Kilatini[/ame] ilikuwa lugha ya mawasiliano kwa eneo kubwa lakini ilipasuka kuwa [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha_za_Kirumi"]lugha nyingi za Kirumi[/ame].

2. Utu wetu uko katika utamaduni. Napenda kujifunza lugha naona ya kwamba kila lugha ndani yake ina utamaduni tofauti. Angalia jinsi wanavyosifu, kutukana, kusalimiana n.k. kwa lugha mbalimbali. Hali hii ni utajiri! Tusiupoteze tujitahidi kutunza lugha zetu iwezekanavyo.

3. Lakini kwa mawasiliano naona faida kuwa na lugha kadhaa zinazofaa kwa mawasiliano kati ya mataifa. Ila tu: tusishangae watoto wetu watajifunza Kichina nadhani - wenzangu wanaonaje?
 
Ni wazo zuri makyao. Lakini nani atakubali kuacha lugha yake akumbatie ya mwenzie?
Pia ingekuwa vema ukitoa mapendekezo ya namna ya kuanzisha hiyo lugha na namna ya kumfikishia kila binadamu wa kila sehemu. Mfano, tukichukua kichagga kiwe lugha hiyo, tunaanzia wapi?

MUTENSA,
Jambo la msingi kabisa ni kuona umuhimu.
Kwa kuwa umeona huo umuhimu.
tuzae mbinu na njia kwa pamoja.
 
Hili lilishajaribiwa na lugha ya Esperanto ambayo ilishindwa vibaya sana, it is not practical at all.Ukitaka kujifunza how impractical this is study the fall of Esperanto.

BLURAY,
Hitimisho lako linanitia wasiwasi.
Je ni lazima A akishindwa na B ashindwe?
 
....... Kwanza hakuna dokezo ya kwamba dunia inaelekea kuwa na lugha moja ....................................
........................................... Ila tu: tusishangae watoto wetu watajifunza Kichina nadhani

KIPALA,
Changamoto yako ni nzuri.
Lakini mbona sentensi zako (ya nyekundu na ya bluu) zinapingana?

Pia hiyo sentensi ya bluu inakubaliana na changamoto yangu.
Tuweke sawa mkuu.
 
Dunia ya sasa inataka mtu ajue lugha nyingi awezavyo.Kwamba ULIMWENGU unaweza kukubaliana kuwe na lugha moja tu... kwa maoni yangu naona itakuwa ngumu.... chukulia mfano wafaransa walivyo na kiburi na lugha yao.Ukienda kwao hata kama wanajua kiingereza, ukiwasemesha hawatajali kukujibu..inabidi uanze kutafuta vocabulaire yako iliyopotea miaka mingi uweze angalua kuomba maji.Lugha ni utambulisho - mara nyingi lugha zilizokomaa, wenyewe hawatapenda kuzipoteza na watazilinda kwa gharama yoyote ile.Hapa Tanzania kuna mapambano kutaka kukipandisha kiswahili kwenye chati zaidi ili angalau kiwe moja ya lugha zenye kutumika angalau kwenye bara la Africa....jitihada hizi haziko kwenye kiswahili tu, ziko pia kwenye lugha nyingine kama kihausa n.k. Mwelekeo nionavyo hauko katika kupata lugha moja bali kueneza lugha nyingi zaidi ulimwenguni.
 
Nawaza kuwa ingekuwa vema kukawa na lugha moja ambayo itakuwa ndiyo Lugha rasmi ya ulimwengu wote.
Kuwepo kwa Lugha moja rasmi ya ulimwengu, kungeleta faida zifuatazo:-

Kurahisisha mawasiliano.
Kujenga umoja wa kimataifa.
Kufanikisha ueneaji wa tekinolojia ulimwenguni.
Kupunguza dhana ya ukabila na ubaguzi wa kimataifa.

Unayosema ni kweli kabisa, lakini ni lugha gani hiyo na vigezo gani vitakavyotumika katika kuamua lugha hiyo ni ipi?

Kwa sasa hivi kutokana na population kubwa ya Wachina Wazungu wengi wameanza kujifunza mandarin na cantonese lugha ambazo zinaongewa n watu wengi China. Na kwa maoni yangu miaka michache ijayo idadi ya Walimwengu watakaokuwa wanajifunza lugha hizo itaongezeka kwa kasi sana ili kuwawezesha kufanya biashara au hata kupata ajira China ambayo sasa hivi ndiyo Economic Power of the World.
 
kunena kwa lugha moja,maanake dunia nzima tuukubali ukweli sisi sote NI WAMOJA!tukikubaliana na hilo maanake hatutagombana tena,kwa sababu HATUNA CHA KUGOMBANIA,sisi wote si ni wamoja tayari?

sasa hili swala HALIWEZI KUTOKEA KWA KIZAZI HICHI.hebu turudi nyuma kidoooooooooooooooooooooooogo hata kama tutachelewa.karne kadhaa zilizopita watu walielewana kwa lugha wakawa na fikra 'motomoto' za kimaendeleo.wakajenga mnara ili wamfikie mungu.inaonekana walikuwa wanaukaribia UFALME WA MUNGU,mara akawavuruga.

sasa hebu fikiri:kizazi kile ambacho mungu alikuwa karibu nao,kwa dhambi zao chache tu HAKUTAKA WAMFIKIE,itakuwaje kwa kizazi hichi 'cha nyoka?'

mimi naona haiwezekani!HISTORICAL POINT OF VIEW INATUHUKUMU!
 
WomenofSubstanc
user_online.gif

WomenofSubstanc has no status.
JF Senior Expert Member
Join Date: Fri May 2008
Posts: 1,708
Thanks: 1,664
Thanked 1,429 Times in 784 Posts
Rep Power: 24
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Credits: 3,139,250


icon1.gif
Re: LUGHA MOJA ITAWALE ulimwengu?

Quote:


... kwa maoni yangu naona itakuwa ngumu.... chukulia mfano wafaransa walivyo na kiburi na lugha yao.QUOTE]

WOMENOFSUB,
Kusema itakuwa ngumu haimaanishi haiwezekani.
Pia nataka hii huu mtindo wa LUGHA YAO, tuumalize




Mkuu..kuwa ngumu nina maanisha kuwa na changamoto..inawezakana though..changamoto mojawapo ndo hiyo ya ku resist.
__________________
"It's far better to tell the truth and be rejected, than to hold
it back and be accepted"
MFANO WAKE NI KUWA MTU HAONEKANI KUWA NI MSOMI HADI ASEME KINGEREZA MIMI NADHANI UKOLONI UNATUSUMBUA KABLA YA KUCHAGUA HIYO LUGHA MNAYODAI ITUMIKE DUNIA NZIMA.
 
Nawaza kuwa ingekuwa vema kukawa na lugha moja ambayo itakuwa ndiyo Lugha rasmi ya ulimwengu wote.
Kuwepo kwa Lugha moja rasmi ya ulimwengu, kungeleta faida zifuatazo:-

Kurahisisha mawasiliano.
Kujenga umoja wa kimataifa.
Kufanikisha ueneaji wa tekinolojia ulimwenguni.
Kupunguza dhana ya ukabila na ubaguzi wa kimataifa.

Exaud,
Lugha ni sauti za nasibu......, hakuna watu waliokaa na kupanga sasa tuwasiliane kwa kiswahili au kingereza.

Lugha hukua na kuenea kutokana na matumizi na wingi wa watu. Wazo la kuwa na lugha moja kinadharia ni zuri ila kwa vitendo ni kitu ambacho hakiwezekani!
Kinachowezekana ni kuwa na lugha moja inayotumika kwa wingi sehemu mbalimbali duniani mfano kingereza.

Kwa sasa dunia ni kama kijiji na kujifunza lugha ya nchi nyingine ni jambo rahisi sana, hivyo msukumo kwa sasa uko kwa mtu mmoja kujifunza lugha ya mwingine ili kuweza kurahisisha mawasiliano, kujenga umoja na ueneaji wa technolojia. Sidhani kama ubaguzi ungepungua kwa na lugha moja kwa sababu kubagua ni silka ya mtu.
 
Nawaza kuwa ingekuwa vema kukawa na lugha moja ambayo itakuwa ndiyo Lugha rasmi ya ulimwengu wote.
Kuwepo kwa Lugha moja rasmi ya ulimwengu, kungeleta faida zifuatazo:-

Kurahisisha mawasiliano.
Kujenga umoja wa kimataifa.
Kufanikisha ueneaji wa tekinolojia ulimwenguni.
Kupunguza dhana ya ukabila na ubaguzi wa kimataifa.


KUNA LUGHA INAITWA KIESPERANTO ZAMANI TULIAMBIWA KUWA NI LUGHA ITAKAYOKUWA IKIIUNGANISHA DUNIA...
SINA UHAKIKA SANA NA HILI
LAKINI MZEE PITIA KWENYE HILI DIRISHA ILI UPATE MENGI KUHUSIANA NA HILI Swahili
 
Back
Top Bottom