Lipumba: serikali itegemee zaidi

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
Serikali itegemee maajabu
CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema Serikali itegemee maajabu zaidi ya tiba za asili kuliko ya Loliondo, kwa kuwa wananchi wamechoka na ubabaishaji wa sekta ya afya.Profesa Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, umati unaoendelea kufurika kwa Mchungaji Mwasapile ni kiashiria kwamba Watanzania wamekata tamaa na huduma za afya zinazotolewa na Serikali.

“Ikiwa Serikali haitajali huduma muhimu za afya kwa wananchi wake, tutarajie mengi zaidi ya haya ya Loliondo,” alisema Lipumba.

Alisema wananchi wakichoka na kukata tamaa na chombo chenye dhamana ya kuwahudumia, watatafuta njia mbadala ya kujikwamua na tatizo kama ilivyokuwa Loliondo.

Profesa Lipumba alieleza kuwa kasi ya watu kwenda kutafuta tiba mbadala kwa mchungaji, inaonyesha kuwa Watanzania wameshakata tamaa na huduma za afya zinazotolewa hospitalini.

"Kimsingi hii ni dalili ya wazi kuwa, sekta ya afya imeshindwa kazi. vinginevyo isingewezekana watu watoroke hospitalini kwenda Loliondo," alisema.

Profesa Lipumba alisisitiza kuwa watu kukimbia tiba za hospitali na kwenda kutafuta tiba mbadala ni aibu kwa taifa hasa kwa sekta ya afya ambayo imeajiri watu na kuwalipa mishahara kwa kazi hiyo.

“Ni kiashirio kibaya sana kwa taifa kuona watu wakiwa wanatorosha wagonjwa wao hospitalini kutafuta tiba mbadala," alisema.

Profesa Lipumba aliongoza kuwa umati uliojaa Loliondo unaonyesha picha halisi kuwa, Watanzania wengi ni wagonjwa, lakini sekta ya afya haina uwezo wa kuwahudumia.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo huku maelfu ya watu yakiendelea kumiminika Loliondo kupata tiba ya mchungaji huyo aliyoeleza kuwa aliigundua kwa njia ya maono.

Ongezeko la watu wanaoelekea Loliondo limezidi hasa baada ya Serikali kubariki tiba hiyo inayotolewa katika kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro.

Mchungaji, Mwasapila juzi alipongeza uamuzi wa Serikali kuondoa tishio la kuzuia kutoa dawa kwani watu wengi wamekuwa wakinufaika na dawa na mahitaji yanaendelea kuwa makubwa.

“Tunamshukuru Waziri William Lukuvi kwa kuruhusu dawa iendelee kutolewa na kutoa ahadi ya kuleta huduma mbalimbali muhimu katika kijiji hiki,” alisema Mchungaji Mwasapile.
source: nipashe
 
Back
Top Bottom