Lipumba: Serikali imeanguka

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
• HALI YA MAFUTA BADO TETE DAR, MIKOANI

na Mwandishi wetu - Tanzania Daima

SERIKALI imetahadharishwa kuwa isipochukua tahadhari kusaka suluhu ya kudumu ya tatizo la mafuta na umeme, itaanguka na uchumi wake utaporomoka kwa kiwango cha kutisha.

Matokeo ya kuporomoka kwa uchumi huo ni kwa wananchi kuendelea kuwa katika maisha magumu kutokana na kupanda kwa bidhaa za kilimo, viwandani na huduma zote za jamii.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibraahimu Lipumba, alisema ilichokifanya serikali hakikuwa kibaya, lakini ilikurupuka kutangaza bei elekezi ya mafuta bila kujali athari wanazoweza kuzipata wafanyabiashara wa nishati hiyo.

"Unajua hakuna sheria ya serikali kupanga bei ya mafuta, soko la mafuta ni huria. Ewura wanachofanya ni kutoa bei elekezi na bei elekezi ni kama ushauri na ndiyo maana wenye mafuta nao walikuja juu.


"Wafanyabiashara hao walizoea bei elekezi za Ewura zilikuwa ni za juu, sasa hili la kushusha kwanza lazima watambue lazima kuwe na maandalizi ili wasiuumize upande wowote," alisema Profesa.

Lipumba ambaye ni mmoja wa wanazuoni waliobobea kwenye masuala ya uchumi nchini, alisema wakati wa kufanya maamuzi hayo, serikali haikujipanga, hivyo ikajikuta badala ya kumsaidia mwananchi wa kawaida, ikamwongezea mzigo mara dufu.

Kwa mujibu wa Lipumba, kwa vile serikali imewabana wafanyabiashara hao kuuza mafuta, watakachokifanya baada ya kumaliza hazina ya mafuta waliyonayo, hawataagiza tena bidhaa hiyo na hapo ndipo itatokea balaa zaidi.


"Katika mazingira hayo, tutarajie maumivu makubwa kwa wananchi tofauti na awali kwani gharama za usafiri, mazao, umeme vitapanda na hivyo uchumi wa nchi kuzidi kuporomoka," alisema Profesa Lipumba.


Alisema katika kipindi cha wiki moja tangu kutangazwa kwa bei elekezi iliyoibua balaa nchini, nauli zilipanda, hasa za mikoani, maana wenye magari wananunua mafuta kwa njia ya magendo.

Ili kuepuka hali hiyo, Profesa Lipumba aliishauri serikali kuhakikisha inakuwa na chombo chake cha kufanya biashara hiyo ili kuepuka madhara kama hayo.

Aliishauri serikali kuliongezea nguvu Shirika ka Maendeleo la Petroli nchini (TPDC) ili kuepuka matatizo yaliyojitokeza.


Viwanda vyasimamisha uzalishaji
BAADHI ya kampuni na viwanda jijini Dara es Salaam, vimelazimika kupumzisha wafanyakazi wao kutokana na tatizo la upatikanaji wa mafuta na umeme.

Makampuni na viwanda hivyo, vimefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wafanyakazi wanafika sehemu za kazi bila kufanya shughuli zozote za uzalishaji.


Miongoni mwa kampuni zilizopumzisha wafanyakazi wake ni pamoja na kampuni ya ujenzi ya Ihanga Construction Company.

Mmiliki wa kampuni hiyo, Burton Kihaka, alisema kila siku huingia hasara ya zaidi ya sh milioni mbili kutokana na kulipia mitambo ya ujenzi huku ikiwa haijafanya kazi kwa zaidi ya siku saba tangu tatizo la mafuta lianze.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha serikali kutokuwa makini katika mikataba wanayoingia na wawekezaji hasa katika sekta nyeti kama ya mafuta na umeme.


Aliishauri serikali kuwekeza zaidi TPDC ili iwe wakala mkuu wa uagizaji na usambazaji wa mafuta.


"Vifaa vyote kama magreda, maburudoza, vijiko vinatumia mafuta na hapa tunakodi vifaa kwa kulipia fedha nyingi bila kujali vimefanya kazi au la, hivyo kwa siku kampuni inalazimika kulipa sh milioni moja hadi mbili kwa siku na bado fedha za wafanyakazi," alisema.


Naye Naibu Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki, Moses Swai, alisema tatizo la umeme mbali na kuleta madhara katika utendaji, bado wamelazimika kupunguza baadhi ya wafanyakazi.


"Awali umeme ulikuwa ukikatika bila taarifa hali iliyokilazimu kiwanda kukosa pamba kwa ajili ya uzalishaji, na tatizo hilo lilitulazimu kupunguza wafanyakazi lakini Februari mwaka huu tuliweza kuendelea na shughuli za uzalishaji lakini hili lililojitokeza limetuathiri sana," alisema Swai.


Nauli za daladala juu

WAKATI Wantanzania wakiendelea kuumia juu ya upatikanaji wa nishati ya mafuta wakati wadau wa nishati hiyo wakiendelea kuvutana, jijini Mbeya hali imezidi kuwa tete kwa wananchi wa jiji hilo.

Tanzania Daima imeshuhudia jana asubuhi abiria wengi waliokuwa wakisubiri usafiri wa daladala kuelekea sehemu zao za kazi wakipata adha ya usafiri huo, kutokana na kukosekana kwa magari; ama kuwepo kwa magari yenye nauli iliyopanda mara mbili ya nauli ya kawaida.


Baadhi ya daladala zilionekana kuegeshwa pembezoni mwa barabara kutokana na kuishiwa mafuta na madereva wakijikuta hawana pa kwenda kununua mafuta na kuwapeleka abiria sehemu wanayokwenda.

Bei ya kawaida kwa abilia anayeshuka kutoka kituo kimoja hadi kingine ni sh 300, lakini kwa sasa inatozwa kati ya sh 500 na 1,000 kwa kila kituo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya madereva wa daladala jijini hapa walisema kuwa pamoja na makampuni yanayouza mafuta kukubali kurejesha huduma hiyo, bado wananchi wa mikoani wanapata mateso kwani vituo vyote mjini hapa havina mafuta.


Dereva ambaye anafanya safari kati ya Soko Matola na Uyole Joseph Mwaikisu alisema wameamua kupandisha nauli kutokana na kupanda kwa gharama ya mafuta kwani wanalazimika kununua kwa sh 4000 kwa lita.


Kwa upande wao, baadhi ya abiria walisema kitendo cha serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wafanyabiashara hao ni kutowatendea haki wananchi wake.


"Mimi binafsi nina gari langu lakini imenilazimu kupanda daladala kwa ajili ya kufuata mafuta Igawa wilayani Mbarali ambako nimefanikiwa kupata lita 20 za petroli lakini nako kuna petroli pekee hakuna mafuta ya aina nyingine wanadai kuwa yamekwisha," alisema Wastala Mathew.


Akizungumzia hali hiyo Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Majini na nchi kavu (SUMATRA) Mkoa wa Mbeya Amani Shamaje alisema kuwa yeye si msemaji wa suala hilo wanaotakiwa kuzungumzia ni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (EWURA).


Kwa upande wake Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani mkoani hapa limesema kuwa suala la kupandishwa nauli kiholela ni kinyume na utaratibu wa nchi, hivyo wao kama kitengo wanalifanyia kazi na wako katika kikao kujadili namna wanavyoweza kushughulikia suala hilo.


Tanga, Iringa hali bado tete
Wauzaji wa mafuta katika baadhi ya vituo vya mafuta mkoani Tanga, wameanza kuuza mafuta kutekeleza amri ya serikali iliyoitoa saa
24 kwa wauzaji mafuta waliogoma kurejesha huduma hiyo.


Kwa upande wao baadhi ya madereva wa magari madogo na makubwa walisema baadhi ya vituo vya nafuta vimeanza kuuza mafuta kuanzia jana.


Mkoani Iringa, inaripotiwa kuwa watalii mbalimbali waliokuwa wakielekea katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa, jana wamekesha katika kituo cha mafuta Gapco wakisubiri foleni ya mafuta huku walanguzi wa mafuta hayo wakijinufaisha kwa kulangua sh 3500 kwa lita moja.


Ufumbuzi wa uhaba wa mafuta katika Manispaa ya Iringa bado ni mgumu baada ya vituo vyote kuishiwa mafuta toka usiku wa jana hali iliyosababisha madereva kukesha katika kituo cha Gapco eneo la Mshindo wakisubiri mafuta baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa upo uwezekano wa mafuta ya petroli na dizeli kuingia wakati wowote.

Pamoja na vituo viwili kati ya vituo zaidi ya saba vya ndani ya Manispaa ya Iringa kuonekana kuanza kuuza mafuta jana, hali ya usalama katika vituo bado tete kwani baadhi ya madereva walipigana ngumi kugombea mafuta huku askari polisi wakifanya kazi ya ziada kutuliza vurugu hizo.

Kwa upande wa hali ya usafiri katika Manispaa ya Iringa, hali bado mbaya baada ya teksi zinazotoa huduma hiyo kushindwa kufanya kazi. Hata hivyo teksi chache zilizotoa huduma ya usafiri, zilitoza kiwango kikubwa cha nauli cha kati ya sh 3000 hadi sh 5000 kwa safari za katikati ya jiji.


Baadhi ya wananchi, walimtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kujiuzulu kutokana na tatizo la mafuta.



 
Lipumba ni Mwanauchumi, anaona Uchumi utaporomoka sababu ya ukigeugeu wa Serikali ya CCM

Tatizo hapa ni wote kiongozi na viongozi aliowachagua wote hawaiwezi kazi
 
Back
Top Bottom