Ludewa wamshukuru Rais Samia kuidhinisha bilioni 977 kuboresha elimu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wilaya ya Ludewa inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kuipatia fedha Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa milioni 977,600,000/= chini ya mradi wa Boost katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.

Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imepokea fedha hizo tarehe 24 Aprili 2023 na fedha hizo zimegawanywa kama ifuatavyo:

1. Kata ya Mavanga imepokea fedha ya kujenga shule ya msingi mpya eneo la Ruhuhu Darajani kiasi cha jumla ya shilingi milioni 347.5. Aidha shule ya msingi Mbugani imepokea kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya choo.

2. Kata ya Ludewa imepokea fedha ya kujenga madarasa 2 ya elimu ya awali katika shule ya msingi Ludewa Mini kiasi cha Jumla ya shilingi 69,100,000/=

3. Kata ya Milo imepokea fedha ya kujenga madarasa 3 a matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Mapogoro kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000/=

4. Kata ya Ludende imepokea fedha ya kujenga madarasa 3 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Maholong' wa kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000/=

5. Kata ya Mlangali imepokea fedha ya kujenga madarasa 4 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Mangali kiasi cha jumla ya Shilingi 106,000,000/=

6. Kata ya Mundindi imepokea fedha ya kujenga darasa 1 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi elimu maalum Mundindi kiasi cha jumla ya Shilingi 31,000,000/=

7. Kata ya Lupingu imepokea kiasi cha fedha cha jumla ya shilingi 181,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3, ujenzi wa matundu 3 ya choo na nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi Nindi.

FyWIh57WIAEN7ay.jpeg

FyWIh5_X0AA2w81.jpeg
 
Back
Top Bottom