Mbunge wa Monduli na Waziri mkuu aliejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa ni miongoni mwa wabunge wachache ambao ni nadra sana kumsikia au kumuona akizungumza au kuchangia hoja bungeni.
Tangia kujiuzulu kuwa Waziri mkuu mwaka 2007 Mh Lowassa hajawahi kuchangia kwa kuongea hoja bungeni zaidi ya mara mbili.
Lowassa km tumjuavyo sio mtu muongeaji sana na hata hoja nyingi bungeni huchangia kwa maandishi,lakini amekuwa akiongea kwa kupitia media mbalimbali na ktk matamasha na harambee huku akijiita kuwa yeye sio mtu wa maneno ila ni wa vitendo.
Sijajua kwanini mh Lowassa hukwepa kuongea Bungeni lakini hupenda kuongea na waandishi wa habari. Km ktk kile kipindi cha Semenyu wa ITV kinachorushwa kila Jumatatu saa 3:00 usiku.
Tangia kujiuzulu kwa Mh Lowassa binafsi niliwahi kumsikia akiongea bungeni mara mbili. Na mara zote baada tu ya kusimama utasikia baadhi ya Wabunge wakimshangilia. Mara ya kwanza ni pale alipotoa kauli akiishauri serikali ichukuwe MAAMUZI MAGUMU.
Mara ya pili ni jana wakati akimuunga mkono waziri LUKUVI ktk hoja iliyoibuka baada ya Mbunge wa Cdm Susan Liymo kuuliza swali kuwa ni lini serikali itawaleta nchini wataalamu wa kutengeneza na kuzuia mvua nchini km ilivyoahidi?
Akijibu swali hilo waziri Huviza aliwataka wananchi wasidanganyike kwa kuwa hakuna mwarobaini wa kuzuia na kutengeneza mvua isipokuwa ni kutunza mazingira.
Kauli hiyo ilimfanya Lukuvi kusimama na kusema,ni kweli Waziri mkuu aliejiuzulu(Lowassa) aliwahi kufanya ziara nchini Thailand na sio Malesia km Waziri Huviza na Susan walivyodai.
Lukuvi alisema kuna utaalamu huo na Lowassa aliwaomba wataalamu hao waje kufundisha wataalamu wa Tanzania teknolojia hiyo lakini ilishindikana kutokana na Tanzania kutokuwa na fedha.
Hata hivyo Mwenyekiti wa bunge Jenister Muhagama aliwataka mawaziri hao kukutana kupata jibu sahihi maana wananchi hawajui nani anasema ukweli.
Wakati Muhagama akitoa maelekezo hayo ndipo aliposimama Mh LOWASSA na kusababisha Bunge kulipuka kwa shangwe. Lowassa alisema; "Alichokisema Waziri William Lukuvi ndicho sahihi" akamaliza na kukaa.
Kushangiliwa kwa Lowassa kila mara anaposimama kuzungumza bungeni je inaashiria nini? Au kwa kuwa sio kawaida yake kuzungumza kwa hiyo kila mbunge anataka kusikia atakachozungumza?