Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi

Naomba ufafanuzi, ni waziri mkuu MSTAAFU au waziri mkuu aliyejiuzulu?? Samahani kwa swali langu
Huwezi kupata jibu.tathmini yenyewe ni very simple and poor.ila washabiki na wazungusha mikono wa ukawa ambao wako rundo humu ndani watakutukana bure brother. Magu ni zawadi ya watanzania toka kwa mungu..hiyo kasi,ari na hamasa ya EL siioni mitaani zaidi ya humu ndani..
 
Kweli umenena: katoka kwa mungu. Tungebarikiwa zaidi kama nchi endapo angekuwa ametoka kwa Mungu wetu aliye hai.
 
Hebu wajuzi mtujuze, Kaaya ndio lilikuwa jina la kaka yetu? Kaaya ni jina la Kimeru au Kimasai
 
Lowassa autathimini mwaka mmoja baada ya uchaguzi.

Tarehe Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.

Naamini nilileta sura na msisimko mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana yake ni nini.

Napogeuka nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.

Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.

Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi, tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

Pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.

Nawashukuru sana wananchi kwa imani kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla. Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwengine, kwa hiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza. Kasi, nguvu, ari na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.

Edward Lowassa

Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe kamati Kuu CHADEMA.

Note ÷Tarehe kama ya leo mwaka jana...Watanzania tulifanya mtihani wa hesabu (uchaguzi)...na sasa tunaendelea kuisoma namba....wale wa kanga na pilau za uchaguzi kimyaaa
Paka shume ni nani?

Kweli umenena: katoka kwa mungu. Tungebarikiwa zaidi kama nchi endapo angekuwa ametoka kwa Mungu wetu aliye hai.
Hahahahahahaha kiongozi utaamini tu baadae ya kwamba ameletwa na mungu aliye hai..hii inatokana na kuwajali walokuwa hawana haki,wanyonge,na wenye mahitaji muhimu.tunaopiga makelele ni sisi ambao mirija ya kinyonyaji imekatwa aidha moja kwa moja au kupitia jamaa zetu
 
Ok. Ngoja tumpe muda.
 
Back
Top Bottom