LINDI: Wanafunzi 30,235 wanatarajiwa kuanza elimu ya msingi

May 4, 2020
32
37
Takribani wanafunzi 30,235, wanatarajiwa kuanza elimu ya msingi (darasa la kwanza) Mkoani Lindi punde muhula mpya utakapoanza tarehe 11 mwezi huu. Kati ya idadi hiyo wavulana ni 15,266 na wasichana ni 14,969 huku kwa upande wa darasa la awali wanaotarajiwa kuanza darasa hilo ni wanafunzi 27,220.

Hayo yameelezwa na Afisa elimu mkoa wa Lindi, Vicent Kayombo wakati akizungumza na Mashujaa Fm kuhusu muhula huo mpya wa masomo na mikakati yao ya kuboresha elimu kwa mwaka 2021 na kuwaasa wazazi kutowachelewesha kuwaandaa wanafunzi.

Akizungumzia hali ya madarasa kwa shule zilizokuwa na upungufu wa madarasa, Mwl. Kayombo amewahakikishia wazazi katika maeneo hayo kuwa wanaendelea na hatua za mwisho za ukamilishaji wa miundombinu hiyo na kwamba suala hilo halitoleta athari kwa wanafunzi kwani wameshatafuta mbadala.

Hata hivyo Afisa elimu huyo amesema kuwa kwa Mkoa wa Lindi wamepata jumla ya waalimu 306 kwa shule za msingi na sekondari kupitia ajira mpya 8000 zilizotolewa na serikali hivi karibuni na kwamba walimu hao wataenda katika shule zilizokuwa na upungufu
 
Kama Mkoa wa Lindi umepata walimu 306 (msingi na sekondari),natilia shaka ile idadi ya walimu walioajiriwa na serikali kama inafika 8000
 
Back
Top Bottom