Lilongwe: Watanzania Washangilia Balozi wa Tanzania kuondolewa, yadaiwa alizorotesha Mahusiano ya Ubalozi na Watanzania wenzake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,054
219,072
Hii ndio Taarifa mpya ya Sasa kutoka Nchini Malawi , Kwamba Wafanya biashara wa Kitanzania pamoja na wafanyakazi wa Kitanzania wa Taasisi na mashirika ya kimataifa walioko Malawi , jioni hii wanafanya hafla ya siri ya kusherehekea kuondolewa kwa Humphrey Polepole kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Habari zaidi kutoka Malawi zinadokeza kwamba Tangu kuteuliwa kwa Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi uhusiano kati ya watanzania wanaoishi nchi hiyo na Ubalozi wao ulizorota ama waweza kusema ulikufa kabisa , hii ilitokana na Watanzania wa huko kukataa kuwa na balozi aina ya Polepole katika nchi ya Kidemokrasia ya Malawi .

Humphrey Polepole ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM , alishirikiana na John Magufuli aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM , pamoja na Katibu wao Bashiru Ally kuhujumu demokrasia nchini Tanzania , watu hawa walitumia hela za umma kununua Wapinzani na kuiba kila Uchaguzi uliokuja mbele yao kwa kumshirikisha mshirika wao mkuu Dr Wilson Mahera aliyekuwa Tume ya Uchaguzi (Hakuna Mtanzania asiyelijua jambo hili)

Kwa kufupisha , Uteuzi wa Polepole kuwa Balozi nchini Malawi kuliwafedhehesha sana Watanzania wa Malawi jambo lililopelekea kuvunja uhusiano na Ubalozi huo na kuzorotesha shughuli nyingi .

Tunaamini sasa baada ya mamluki huyu kuondolewa mambo yatarudi kama awali

Kwa mara ya kwanza napenda kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuyafanyia kazi malalamiko ya Watanzania walioko Malawi na kuchukua hatua .
 
Hii ndio Taarifa mpya ya Sasa kutoka Nchi Malawi , Kwamba Wafanya biashara wa Kitanzania pamoja na wafanyakazi wa Kitanzania wa Taasisi na mashirika ya kimataifa walioko Malawi , jioni hii wanafanya hafla ya siri ya kusherehekea
Kwamba umepita mitaani ukaona watu wako bizee wanashangilia? Haya auongo yanakusadia nini hasa wewe na chama chako na familia yako

USSR
 
Sasa wewe erythrocyte unakoelekea utakuwa huaminiki umetoa wapi habari hizi ? Source ??? Evidence ??? ,uko too pro CHADEMA na anti sukuma Gang .
Chanzo ni mimi mwenyewe , nishaeleza sana kuhusu Polepole na ubalozi wa Malawi humu Jf , na mara zote nime declare interest kwamba mimi ni mfanyabiashara mwenye shughuli zangu nchini Malawi na kwingineko , labda kama wewe ni mgeni hapa jf .

Mkitenda ubaya hamtanyamaziwa kamwe na kila ubaya utalipwa tu
 
Kwanini unaandika uongo wa namna hii katika jukwaa la wenye akili timamu

Kama ni siasa basi inakupeleka vibaya sana maana unaandika uongo huku wewe ukitegemewa ulete habari za chama chako.

Unadhan kuna mwenye akili timamu atakuamini pale utakapoleta habari zinazohusu chama chako zaidi wataona kama propaganda.

Uongo sio sifa bora kwa mwenye akili timamu nipo hapo ulipo andika na huu ujinga unaoandika siuoni wala sijausikia.
 
Acha uongo wako wewe mwana chadema uliyepoteza muelekeo na kutekwa na habari za CCM na uchapa kazi wa Rais wetu mama Samia suluhu Hassani.

Nilifikiri nitaona umeandika kwa ushahidi kuwa ni vipi mh Balozi alikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara katika kufanya biashara zao nchini Malawi au Ni vipi alishindwa kuwasaidia walipopata changamoto ya kupata vibari au kupata au kutumia fursa ya kibiashara ya kupeleka au kutoa bidhàa Malawi kuja Tanzania au kwenda Malawi,lakini hujaeleza kitu juu ya hayo Jambo linaloonyesha wewe Ni muongo na mzushi tu.

Hujaeleza Ni vipi wafanyakazi wamchukie na kufanya sherehe ya kuhamishwa kwa mh Balozi ,hujaonyesha Wala kueleza Kama alishindwa kujenga umoja na mshikamano wa wafanyakazi au aliwagawa kwa misingi ya aina yoyote Ile, hujaeleza kwa kuwa unajuwa kuwa habari yako Ni ya uongo na uzushi mkubwa Sana.

Suala la kusema alishiriki kuwanunua wapinzani,Hili ningependaa kusema kuwa unajitia aibu na kujivua Nguo hadharani maana umethibitisha bila Shaka kuwa upinzani ninyi Ni wababaishaji,vigeu geu,watu wenye njaa Kali Sana matumboni mwenu ,njaa yenu IPO Hadi vichwani mwenu,hamna utashi Wala maamuzi ,hamfai kupewa nchi Wala kuaminiwa Wala kuungwa mkono maana mna Bei yenu ambayo mtu akifika mnanyoosha mikono juu mwendo wa mateka, ndio maana mnapuuzwa na watanzania kwa kuwa ninyi ni watu msioweza kujiongoza Wala kusimamia Jambo,hamna falsafa Wala itikadi,ninyi falsafa yenu na itikadi yenu Ni TUMBO lipate kupona njaa kwa kitu chochote mtakachorushiwa midomoni.

Hii inaonyesha kuwa chama chenye na upinzani wote kwa ujumla mnapigania maslahi ya matumbo yenu ndio maana mnaweza kununulika,pili inaonyesha dhahiri upinzani wa nchi hii hamuwezi kuzilinda na kuzitetea maana akija mwenye mfupa wenye mnofu mtauza Rasilimali zetu.

Hakika watanzania wanastahili pongezi kubwa Sana kuwapuuzeni upinzani na kutowapatieni ushirikiano wa aina yoyote Ile mkiwaomba wawaunge mkono,sisi CCM hata tuamue kusema kuwa mwakani tunabeba mitaa na vijiji vyote bila kupingwa naamini watanzania watatuunga mkono na kuwapuuzeni upinzani na hamtakuwa na chochote Cha kutubabaisha Wala kupewa ushirikiano na mtanzania yeyote mwenye Akili Timamu maana nyie hamjitambui na mnapaswa kuongozwa hata kwa lazima mpaka msonge mbelee
 
Kwanini unaandika uongo wa namna hii katika jukwaa la wenye akili timamu

Kama ni siasa basi inakupeleka vibaya sana maana unaandika uongo huku wewe ukitegemewa ulete habari za chama chako.

Unadhan kuna mwenye akili timamu atakuamini pale utakapoleta habari zinazohusu chama chako zaidi wataona kama propaganda.

Uongo sio sifa bora kwa mwenye akili timamu nipo hapo ulipo andika na huu ujinga unaoandika siuoni wala sijausikia.
Weka ukweli wako hapa tuuone , who are you by the way ? si kila mamluki anaweza kushirikishwa kwenye kila jambo
 
Back
Top Bottom