Lissu akubali Tanzania ni salama na Rais Samia

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,443
1,046
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ameahidi kurejea nchini baada ya kuona Tanzania sasa ni salama chini ya Rais Samia Suluhu kama tunakumbuka Rais Samia Suluhu Februari 2022 alifanya ziara ya kikazi nchini Ubelgiji Lissu alitumia fursa hiyo kukutana na Rais Samia Suluhu na kufanya mazungumzo kwa saa moja.

Baada ya mazungumzo yale Lissu alieleza kuwa amezungumza na Rais Samia kuhusu kesi iliyokuwa inamkabili mwenyekiti wa Chadema na kesi hiyo Rais Samia Suluhu aliifanyia kazi ikafutiliwa mbali.

Lissu aliongelea pia kuusu zuio la mikutano ya hadhara ambalo Rais Samia Suluhu amelifanyia kazi mwanzoni mwa mwaka huu.

Lakini Pia anaesema alimueleza kuhusu haki zake alizonyimwa baada ya kuvuliwa ubunge kwani alikuwa mbunge pekee ambaye hakupokea kiinua mgongo pia hili nalo Rais Samia Suluhu alilifanyia kazi.

Nimerejea haya yote kuona ni kwa kiasi gani Rais Samia Suluhu anapenda maridhiano yani zile nguzo za uongozi wake zinaiongoza nchi vizuri amefanyia kazi yale yote yaliyokuwa kinyume na sheria na sasa ulinzi na usalama wa nchi yetu umeimarishwa na ndio maana Lissu anapata ujasili wa kurudi nchini baada ya kukaa nje kwa miaka 5.

Mungu aendelee kumuongoza Rais Samia Suluhu ili aendelee kuiongoza nchi kwa kufata sheria na katiba ya nchi.
 
Lissu karibu nyumbani asali yako bado ipo though kiinua mgongo chako umeshakula
 
Kwani Tanzania iliwahi KUKOSA amani tangu liniii?? Mbona alikuja kupiga kampeni kiriho safiii, na baaada ya kugaragazwa asubuhi akarudi huko tena
 
Waocwarudi watulize mishipa wapambanie maisha na siku zisonge,hakuna mtu ana attention nao ki viile zaidi ya hapo hapo Ufipa sthtreets.

Watanzania wa sasa walifunguka macho bado masikio tu.
 
Kwani Tanzania iliwahi KUKOSA amani tangu liniii?? Mbona alikuja kupiga kampeni kiriho safiii, na baaada ya kugaragazwa asubuhi akarudi huko tena
Acha kujisahaulisha umesahau kuhusu watu wasiojulikana? matukio yalikuwa yanapishana kila siku ukiachilia mbali waandishi wa habari kuuwawa pia roma kutekwa yani ilikua tafrani lakini toka Rais Samia Suluhu aingie madaraka matukio ya ajabu yameisha kabisa uhuru wa vyombo vya habari vimerejea pia democrasia imerejea
 
Waocwarudi watulize mishipa wapambanie maisha na siku zisonge,hakuna mtu ana attention nao ki viile zaidi ya hapo hapo Ufipa sthtreets.

Watanzania wa sasa walifunguka macho bado masikio tu.
Kurudi kwao kunaashilia kuwa Tanzania ni salama na Rais Samia Suluhu so its better warudi nchini maana hata democrasia imerejea
 
Kwani Tanzania iliwahi KUKOSA amani tangu liniii?? Mbona alikuja kupiga kampeni kiriho safiii, na baaada ya kugaragazwa asubuhi akarudi huko tena
Kweli Tanzania aikuwai kosa amani hila kwetu sisi mimi na wewe lakini sio kwa lissu chupuchupu apoteze maisha Suala la amani mi naona dunia nzima ni suala la mtu personal nchi inaweza ikawa na amani hila kuna wananchi wake baadhi awana amani kabisaaa
 
Acha kujisahaulisha umesahau kuhusu watu wasiojulikana? matukio yalikuwa yanapishana kila siku ukiachilia mbali waandishi wa habari kuuwawa pia roma kutekwa yani ilikua tafrani lakini toka Rais Samia Suluhu aingie madaraka matukio ya ajabu yameisha kabisa uhuru wa vyombo vya habari vimerejea pia democrasia imerejea
Wataje wewe Sasa hao watu
 
Kweli Tanzania aikuwai kosa amani hila kwetu sisi mimi na wewe lakini sio kwa lissu chupuchupu apoteze maisha Suala la amani mi naona dunia nzima ni suala la mtu personal nchi inaweza ikawa na amani hila kuna wananchi wake baadhi awana amani kabisaaa
Kwa hiyo chupuchupu yake ndoo Tanzania Haina amanii
 
1. Katiba Mpya.

2. Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano.
 
Back
Top Bottom