Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Zile kelele za Polisi wengi kutumika wakati wa kuwakamata kwenu ni matumizi ya nguvu pasipo ulazima, sasa huu utititri wa mawakili vp?
Utitiri wa mawakili ni kuonyesha msisitizo pia kupanbana na Amri toka juu kwa majaji ambao hawafanyi kazi kwa mujibu wa sheria bali wanafanya kazi kwa mujibu wa zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM.
 
mgonjwa hutibiwa kwa hiali zake wala halazimishwi na sheria za udaktari na miiko yao ipo wazi, lakini sheria za polisi haziruhusu polisi wa kiume kumgusa mwanamke tena kumfukuza mahakamani kumlazimisha apande gari wakati alikuwa na kazi zake mahakamani,
Sheria inasemaje kama mtu anatakiwa kuondoka mahakamani mara moja halafu akawa hataki kuondoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mahakamani kwa kesi za magufuli huwa hazupo huru , lakini huwa huru kwa kesi zingine ambazo hazina Amri toka juu.
Kwa hakimu / jaji mwenye taaluma na amekula kiapo ,anajitambua hafuati maagizo ya mtu zaidi ya kutekeleza matakwa ya sheria halali zikizowekwa
 
Mimi nina mashaka na hawa wanaojiita MAWAKILI. Inakuwaje mtu unayejiita WAKILI, Kwa sifa yako unatakiwa kuwatetea watu wenye kesi mahakamani halafu unapopata katatizo kadogo tu unakodi LUNDO la WANASHERIA ili kukusaidia.
Je, wewe unakuwa ni WAKILI kilaza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo nguvu wanazotumia kwa mambo ya kipuuzi wangeziwekeza kusaka kila afisa wa Serikali na mwana ccm yeyote aliyewah kushiriki wizi na kuwashtaki hakika wangelitendea haki sana Taifa hili,wangeungwa mkono lkn kwa haya wanayofanya malipo yao hayako mbali maana lengo lao ni kudhalilisha na watadhalilika wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka michache nyuma upinzani (hasa Chadema) ulijengwa kwa misingi sahihi na inayostahili kisiasa, hadi ikavutia watu wengi na wengine maarufu (kama mawaziri mkuu wawili wastaafu). Ilionekana ni tegemeo mbadala ktk uongozi wa nchi.
Ajabu baada ya stratejia ya chama kushikwa na watu wengine (kwa kupukutisha wale waliokua wanasiasa wa kweli) sasa hivi chama kinajikita zidi ktk umaarufu wa kisheria na kuonekana kama ni taasisi ya kisheria zaidi na si ya kisiasa.
Ili kujijenga zaidi ni lazima kuangalia matakwa ya chama kama kweli kipo ktk mlengo sahihi, tofauti na hivyo itakua ni kwa baadhi ya wanasheria kujijenga zaidi kwa na si kukijenga chama.
 
Sijui kwa nini vilaza wale hawakupeleka maWP kumshikashika mama mwenzao? mbali na kumshikashika na ''kumtengua bega'', kumtoa ''afisa wa mahakama'' kwenye eneo lake la kazi na ''kumzuia kutimiza wajibu wake'' kwa style ile ni kosa la jinai:)
acha watiwe adabu ili wajifunze, wanafikiri kila kitu ni kutumia tu miguvu
 
Mambo mengine sasa yamekuwa sifa kupitiliza...

Imekaaje kama vichwa vya habari hapo kesho vingesomeka..

" TLS yatoa msaada wa uwakili kwa kesi 300"
 
Mazoea ni shida sana.hao polisi wamezoea kuwavuta,vudata dada zetu mitaani.wakijuwa kuwa ni haki kumbe ni kinyume cha sheria. Hayo ndio matokeo ya kushikwa akili na amri kutoka juu.Aje huyo amri kutoka juu amtete.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom