Live Feeds: Kutoka mahakama Kuu ya Rufaa Kivukoni - Rufaa ya Lema, Dec 04, 2012

Hivi watu wanaofungua kesi bila kupata ushauri wa kisheria; wanasababisha rasilimali za Umma kama muda, rasilimali watu na pesa kutumika kusikiliza kesi zisizo na mshiko, wanatofauti gani na Mafisadi ?

Makamba baada ya uchaguzi aliwaambia makada wao wafunge kesi zidi ya wabunge wa vyama vya upinzani(CHADEMA), hivyo ni mikakati ya chama chao kuwazoo fisha wabunge wa chadema...
 
Kama hapo mahakaman hakuna ulinz mkali basi lema atashinda kama upo ule kama wa kumlinda obama basi imekula cdm.
 
Hahahahaha mwenzenu nasikia raha sana kupata habari nzuri dhidi ya Kamanda Lema na CDM kwa ujuma,hakika Mungu anaenda kutenda sasa na ndivyo itakavyokua kwa Mh Lema kurejeshewa Ubunge wake,öooh!! Haleluya.
 
Kitendo cha Mbunge kushitakiwa akakutwa ana makosa, halafu akakata rufaa ili kutegemea umahiri wa mawakili na si ukweli wa kuwa ni mwakilishi mwema, kinamfanya Lema kuwa hafai kabisa kuwa mwakilishi wa wananchi.

Sioni mantiki ya watu kumshabikia mwakilishi anaewakilishwa baada ya kushindwa.

Husomi hata historia fupi tu ya Tanzania ambapo Nyerere alibambikiwa kesi kama Lema na wakoloni na lionekana mhalifu wa kufungwa na akalipa faini kama mtu mwenye hatia lakini aligombea urais na akawa rais. Si mara zote kushtakiwa unakuwa umetenda kosa ila katika siasa wenye nguvu wakiona wanazidiwa hukimbilia mahakamani walikoweka majaji wao ili kumkandamiza mpinzani kwa kivuli cha mahakama. Nelson mandela alifungwa jela 22 yrs na alitoka akawa rais na ile kufungwa ikampa heshima hadi leo. Heri kuumia kwa kutenda wema kuliko kuwafurahisha mafisadi huku ukiburudika na mali za dhuluma.
 
Jina kama Batilda au Mumewe Burhan.

Namuongezea...

Kitendo cha Lema kupatikana na hatia nyingine, na baadae Hakimu kumuhukumu kwa kosa lingine kinathibitisha unajisi wa wazi kwa mhimili huo muhimu nchini!! Yaani uibe kuku uhukumiwe kwa kuua mtu..ipo wapi hii??

Kitendo cha Hakimu kukubalia ushaihdi wa makada wa CCM na kukataa ushahidi wa watu wa Lema kwa madai ni makada kinatia doa katika utoaji haki nchini

Kitendo cha Batilda kuitwa zaidi ya wiki kutoa ushahidi kama aliwahi kugongwa na Loawassa ama la na kukataa kuja kutibitisha na baadae Jaji akaridhia upande mmoja kuwa hajagongwa wakati yeye hakuwahi kuwashikia miguu ni ubutu mwingine katika maamuzi.. Ili swala liwe kashfa ni lazima liwe uongo.. Mimi na wewe nani anaweza kusema Lowassa na Batilda hawajapeana mimba?? Kama wamepeana ni kashafa??

Kitendo cha Jaji kukubali hatia kwa Lema kwa kosa la kufikirika..maneno na vijembe vya wagombea ambayo hayakuwahi kuwa tatizo mwanzo wa uchaguzi hadi mwisho...(kumbuka Batilda aliwahi lalamikia mambo mengine...na sio kudhalilishwa) thrid parties wanawezaje kuwakilsiha madhara ya Batilda kuelezwa amegongwa na Lowassa??
 
Mkuu Matola heshima mbele sana mkuu,

Kuna uwezekano jaji mkubwa alipewa maelekezo ya kupindisha sheria lakini akaona atajipaka tope bure na akaamua kuingia mitini, leo sheria na vigezo vya mahakama lazima vifuatwe, siamini kama half bench itakubali kujipaka tope, leo kazi ipo wamuulize mzee wa Saigon nini kilimpata..
Kwangu mimi kesi hii nikiiangalia katika misingi ya kisheria kujitoa kwa Jaji Mkuu ni Advantage kwa Lema na Chadema, kwa sababu kama Half bench ikivulunda ( lakini haitokuwa hivyo nawaamini sana ) basi Lema na Chadema bado wanakuwa na haki ya kuomba Hukumu ipitiwe na Full bench jopo la Majaji 7 likiongozwa na Jaji Mkuu.

Madhara ya half bench ikiwa inaongozwa na Jaji Mkuu, hukumu yake huwa ni ya mwisho kwa sababu uwepo wa Jaji Mkuu humaanisha ni kama full bench. kwahiyo kisheria hii faida kwa Lema na Chadema na katika mchakato wa kuzichallenge taasisi zetu za maamuzi.
 
There are currently 1129 users browsing this thread. (303 members and 826 guests)

Hii inaonesha umuhimu wa kesi hii kwa wanajf na watz kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom