Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Katika kuonyesha kuwa CCM inahofu katika uchaguzi mdogo wa madiwani, magari zaidi ya 10 ya jeshi la Polisi mkoa wa Arusha yamezunguka nyumba ya Lowasa ambae ni waziri Mkuu mstaafu na kuzuia msafara wa Magari na pikipiki kuelekea kata ya Musa wilaya ya Arumeru kumnadi mgombea udiwani.
Tukio hilo limejiri Leo j3 kuanzia majira ya SAA 9 alasiri ambapo Polisi wenye silaha na mabomu walitanda nyumbani kwa Lowassa Monduli, kwa lengo la kumzuia asiende kwenye Mkutano wa kampeni kumnadi mgombea udiwani.
Aidha wafuasi wa CHADEMA waliomfuata kumpokea wakiwemo viongozi walizuiwa na Polisi huku Katibu mwenezi wa jimbo John Seneu au Jombii akitiwa mbaroni na Polisi.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni hofu kwa CCM zinazopelekea kutumia vyombo vya dola vibaya
Kudhibiti siasa za CHADEMA kwa maslahi ya wagombea wa CCM, huu ni uonevu mkubwa kwa mustakabali wa taifa letu na unapashwa kukemewa na kulaaniwa.