Lowassa, Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Kwa ndugu zangu wanaosoma biblia, nilikuwa ninasoma kitabu cha Mathayo 11. Nikafikiria sana uwiano wa habari za Yesu na Yohana Mbatizaji na Lowassa baada ya kufika kwenye hizi aya:

2 Yohane mbatizaji akiwa gerezani alipata habari juu ya matendo ya Kristo. Basi, Yohane akawatuma wanafunzi wake, 3 wamwulize: "Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?" 4 Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona: 5 vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa na viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. 6 Heri mtu yule asiyekuwa na mashaka nami."

N.B: Truly speaking, sioni kama Lowassa ana afya nzuri kwa sasa, anasahau hata maneno anayotaka kuongea (sijui ndio parkinson disease? au Alzeihmer - early onset, lakini bado hili haliondoi mantiki ya kwamba Rais ni taasisi, inayochaguliwa na wananchi. Ikiwa watu wanaabudu mawe na miti, nani utakayekataa Lowassa akichaguliwa kuingia ikulu?
 
Kumwingiza Lowassa Ikulu Ni Sawasawa Na Kumtoa Baraba Gerezani Na Badala Yake Kumsulubisha Yesu....!
 
Kumwingiza Lowassa Ikulu Ni Sawasawa Na Kumtoa Baraba Gerezani Na Badala Yake Kumsulubisha Yesu....!

Lakini kumbuka kuwa Baraba alitolewa gerezani na YESU akasulubiwa ili neno litimie na mwanadamu apate kupona!
Sasa ni saa ya ukombozi, nia na madhumuni ni kuufuta mfumo muflisi wa mabwanyenye wa CCM.
Yes we CAN... lets make CHANGES that will prevail a signal for BELIEVing in new Revolution!
CCM ing'oke kwanza!!!
 
👏👏👏🙌🙌🙌

Nendeniiiiiiiii mkawaambie CCM, vipofu wanaona, viziwi wanasikia, viwete wanatembea na maskini wanahubiriwa habari njema..... nimeona haya kwa macho yangu, tokea Dar hadi Mbeya

Lowassa ndio YEYE, HAKUNA MWINGINE... Mkombozi wetu, Mfalme wetu... Mwana wa Mungu...!!!

Hadi sasa 95% hawana MASHAKA NAYE.....heri yao waliokombolewa...!!!

Kawaambieni CCM haya yanayotokea...

Mungu kajidhihirisha kupitia Lowassa...!!!

👉👉👉👉 Tuombee 👈👈👈👈👈

Eeeh Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, muumba wa viumbe vyote na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, tunaomba UMLINDE NA KUMPA NGUVU NA AFYA TELE MKOMBOZI WETU LOWASSA, MWANAO MPENDWA, ULIYETULETEA, UILINDE UKAWA KWA NGUVU ZAKO ZOTE NA VIONGOZI WAKE NA WANANCHI WAPATE KUONA UKOMBOZI HUU....

Eeeh Mungu baba, UA na ITEKETEZE KABISA NA KUIZIKA CCM, IPELEKE JEHANAM, kuzimu na uitoe kabisa katika akili za watanzania, na kuifuta hata katika kizazi kijacho, Mungu nakuomba usikie maombi yetu na UFANYE HIVYO...!!!

Amen....!!!
 
Lakini kumbuka kuwa Baraba alitolewa gerezani na YESU akasulubiwa ili neno litimie na mwanadamu apate kupona!
Sasa ni saa ya ukombozi, nia na madhumuni ni kuufuta mfumo muflisi wa mabwanyenye wa CCM.
Yes we CAN... lets make CHANGES that will prevail a signal for BELIEVing in new Revolution!
CCM ing'oke kwanza!!!

Ila mjue tu ya kwamba hao mafarisayo watamsulubisha kwa mara ya pili; ya kwanza pale dom na ya pili kwenye bvr. Chungeni sana kauli zao hao sio za bure kwa maana ipo hila kuu iliyojificha mumo hawategemei kura za wananchi kushinda. Wala hawasemi bure mnatumia oili chafu injini zinakaribia kunoki mara wengine ushindi lazima mara tunangoja ienaiena, nk. Lipo jambo limejificha; nyie mnacheka na mafuriko wao wanacheka na bvr. Hivi hiyo orodha ya wapiga kura imetolewa soft copy na kupewa vyombo huru na nakala zingine vyama vya siasa? hizo bvr anakaa nazo nani? haiwezekani kufuta majina na kuandika mengine mapya ambayo yatapiga kura kwenye vituo vya siri au kujazia kura vituo vikishafungwa? nani atasafirisha masanduku? vyombo vya dola vimepewa maelekezo gani? nyie chekeleeni tu mafuriko wameshasema mtashangaa wameshindashindaje.
 
Kawambie ccm mambo unayoyaona na kuyasikia,makada wa Ccm wanahamia ukawa, Lowasa ndiye habari ya mjini, mikutano ya ukawa inajaa watu maelfu, makufuli habari zake hazisikiki tena, mbowe kapona yupo fiti na ikulu IPO karibu kabisa na ukawa!
 
Ila mjue tu ya kwamba hao mafarisayo watamsulubisha kwa mara ya pili; ya kwanza pale dom na ya pili kwenye bvr. Chungeni sana kauli zao hao sio za bure kwa maana ipo hila kuu iliyojificha mumo hawategemei kura za wananchi kushinda. Wala hawasemi bure mnatumia oili chafu injini zinakaribia kunoki mara wengine ushindi lazima mara tunangoja ienaiena, nk. Lipo jambo limejificha; nyie mnacheka na mafuriko wao wanacheka na bvr. Hivi hiyo orodha ya wapiga kura imetolewa soft copy na kupewa vyombo huru na nakala zingine vyama vya siasa? hizo bvr anakaa nazo nani? haiwezekani kufuta majina na kuandika mengine mapya ambayo yatapiga kura kwenye vituo vya siri au kujazia kura vituo vikishafungwa? nani atasafirisha masanduku? vyombo vya dola vimepewa maelekezo gani? nyie chekeleeni tu mafuriko wameshasema mtashangaa wameshindashindaje.

Huwezi kumshinda adui yako siku zote kwa mbinu zile zile kwenye jambo hilo hilo labda naye awe zuzu. Tatizo hapa siyo wizi wa kura bali katiba yetu mbovu inatumika kuhalalisha wizi. Haiwezekani matokeo ya ushindi wa uraisi yasihojiwe mahakamani hata kama mshindi katumia njia zisizo halali kama kuiba kura n.k. na kama watalazimisha kuiba kura kwa makusudi basi tuwe tayari kushudia na pengine kuwa wahanga was machafuko kama ilivyotokea Kenya 2007. Maana haki isipopatikana mahakamani watu hulazimika kutafuta nje ya mahakama!
 
Huwezi kumshinda adui yako siku zote kwa mbinu zile zile kwenye jambo hilo hilo labda naye awe zuzu. Tatizo hapa siyo wizi wa kura bali katiba yetu mbovu inatumika kuhalalisha wizi. Haiwezekani matokeo ya ushindi wa uraisi yasihojiwe mahakamani hata kama mshindi katumia njia zisizo halali kama kuiba kura n.k. na kama watalazimisha kuiba kura kwa makusudi basi tuwe tayari kushudia na pengine kuwa wahanga was machafuko kama ilivyotokea Kenya 2007.
Hawapo tayari kubadili katiba! mioyo yao imekuwa migumu! wakati ni huu!
 
Tume wameandaa wao! maoni ya wananchi yametolewa! wameyakataa! Je, tusemeje sasa?
 
Na wasije wakadhani majeshi yetu wote in ccm watakuwa wamechemka sana ndiyo maana zikitokea fujo kubwa has a zinazotokana na matokeo ya uchaguzi wa rais hata baadhi ya wanajeshi au polisi wanakuwa neutral au wanahamia hata upande wa pili maana siyo wote wanaamini au ni washabiki wa wizi au dhuluma inayotendeka wakati huo!
 
Huwezi kumshinda adui yako siku zote kwa mbinu zile zile kwenye jambo hilo hilo labda naye awe zuzu. Tatizo hapa siyo wizi wa kura bali katiba yetu mbovu inatumika kuhalalisha wizi. Haiwezekani matokeo ya ushindi wa uraisi yasihojiwe mahakamani hata kama mshindi katumia njia zisizo halali kama kuiba kura n.k. na kama watalazimisha kuiba kura kwa makusudi basi tuwe tayari kushudia na pengine kuwa wahanga was machafuko kama ilivyotokea Kenya 2007.
Hilo la machafuko tuliweke pembeni kidogo wala sidhani kama tumeshafika huko la maana kuchukua hatua stahiki kuona daftari linawekwa wazi na linahakikiwa ipasavyo vinginevyo wasulubiwe haohao tume na wala sio kuvuruga amani ya nchi. Hatua zikichukuliwa mapema na wadau wote kulitolea kauli litakaa sawa tu
 
Mr. President umenifurahisha sana vile tu natumia kitochi ningekupa like, umeandika vema sana! Nikakumbuka ulivyopotea ghafla EL alivyokatwa na maccm lkn sasa hivi umerudi full force.....
 
Last edited by a moderator:
Hilo la machafuko tuliweke pembeni kidogo wala sidhani kama tumeshafika huko la maana kuchukua hatua stahiki kuona daftari linawekwa wazi na linahakikiwa ipasavyo vinginevyo wasulubiwe haohao tume na wala sio kuvuruga amani ya nchi. Hatua zikichukuliwa mapema na wadau wote kulitolea kauli litakaa sawa tu
Kimsingi hakuna raia mwema was nchi yoyote ile anatamani nchi take iwe kwenye machafuko pengine hata vita. Watu wamelazimishwa na mifumo kandamizi iliopo madarakani kwa wakati huo kufikia hatua ya machafuko na mifano imejaa chungu nzima hapa afrika achilia mbali duniani. Na sisi hatuna tofauti kubwa sana na nchi hzo. Hivyo time ya taifa ya uchaguzi isicheze na maisha wa watanzania kwa kutufikisha hatua hiyo! Tume za uchaguzi ktk nchi mbali mbali zilizokumbwa na machafuko ndio chanzo kikuu cha kuleta Fujo na machafuko. TUNAMUOMBA SANA LUBUVU NA TUME YAKE KAMA KWELI NI WAZALENDO WA NCHI HII BASI ATENDE HAKI KWA WATANZANIA. YASIJE YAKAMKUTA YA KIVUITU WA KENYA.
 
Back
Top Bottom