Live Updates: Yanayojiri bungeni Dodoma, leo tarehe 17 Juni 2014

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,782
336
Kikao cha bunge la bajeti kinaendelea tena leo ambapo kwa ratiba inavyoonyesha kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu kisha mjadala wa bajeti kuu ya serikali utaendelea.....stay tune for live updates...mwanzo mwisho.

===updates..
swali kwa ofisi ya waziri mkuu.
mh. Augostino lyatonga mrema anamuuliza waziri mkuu, katika mji wa himo kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya makazi ambapo sasa serikali inataka kuyatumia maeneo hayo kuweka viwanda.
je, ni nini athari za viwanda kujengwa kwenye makazi ya watu?
je, serikali itakuwa tayari kuwafidia wananchinambao makazi yao yataathirika?

naibu waziri wa tamisemi anaendelea kujibu maswali haya.

===updates
mh.victor mwambalaswa amemuuliza waziri mkuu
Mkuu wa wilaya ya chunya aliunda tume ya kuchunguza ubadhirifu katika uendeshaji wa ushirika wa tumbaku wilayani na matokeo ya uchunguzi yameshawasilishwa kwa mkuu wa wilaya, je nini matokeo ya uchunguzi huo? Waziri anafafanua.

===clara mwatuka anamuuliza wwairi wa utumishi.kwamba sharti mojawapo katika kulipa malimbikizo ya mishahara ya watumishi ni pamoja na kukubali cheo au daraja...,je, imewahi kutokea kwa mtumishi yeyote kukataa cheo? Waziri pamoja ufafanuzi anasema haijawahi kutokea mtumishi kukataa cheo.

====swali kwa wizara ya uchukuzi
betty machangu anamuuliza waziri wa uchukuzi , serikali kupitia SUMATRA imetangaza kuwa mabasi yanayotoka mikoaninkwenda dsm hayahitaji kuingia kwenye stend ndogo kwenye halmashauri ambapo stend hizo zimejengwa kwa gharama kubwa? Na hatua hiyo si itapunguza mapato kwa halmashauri? Serikali ifute waraka huo....
---naibu waziri anasemakuwa amri hiyo ni kwa mabasi makubwa tu na ni kwa mabasi ambayo hayana abiria wanaoshuka katika maeneo hayo. Aidha kuhusu suala la mapato mabasi hayo yanapita mizani ambazo serikali imejenga kila mkoa hivyo mapato yapo pale pale.

====swali kutoka kwa rachel mashishanga...mwaka 2012/013 serikali ililipwa bima ya ajali ya ndege iliyotokea mwanza ambapo iliahidi kununua ndege zingine lakini haikufanya hivyo......waziri anasema nia ua kutekeleza azma hiyo ipo pale pale ingawa fedha hizo hazijalipwa zote kama ilivyotakiwa kuwa.
===waZiri anasema ipo kampuni ambayo itaanzisha safari za ndege kutoka dsm- dodoma - arusha dar kwa gharama nafuu
===anne kilango ameuliza swali kuhusu ndege za kenya kuutangaza mlima kilimanjaro ambao uko tz, je nini mantiki ya hili? Mwanashera mkuu wa aerikali anafafanua kwamba kenya haina makosa kwa sababu sisi tz hatujaanzisha matangazo ya namna hiyo na pia kenya kijiografia ipo karibu na mlima kili.

====updates
mjadala wa bajeti ya serikalinumeanza na mchangiaji wa kwanza ni peter serukamba ambapo anaishangaa serikali kuwa descourage wawekezaji wa ndani na kuwakumbatia wale wa nje.....anasema serikali ije na majibu ya matatizo ya wananchi
====sasa anachangia sugu
anaanza kwa maneno kwamba ipo slogan ya kusema vijana waache kulalamika anasema vijana wataendelea kulalamika mpka kieleweke
===anasema tuhamasishe biashara ndogo ndogo.....tu promote small businesses.
===sugu anasema kwa kuhamasisha biashara ndogo ndogo itafika wakati hata wanafunzi wa vyuo vikuu kufanya kazi yaani temporary employment ie tempo.
===sugu anazungumzia maslahi kwa madaktari, esp on call allowance, posho mbalimbali, kuchelewa kuthibitishwa kazini, malipo ya arriers,fedha za likizo.
==anazungumzia ishu ya house allowance kwa wafanyakazi wa serikali esp madaktari...anasema serikali haiwezi kujiondoa kwenye house allowance kwa wafanyakazi
===madaktari wanalalamika juu ya fursa za kusoma kutoka kwa upendeleo,
=== hospitali za rufaa, huduma za x-ray hamna hospitali ya rufaa ya mbeya......mbeya hosp ina majengo mazuri ya ghorofa kwann hakuna vifaa?? Au mnataka waziri awe mnyakyusa ndio hili jengo limaliziwe?

===++=more updates
diana chilolo anachangia sasa, anaeleza kwa uchungu kuhusu hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida ambayo hadi sasa haijakamilika...anasema kwanini serikali isiingilie kati imalizie hospitali hiyo badala ya kuwaachia wananchi wa singida peke yao
===anazungumzia kodi kwa wafanyakazi, kwamba kodi ya 12% ni kubwa mnoooo
===amezungumzia bima ya afya kuwa ipanue wigo wa watu wanaopaswa kuhudumiwa katika familia na mfuko huo kwamba tegemezi nao waingizwe
===anasema kila kitu nchi hii ni kuchangia kuchangia tuuje ni kitu gani ambacho tunawapa watz bure??

====
=====hivi sasa amesimama asumpta mshama, anasema anashukuru serikali kujenga barabara ya bunazi katoma kasenye nk japo kuna mapungufu anaomba yarekebishwe, umeme maeneo ya mtukula, hospitali na vituo vya afya na zaidi anashukuru kupelekwa ambulance katika hospitali ya wilaya yake.

===updates
anayeongea hv sasa ni leticia nyerere
anasema kuwe na vivutio na hamasa kwa walipa kodi hapa nchini kama ilivyo kwa nchi zilizowndelea, anasema nchi hizo zina utaratibu wa mlipa kodibkujaza fomu maalumu ya kulipa kodi kisha hulipwa kama zawadi au motisha.
===anasema tuwe wazalendo kwa taifa na tuwe na utamaduni wa kushukuru kwa kile kinachofanywa na serikali, kwamba ukiwa mjuaji sana halafu ujuaji wako usiwe na maana kwa wananchi kama hakuna la maana ulilofanya.

====sasa anachangia mh.rajab mbaruk,yeye alianza kwa kusifu kuwa pemba yote inaongozwa na wabunge kutoka chama cha wananchi cuf akimjibu naibu spika aliyetambulisha viongozi wa ccm wilaya ya kongwa.
===anasisitiza kudai risiti pindi ukinunua bidhaa lakini kuna udhaifu katika hilo hivyo mamlaka ya kodi nchini iangalie upya jambo hili.
====anasema ana imani na mawaziri wa fedha hasa mwigulu jinsi alivyoonyesha makeke kuishughulikia cuf na chade,a lakini je ataweza kuwashughulikia mafisadi waliojaa serikalini??

====updates
esther matiko ameanza kwa kuilaumu serikali kwa ongezeko dogo la mshahara wa mfanyakazi na punguzo dogo sana la kodi kwenye mshahara wa mfanyakazi.
===anasikitikia kutelekezwa kwa sekta ya sanaa na wasanii hapa nchini, ambapo nchi kama nigeria zimeipa kipaumbele sekta hii na kuifanya kuwa chanzo kikuu cha mapato ya nchi, pia kilimo
====anasema seikali inaishia kucheza na takwimu huku mambo yakiharibika na uchumi unadidimia.
===anachangia rage hivi sasa....anazungumzia deni la taifa kwamba wizara ya fedha na wataalam wanajitahidi kufanya kazi

===amos makala anatoa taarifa kwa bunge kufafanua kauli ya esther matiko kuwa tangu uhuru serikali imewapatia maji watu 500,000 tu, makala anasema usahihi wa kauli hiyo ni kwamba kila mwaka werikali inawapatia wananchi 300000 - 500000 maji safi na salama anasema yuko tayari kuongozana na matiko kwenda kwenye vijiji alivyosema havina maji kutatua kero hiyo.
====cyril chami amesema kuwa wananchi walioko jirani na hifadhi hawanufaiki na mapato ya hifadhi hizo mf mlima kili,tarangire na sehem zingine

===updates
ridhiwan kikwete anaongea hv sasa,anasema naye anaungana na mbaruk kuwa wananchi wanaozungukwa na hifadhi za taifa hawanufiki nazo.
===anazungumzia micro finance banks,saccos na masharti yao magumu ya mikopo
===anasema saccos zisamehewe kodi
===anasema sekta binafsi ipewe kipaumbele
=====anapigia upatu bandari ya bagamoyo
===kuhusu misamaha ya kodi ni sawa lakini tuangalie maeneo ya kusamehe, kwamba vifaa vya ujenzi mfano bati zisamehewe
===kwenye kilimo anashangaa eti kilimo kinachangia 4% tu ya pato la taifa...kichekesho hiki wakati nchi nzima ni mashmba
===anasema tusizungumzie kukua kwa uchumi kwenye vitabu tu, hali halisi ya maisha ya wananchi haina uhusiano kabisa na takwimu hizo za kwenye makábrasha...

naib spika anampongeza ridhiwan na anasema like father like son.

===more updates
majadiliano ya hotuba ya bajeti yanaendelea hivi sasa jioni hii, alianza mh.hadji mponda ambaye alizungumzia suala la barabara za jimbo la ulanga magharibi, na kilimo cha umwagiliaji morogoro.
===sasa anachangia mh elizabeth batenga.ambaye ameanza kwa kuishangaa serikali kupuuzia suala la afya za wananchi hasa kitengo cha uzazi ambapo ukienda wodi za wazazi/kina mama wanaojifungua ni msiba mkubwa....kina mama wawili kitanda kimoja huku wengine wakilala chini.
===mbunge anazungumzia suala la malipo kifogo sana ya pension kwa wastaafu akitolea mfano kwa wanajeshi ambao hustaafu huku wakiwa na umri mzuri ie dio mkubwa sana pamoja na kukabiliwa na majukum makubwa ya kifamilia.

===updates
betty machangu anaipongeza serikali kwa kupunguza kiwango cha kodi kwa wafanyakazi
pia anaipongeza kwa kuongeza/kupandisha mshahara wa mfanyakazi

===updates
ni vicent nyerere sasa...ameanza kwa kumpongeza chenge kwa kuwa muwazi kuwa serikali haisikiii.....
===anasema serikali tuhamasishe uwekezaji wa ndani, kwa kuanza tungeanza na kiwanda cha matairi kwani soko lake ni kubwa hata serikali tu inatosha
===anasema mabadiliko ya baraza la mawaziri hayakuwa na tija kwani kilichofanyika ni kubadili sura tu kwani tatizo mfano la ukaguzi bandarini halijabadilika
===Anamshangaa waziri wa mambo ya ndani kuomba fedha kwenye bajeti inayotokana na kodi kwa ajili ya kulisha wafungwa!!!!!!!!! Anasema yeye angekuwa waziri angeomba matrekta ili wafungwa wakalime wazalishe chakula.
===anashangaa sana tumekuwa watu wa kulalamika tuuu mimi nyerere nilalamike, spika alalamike, riziwani naye alalamike tunaenda wapi kma taifa???????
====anashangaa mawaziri kuomba bajeti hapa hadharani lakini hawaleti majibu ya matumizi kwa uwazi.

===updates
said nkumba anachangia na ameanza kwa kuipongeza wizara ya afya kwa kufuatilia maagizo ya katibu mkuu wa ccm kwa kwenda kusikiliza kero za wananchi
===anazungumzia upungufu watumishi ktk ofisi za umma hasa halmashauri na pia upungufu wa zana kilimo hasa pembejeo za kilimo.
===anazungumzia udhaifu mkubwa uliopo kwenye hifadhi za taifa anasema ni bora baadhi ya hifadhi ni bora maeneo hayo yagawiwe kwa wananchi watumie kwa shughuli za maendeleo km kilimo.
===amezungumzia suala la maji kwa ujumla kuwa wizara imejitwhidi lakini bado kuna haja ya kuongeza jitihada
===anampongeza mh rais kwa tamko lake hivi karibuni akiwa tabora kuhusu ubadhirifu katika vyama vya ushirika..
 
serukamba anasema matumizi ya serikali ni makubwa. ma - CCM bwana. Jana nilimsikia shekifu naye anasema hivihivi.

Serukamba anamsema bwana kikwete kiaina, kwamba maneno kwenye reli ya kati ni mengi sana, hivi ahadi ya rais ilikuwa vipi kwenye hii kitu.

Ma CCM Bwana.

Hivi hayana vikao vingine vya kuielekeza serikali zaidi ya kuja kuongea ongea na kujipendekeza pendekeza Bungeni, si yanasema ndo yanaongoza serikali.

Alafu anaonekana halipi Kodi ya Majengo, anasema serikali haikusanyi kodi ya majengo, hivi ma-CCM hayapeani hata taarifa yao yenyewe?

Lisikie, linasema twende kwenye PPP economy model, alafu linasema serikali haiheshimu private sekta, linasema tumeua mashirika yote, linamsema Muhongo na tabia yake ya kudharau wafanyabiashara wakati liliunga mkono bajeti ya Muhongo.

naona halijielewi,limeanza kusifia Kenya tena, alafu limetoka kusema tubadili mind set yetu.

Linakumbuka shuka wakati tumekucha halijui kama tumeamua kuyaondoa.

linaendelea, eti education imekufa hakuna anayejali, linaishangaa serikali kwa kuchukulia issue ya ajira sio tatizo, walah naacha kuangalia bunge haya majaa yanaudhi.

limesema linaunga hoja, limekaa
 
Sugu anaongea.
anatoa angalizo kwa watu wanaoongoza nchi kwa kulalamika. amegusia slogan mpya ya kuwataka vijana waache kulalamika, anasema vijana hawalalamiki bado wanafight.

Sasa anamwaga point za msingi
SMALL BUSINESSES (Hakuna li-CCM waziri, Rais wala li-Bunge limezungumzia hii kitu toka bunge hili lianze).

naona ilikuwa kidokezo tu, kazungumzia namna Marekani inavyotoa green cards kwa wageni waoenda kuanzisha small business huko, nadhani hapa kasahau na sisi tunavyokaribisha wachina.

Mama yangu,
-madaktari mbeya hawajapata call allowance kwa kipindi cha miezi sita,
-Kwamba madaktari wanafanya kazi bila kuwa confirmed hata kwa kipindi cha miaka sita, kumbe ma-CCM yanaongoza kibabe namna hii.
-Housing allowance - hivi Kikwete ameisharudisha zile nyumba?
-Mishahara inacheleweshwa
-Leave allowance wanazurumiwa
-Scholarship za kwenda kujiendeleza zinatoka kwa upendeo.

anakazia sasa, kwamba sio vijana tu wanaolalamika kama wanavyosema ma-CCM bali ni mpaka madaktari.

Naona anazungumzia mpango wa Maendeleo.
Kwenye Mpango wa maendeleo wamesema kuna mpango wa kukarabati chumba cha x-ray wakati kumbe kitambo kuna Jengo lilianza kujengwa na profesa mwakyusya ma-CCM wamelitekeleza, sasa anawakumbusha walimalizie.

Sasa anaelezea mazungumzo wake na mafriend yake mabanker.
sasa sugu anaelezea namna mashirika ya UMA yanavyopush interest rate kuwa kubwa.
 
Sugu anaongea.
anatoa angalizo kwa watu wanaoongoza nchi kwa kulalamika. amegusia slogan mpya ya kuwataka vijana waache kulalamika, anasema vijana hawalalamiki bado wanafight.

Sasa anamwaga point za msingi
SMALL BUSINESSES (Hakuna li-CCM waziri, Rais wala li-Bunge limezungumzia hii kitu toka bunge hili lianze).

naona ilikuwa kidokezo tu, kazungumzia namna Marekani inavyotoa green cards kwa wageni waoenda kuanzisha small business huko, nadhani hapa kasahau na sisi tunavyokaribisha wachina.

Mama yangu,
-madaktari mbeya hawajapata call allowance kwa kipindi cha miezi sita,
-Kwamba madaktari wanafanya kazi bila kuwa confirmed hata kwa kipindi cha miaka sita, kumbe ma-CCM yanaongoza kibabe namna hii.
-Housing allowance - hivi Kikwete ameisharudisha zile nyumba?
-Mishahara inacheleweshwa
-Leave allowance wanazurumiwa
-Scholarship za kwenda kujiendeleza zinatoka kwa upendeo.

anakazia sasa, kwamba sio vijana tu wanaolalamika kama wanavyosema ma-CCM bali ni mpaka madaktari.

Naona anazungumzia mpango wa Maendeleo.
Kwenye Mpango wa maendeleo wamesema kuna mpango wa kukarabati chumba cha x-ray wakati kumbe kitambo kuna Jengo lilianza kujengwa na profesa mwakyusya ma-CCM wamelitekeleza, sasa anawakumbusha walimalizie.

Sasa anaelezea mazungumzo wake na mafriend yake mabanker.
sasa sugu anaelezea namna mashirika ya UMA yanavyopush interest rate kuwa kubwa.

Hii Sericali ya SISIEM imetobolewa masikio hivyo haitaweza kusikia asilani.
 
Libunge la CCM Li-mama, limeanza kuongea
yaani sugu ametoka kuongelea matatizo kwenye sekta ya afya, hili li-CCM limeanza kwa kuwapongeza waliolifariji kwa kwenda kwenye utalii wa matibabu nchini india. wonders will never end, hivi ma-CCM hayajui hata pa kuanzia hotuba zao.

any way, likaendelea kwa kumsifia waziri wa fedha, alafu ghafla limeanza kulalamika kwamba Bilioni mbili hazikwenda kwa ajiri ya ujenzi wa hospitali ya rufaa huko singida? linaendelea kuihoji serikali, kwamba wananchi wa singida wameshirikiana na mkuu wa mkoa kujenga hospitali hiyo kwa nini serikali kuu haitimizi ahadi ya kupeleka pesa, linasema linaongea kwa uchungu sana juu ya jambo hilo, sasa na mimi naliuliza, japo usoni halioneshi uchungu kwa nini lilisifia mwanzo wakati linajua lina machungu? mi-CCM bwana.

Limeanza kuongea point, Kwamba watoto walio nje ya ndoa waruhusiwe kupata huduma za Bima ya afya? alafu badala ya kuongelea macro issue sasa limeingia kwenye operational issues, kwamba wanachama wa mifuko ya bima wanalipishwa kupewa kadi mpya kama wamepoteza.

Huyu mama huyu ameanza kuchanganya mambo, kwamba mshahara unakatwa vat, hii kaitoa wapi, eti wafanyakazi waondolewe vat sababu wanakatwa kila mahali, huyu mama nadhani alikuwa anaumwa sana bora alienda india.

kuna mbunge kajaribu kumrekebisha kwamba Aseme PAYE, yeye anasema ndo VAT hiyo hiyo, au ndo machungu yenyewe.

Yaani huyu mama anaishambulia serikali kweli kweli sasa
anauliza hivi, hivi serikali hii inatoa huduma gani bure,wakati kila kitu kinalipishwa,

Mamaaaaaaaaa, kaunga mkono hoja hahahahahahahaha anaitwa chilolo kumbe, Mi-CCM ni shida aisee.
 
Sasa kaja mwingine, ni mweusi unaweza kudhani ni raia wa Sudani kusini. naona anatokea maeneo ya Jirani na Uganda huko

Yeye kasema wazi amekuja kupongeza.

iiiiiiishi, kaanza kulalamikia barabara zikizo chini ya kiwango
anashukuru kupewa ambulance, na mambo meeeengi madogo madogo

Kahama tema, sijui anataka kuongea kila kitu?
Anazungumzia utekelezaji wa bajeti ya 2013/14
swali, Serikali inauhakika gani kwamba mwaka huu itakusanya mapato kama wanavyopanga wakati mwaka jana walishindwa? anaendelea na malengo na ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi? yaani maswali yake bwana? ndo amemaliza hivyi.

kaamia swali la mikopo? anataka kategories za mikopo, mi hata simuelewi, au labda ndo maana serikali haitekelezi?

Naona anaitwa Assumpter Mshana.

Sasa anauliza swali la msingi
kwamba serikali ilapata wapi kibali cha kukopa zaidi ya kiwango kilichohidhinishwa na Bunge?

sasa kaanza unafiki wake. kama kawaida yao, kwamba wananchi wake hawajaona faida ya kukua kwa uchumi, anaponda serikali sasa.

mi wananichanganya hao ma-CCM, ngoja nifanye mambo ya msingi aisee
 
na malalamiko yooooooote ya asumpter mshana, kaunga mkono hoja.
alafu huyu Naibu speaker anasema huyu mwanamke ni wa watu wa Jimbo la Kongwa, kivipi?
 
Huyu Letcia mbona kama anaongea kama kwa nyodo vile, kama mapozi vile, alafu kaweka shedo kama za Heaven on Earth.

Mi nimeishia kumuangalia tu, kasauti kake ni ka zuri, yaani anaongea kama mzungu.

Foreign currency, na vile kaisema Foreign corensi,

Anauliza, umewahi kusikia taarifa lililoendelea bila serikali kulipisha kodi wananchi wake?
anasema kulipa kodi Tanzania ni kama adhabu,

anatoa mfano hapa huko majuu wanahamasisha kulipa kodi namna gani,
Kwamba, kuna form mlipa kodi anajaza ili arudishiwe pesa zake kama amelipia kodi na nini na nini? au huyu dada analipwa huku alafu anakwenda kulipa kodi huko nje nini?

Kimsingi anazungumzia tax refunds, namuona waziri wa Fedha anamuangalia kwa makini kwelikweli, Bashe amtafute huyu Leticia ampe copy ya hii form.

Sasa ameanza kunichanganya sasa, anaponda watanzania kwamba hawalipi kodi lakini hatoi mfano wa yeye kutokulipa kodi,

stupid woman, eti anasema asante kwa serikali kupeleka maji na walimu.
 
Last edited by a moderator:
Kuna Mzanzibar anaongea hapa, kwani hii bajeti ni hadi ya huko?

Sasa anamjibu naibu speaker, anaelezea namna Pemba yote iko chini ya CUF.
Hii inaitwa ukishangaa ya Kongwa ya Pemba yanakuja, in fact huyu Ndugai kuna kipindi alikuwa anaongea mambo ya hovyo kuhusu Kongwa na CCM.

My goodness, kuna taarifa inatolewa na Lage, naona Bunge limekuwa derailed sasa,anazungumzia idadi ndogo ya watu wanaochagua viongozi pemba kulinganisha na Kongwa.

Toba, huyu Mzanzibar huyu, sasa anajibu, anasema anampa Lage mwenye asili ya Somalia ila ni Mtanzania, kwamba Burundi na China wote wana kiti kimoja umoja wa Mataifa.

Point hapa ni Kwamba Lage sio Raia.

Sasa ameanza Point
Anasema akiwaangalia akina Mwigulu Nchemba usoni haoni matumaini ya kuweza kupambana na ufisadi, masikini mwigulu na Malima na dada yao wanaangalia chini kwa aibu kama vitoto vya chekechea.

Kwamba, kuna madhaifu makubwa katika ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wanaoingiza mizigo nchini, anawauliza akina nchemba wataweza kudhibiti au anafiriki uzalendo ni kuvaa scuff.

Tobaaaaaa, anasema sasa Bahari imekuwa ni kama laana, kwamba tumepewa bahari ili iuwe wapemba na waunguja,

Ngoja kwanza
anasema ile meri ya wale wachina wa Magufuri imezama, imezama vipi? na anasema alipendekeza waichome kama ambavyo huwa wanachoma siraha zinazokamatwa kutoka kwa waarifu wakakataa, sasa imezama.

Hili swala la meli, limenichanganya, Kinana asijekuwa amechukua hii kitu.
 
Last edited by a moderator:
CCM MPs are totally confused. you can not have a long list of reservations on a certain subject and yet at the end of your contribution you support the same subject at a 100% rate.
 
PAYE

Ndo alivyoanza huyu dada Esther Matiko.

Na katika hili Mwigulu Nchemba ajue ameanza na mguu mbaya hizo mbio zake.

Huyu dada anaongea technical issues hapa, tax brackets, 9% 16% najua anaongea mambo ya msingi, anawaombea relief wafanyakazi, na amesema atapeleka amendments za tac brackets.

anapendekeza kukuza sekta ya sanaa na michezo, kwamba haikui, anatoa mfano wa Film industry huko kwa kina emenike/Nigeria.

Mpango wa maendeleo wa miaka mitano
Miradi 4 imekamilika
Miradi 12 iko katikati
Miradi 51 iko hohehahe
Miradi 12 haijurikani ilipo

ameirank kwa divisions,

Ohooo kahusisha failure hii na mianya ya ufisadi.

Mamaaaaaaaaaaaaa
Anasema serikali inacheza na Takwimu (Statistical Fraud)
Ayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, kwamba serikali imetoa taarifa bungeni kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja watu waliounganishwa na maji ni 1,500,000, alafu anasema katika kipindi cha miaka 50 iliyopita walikuwa 500,000 anauliza hii imewezekana vipi wakati wizara ya maji ilipata asilimia 27 tu ya Bajeti?

hapa Esther kawashisha ma-CCM maongooooooooooooooo, duuuuuuuuuuuuuuuuuu how can this be?? mamaaaa

Makala anaweka records sawa
Kwamba sio kweli kwamba katika kipindi cha miaka hamsini serikali imewafikishiwa maji wananchi laki tatu, bali serikali ilikuwa inawafikishia maji wanachi laki tatu kila mwaka.

hila hajajibu imewezekanaje kwa mwaka jana wananchi milioni moja na laki tano walifikiwa wakati wizara hiyo ilipata asilimia 27 tu ya bajeti, duuuuuuuuuuuuuu
 
Leo bungeni Ndg Ndugai akiwafahamisha wageni bungeni alipowafahamisha wageni kutoka Kongwa aliongezea kuwa kongwa kuanzia vijiji, wenyeviti ni ccm, kata madiwani ni ccm na mbunge wao ni ccm. na bunge likaendelea. Ilipofikia zamu ya mbunge wa Konde Pemba alimshangaa ndugai kushangaa jimbo moja kuwa na viongozi wa chama kimoja ccm tu. Alimwambia kama ataenda pemba sio jimbo moja tu bali majimbo yote tisa wabunge, madiwani na vijiji vyote huko Pemba waliochaguliwa ni CUF pekee. Ndipo ilimkuna Ndg Rage mbunge wa Tabora kutoa taarifa kuwa Pemba mbunge anachaguliwa na watu 70 tu huku Kongwa Mbunge anachaguliwa na watu zaidi ya 70,000. Akipokea taarifa hiyo ya kibaguzi alimkumbusha ndg Rage kuwa yeye ni kwa sababu ana asili ya Kisomali. Alimuomba afananishe wingi wa China na Burundi kuhusu kila mmoja kuwa na kiti sawa katika umoja wa mataifa My take: Kuna wengi akina Rage wanakaa bungeni kiushabikishabiki bila kujali maslahi ya Watanzania walio wengi maadam wao waliingia bungeni kwa hila na kununua wapiga kura.
 
Hii imekaaje wakuu, mbunge anapopewa nafasi ya kuchangia mjadala bungeni anaanza kwa kutoa shukrani kwa waliomuombea alipoenda kutibiwa India. Je haya ni matambo, au mikogo! Watu wanakosa huduma hapa nchini wamama hawana vifaa kwa ajili ya kuzalishiwa. Dawa hazipo. Mbunge anasema bila aibu wala huruma kwamba alienda matibabu India. Kwenye mijadala wananchi hawatetewi, isipokuwa kutetea serikari na mafanikio haya ya viongozi wetu kushindwa kutibiwa nchini kwenye hospital za kayumba. Tunasemaje?
 
Hili swala la meli, limenichanganya, Kinana asijekuwa amechukua hii kitu.

Hii hapa mbele ya MAGUFULI MWENYEWE......

magufuli.jpg
 
Rage sasa
Nilitoka kidogo.

Rage anaongea point hapa kuhusu issue ya kukopa. anaishawishi serikali iendelee kukopa kama kawaida.
anasema wabunge hawana expertise ya kujadili mambo ya kiuchumi kulinganisha na serikali, anasema hafurahishwi na kuwazalilisha ma-CCM wenzao.

Rage anaongea, kwamba moja ya tatizo la serikali ni kuingia mikataba ya ujenzi wa barabara kabla ya Bajeti, na kwamba mikataba hiyo imekaa vibaya sana kwa serikali pale inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kulipa wakandarasi, anadai ni asilimia sitini tu ya pesa za ujenzi wa barabara zilizokwenda, analalamika alafu anapongeza analalamika anapongeza, ngoja niende nae.

sasa anaongea kwa uzuni, kwamba mkoa wa tabora umepata asilimia 29 tu ya pesa za maendeleo, anaomba waziri wa fedha amuonee huruma hizo zilizobaki ziende.

sasa anaelezea TUWASA inavyodai idara serikali, na ni zilezile, Polisi,na Magereza, kama kawaida hazilipi hizi.

Anaishukuru wizara ya umeme.

Safi, Ndugai anaulizia kuhusu furugu za simba.
Kafanya usanii.

kiufupi alikuwa anajipendekeza pendekeza ukiacha point ya muhimu kwa serikali kuingia mikataba kabla ya bajeti, au kuwa na pesa, sababu inaongeza madeni bila sababu za msingi.
 
Sasa ni Mbunge wa
Sijui ni lecturer huyu jamaa

Anaelezea efficiency - the use of minimum resources
Fairness - kwamba ni equitable distribution of resources
Sustainability - uchumi wetu ni endelevu

anazungumzia five steps of economy, yaani ni kam vile yuke kwenye interview ya kazi, Kikwete Muangalie huyu jamaa kwenye mabadiriko yajao.

Sasa anazungumzia Paymaster General, mamaaaaa huyu Jamaa anamuita Utoh pathologist, sasa ananichanganya He is talking of too much things at Pa, wanafunzi hawa wanakazi

kaenda kwenye mkurabita,

Jamaa anaongea kwa uchungu kweli kweli, na kama kawaida ya wahaya anachanganya na Kidhungu.

Anasema haamini hizi takwimu zinatolewa, Mhaya huyooooooooooooooooooooooo anasema yeye ndo alileta executive agencies kutoka uingereza.

Procrastination, anasema hili ni tatizo la serikali,

Anasema yeye ni senior citizen, sasa anataka kumkera dada saada mkuya, kwamba awe msikufu hata kama anaconfidence, anamushauri kuhusu leadership, anawaambia waendelee kujisomea

lakini alitoka kujiuliza maswali, kwamba aliposikia huju binti ameteuliwa kuwa waziri wa fedha, akajiuliza angeweza kuwa msuya, anadai huyu ni one of the most efficient finance minister, anauliza mkuya anaweza kufikia viwango vyake?

Huyu nshomile bwana, ametaka kumrank mkuya na Gordon Brown, kazi kwelikweli
kwanza, kwa nini Kikwete hampi nafasi huyu ntukamazima?
 
Libunge la CCM Li-mama, limeanza kuongea
yaani sugu ametoka kuongelea matatizo kwenye sekta ya afya, hili li-CCM limeanza kwa kuwapongeza waliolifariji kwa kwenda kwenye utalii wa matibabu nchini india. wonders will never end, hivi ma-CCM hayajui hata pa kuanzia hotuba zao.

any way, linaendelea kwa kumsifia waziri wa fedha, alafu ghafla limeanza kulalamika kwamba Bilioni mbili hazikwenda kwa ajiri ya ujenzi wa hospitali ya rufaa huko singida? linaendelea kuihoji serikali, kwamba wananchi wa singida wameshirikiana na mkuu wa mkoa kujenga hospitali hiyo kwa nini serikali kuu haitimizi ahadi ya kupeleka pesa, linasema linaongea kwa uchungu sana juu ya jambo hilo, sasa na mimi naliuliza, japo usoni halioneshi uchungu kwa nini lilisifia mwanzo wakati linajua lina machungu? mi-CCM bwana.
Sangarara nakupa like kwa kukerwa kama mimi.
 
Back
Top Bottom