Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma wameomba kukutana na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Prof Ibrahimu Lipumba ili kujadili kuyumba kwa uchumi wa taifa na kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alipokuwa akizungumza na wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Dodoma (Udom), Chuo cha biashara (Cbe), Chuo cha Mipango pamoja na Chuo cha Mtakatifu John.Naibu Katibu Mkuu huyo alisema baada ya kuzungumza na wanafunzi hao wa vyuo vikuu na kutambua umuhimu wa uchumi wa taifa maombi hayo wameyapokea na kwamba Prof Lipumba atafanya kongamano na wanafunzi hao kujadili masuala ya kuyumba kwa uchumi na mfumuko wa bei uliopo sasa.Baada ya kusikiliza maombi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kwa kuona jinsi hali ya uchumi ilivyo mbaya kwa sasa tumeamua kuandaa kongamano ambalo Prof Lipumba atazungumza na wanafunzi hawa ili kulitafutia ufumbuzi suala hili, alisema Mtatilo na kuongeza Suala hilo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya mtaalamu huyo wa uchumi kulejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani, alisema.Mtatilo alisema kwa sasa hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya baada ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei jambo ambalo linazidi kufanya maisha ya watanzania kwa magumu.Kiukweli suala la uchumi na mfumuko wa bei linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi kwani jinsi hali ilivyo sasa inatisha ndio maana hata wasomi wameliona jambo hili na kutaka kutafutiwa ufumbuzi wa haraka, alisemaKatika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo alisema wanafunzi hao pia wameomba kukutana na Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ilikuwapa mafunzo ya siasa na utawala bora.Wanafunzi hao pia wameoma kukutana na Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ili kuwapa mafunzo ya siasa na utwala bora jambo ambalo ni la msingi kwa maendeleo ya Taifa, alisemaKatika Mkutano huo ambao ulihuhuliwa na wanafunzi 60, wanafunzi 23 walichukua kadi za chama hicho.20 february,2012