Lijue kundi la Boko Haram

Mwita Matteo

JF-Expert Member
May 16, 2010
216
55
Boko Haram ni jina ambalo hutumika kulitambulisha kundi lijulikanalo kama “watu waliojitolea kueneza mafundisho ya mtume na jihad” yaani Ahlisunnah Lidda’awati wa’l-Jihad’. Boko Haram ni neno la kihausa lenye maana ya “makataa ya elimu ya kimagharibi” au “Elimu ya kimagharibi ni dhambi.”

Kundi lilipewa hilo jina na wakaazi wa Maiduguri mji mkuu wa jimbo la magharibi mwa Nigeria la Borno ambapo kundi hilo lilianzia, mwanzoni mwa miaka ya 2000. Japo jina hilo limepata umaarufu na linatumiwa sana na vyombo vya habari, jina hilo halisawiri malengo ya kundi hilo ambayo ni kuipindua serikali ya Nigeria ambayo inaonekana kughubikwa na rushwa, na kuanzisha taifa la kiislamu ambalo litaongozwa kwa misingi ya sharia, na kufuta ushawishi wa kimagharibi kama vyuo vikuu. Boko Haram linapinga ustarabu wa kimagharibi vikiwemo nadharia mbali mbali za kisayansi na lina hubiri ustarabu wa kiislamu. Mwanzoni Boko Haram ilijulikana kama Talibani ya Nigeria au Yusufiyya.

Chimbuko la Boko Haram lina husiswa na Mohammed Yusuf, Malimu wa madrasa ambaye aliongoza tawi la vijana wa siasa kali miaka ya 1999 huko Maiduguri. Japo kua chimbuko lake haswa ni mwaka 2002 pale Yusuf na wafuasi wake walipoa amua kuondoka Maiduguri kuelekea jimbo la jirani la Yobe, kwa kile walicho kielezea kama kupinga vitendo vya rushwa vilivyo ighubika jamii ya Kinaigeria. Kundi likajaribu kuunda Taifa ndani ya Taifa, ambapo litaongozwa kwa misingi ya uislam.

Sababu za kukua kwao

Kuna sababu nyingi za kukua na kushamiri kwa Boko Haram, ila sababu kubwa na ya msingi ni udhaifu wa Serikali ya Nigeria. Boko Haram ingeweza kuondolewa wakati inaanzishwa kama isingekua udhaifu na rushwa iliyoighubika polisi na mfumo wa mahakama. Mara kadhaa viongozi wa kundi hilo wamekua wakikamatwa, ila waliachiwa kwa dhamana na hawakuwahi kushitakiwa tena.

Geografia ya eneo lao la kimkakati ni sababu nyigine ya ukuaji wao. Kundi hili linafanya shughuli zake ktika jimbo la Borno lililopo kaskazini mashariki mwa Nigeria. Jimbo kubwa ambalo linapakana na Chad, Cameroon, na Niger. Kuna njia za panya nyingi sana zinazotumika kupitisha silaha kutoka nchi jirani. Eneo hili lilikua sehemu ya himaya ya Kanem, ambalo lilikua eneo la kiislam chini ya utawala wa Sayfwa mwaka 1085. Kwa hiyo mtandao wa kibiashara na elimu ya dini ya kiislam zimeshamiri katika eneo hili kwa mika mingi.

Jihadi iliyo anzishwa na Shehu Usuman Dan Fodio ilianzisha ukhalifa wa Sokoto. Ukhalifa huo ulitanda kuanzia kaskazini mwa Nigeria na kuingia katika nchi za jirani na kudumu kuanzia mwaka 1802-1812. Boko Haram walitumia historia hiyo kuwaunganisha watu na kuwafanya askari wao waonekane wa maana.

Kundi linatazamwaje nje na ndani ya Nigeria

Mwanzo wa chimbuko la kundi lilikuwa linatumia vifaa vya kimagharibi kama redio, video na kadhalika, watu hawakulichukulia kundi hilo kwa uzito mkubwa, manake hata viongozi wake walikua wakitumia magari ya kifahari ya kimagharibi, na hata kuishi maisha ya kimagharibi, pia viongozi wao walikua na uhusiano mzuri na wakuu wa majimbo mbalimbali Nigeria. Kundi lilianza kua la kishari mwaka 2009 pale serikali ilipo wavamia na kumua kiongozi wao.

Mataifa ya nje hufikiria kua umasikini wa kaskazini mwa Nigeria ndio uliopelekea watu wengi kujiunga na boko Haram, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine ni kweli japo eneo hilo lina uchumi mzuri usio rasmi ambao hauonyeshwi kwenye takwimu. Kuzorota kwa uchumi usio rasmi kwa kukosa miundo mbinu stahiki toka serikalini kumesababisha watu kujiunga na kundi hilo. Wanasiasa na wafanyabiashara, vipande kutoka kwenye mabenki na masoko pamoja na madau wanaolipwa kwa kushikilia mateka, vimekua vikisaidia kulifadhili kundi.

Sababu nyingine iliyochangia kuendelea kwa Boko Haram ni kuchanganya uislam na imani za jadi na kutumia baadhi ya aya za korani kuagua. Viongozi na wafuasi wa Boko Haram wana uelewa mdogo wa Uislam, na hawatumii muda mwingi kuelimisha umma, na hivyo wanapotosha kuhusu wanacho kiita “jihad”.

Mwanzilishi wa kundi maalimu Mohammed Yusef, alikua muhubiri mwenye mvuto sana, alie anza kuhubiri katika msikiti wa mfanyabiashara tajiri wa kinaigeria aliekua rafiki wa familia ya Bush.

Mohammed Yusef alifukuzwa kwenye msikiti huo baada ya kuanzisha mahubiri ya kupinga umagharibi na akaanzisha shule na msikiti wake, lakini Boko Haram, haikuwahi kuanzisha shule rasmi ambayo ilifuata theolojia flani. Mohammed Yusef, ni muumini wa mafundisho ya Ibn Taimiyyah ( msomi wa kiislam na theolojia wa karne ya 13, alie wavutia akina Muhammad ign Abd al-Wahhab na wengine).

Boko Haram wanajitanabaisha na mafundisho ya Sayyid Qutb na Abd al-Wahhab, lakini hakuna ushahidi kama kuna wana theolojia wengine wa kiislam ambao kundi limevutiwa na mafundisho yao.

Kundi kama Boko Haram wanajijengea taswira ya udini ili kupata msaada kutoka nje, ili kuhalalisha wanacho kifanya, Boko Haram walianza kwa kuwaua wakristo na kushambulia makanisa, kwa makusudio ya kutaka kuungwa mkono na waislam, kwa kisingizio cha mgogoro wa kidini uliopo Nigeria kati ya wakristo na waislam.

Lakini kwa uhalisia kundi limeishia kuuwa waislam wengi mara tano zaidi ya wakristo , na wameshambulia, kuteka na kuwanyanyasa kijinsia wanawake wa kiislamu mara kumi zaidi walivyo fanya kwa wakristo ( wanafunzi wasichana 274, kutoka shule ya Chibok na wanawake zaidi ya 2,000 hii ni kutokana na report ya Amnesty internation)
 
Report ni ya amnesty international, sasa tujadili nini hapo!? Report yenyewe inatoka kwenye hizo nchi zilizo na chuki na boko haram, leta report ya vyombo huru visivyotungamana na upande wowote
 
Report ni ya amnesty international, sasa tujadili nini hapo!? Report yenyewe inatoka kwenye hizo nchi zilizo na chuki na boko haram, leta report ya vyombo huru visivyotungamana na upande wowote
Jamaa unachekesha kweli, ni nchi gani ambazo zitaacha kuwa na chuki na Boko Haram?vipi unawaunga mkono kwa mambo yao nini?

Unataka wapendwe kwa kipi kizuri walichofanya?
 
Report ni ya amnesty international, sasa tujadili nini hapo!? Report yenyewe inatoka kwenye hizo nchi zilizo na chuki na boko haram, leta report ya vyombo huru visivyotungamana na upande wowote

Toa report yako wewe inayoung amkono ubakaji, utekaji, uzuiaji wa wanafunzi wa kike kusoma, mauaji ya watu wasio na hatia eti na usitaarabu wa kiislamu usioonekana katika maisha ya binadamu. Unayoshida isiyo ndogo.

Inahitaji kuwa si wa kawaida kuandika ulichokiandika.
 
Hayo ya ubakaji na kuzuia wanafunzi kusoma umeyatoa wapi kama sio media za mabwana zako wazungu!? Leta habari zilizotolewa na chombo huru
 
Haya makundi yanatetea dini kwa misingi inayobarikiwa kabisa na mafundisho ya dini hiyo
Ndio, mfano upuuzi anaoufanya magufuli unadhani ungekuwa upande wenu mngevumilia!? Haki ya upande mmoja inapominywa ndio inafikia hatua hizo
 
Report ni ya amnesty international, sasa tujadili nini hapo!? Report yenyewe inatoka kwenye hizo nchi zilizo na chuki na boko haram, leta report ya vyombo huru visivyotungamana na upande wowote
Hivi we unawapenda boko haram? Kwa lipi hasa?
 
Ndio, mfano upuuzi anaoufanya magufuli unadhani ungekuwa upande wenu mngevumilia!? Haki ya upande mmoja inapominywa ndio inafikia hatua hizo
Kwanza nyie watu hamna shukurani kabisa.
Mmepewa vibali vya kuingiza sukari nchini toka nje nyie wenyewe dini nyingine zote hawakupewa mbona hawakulalamika??

Mmepewa majengo ya Tanesco mkabadili kuwa Chuo chenu mbona hamkulalamika, Halafu chuo chenyewe hakitaki kujiunga TCU, wakati vyote vimeungwa TCU na hakna anayelalamika.

Punhuzeni kulia lia, jengeni mfumo
 
Report ni ya amnesty international, sasa tujadili nini hapo!? Report yenyewe inatoka kwenye hizo nchi zilizo na chuki na boko haram, leta report ya vyombo huru visivyotungamana na upande wowote
boko haramu inachukiwa na kila mtu ambaye anaitakia hii dunia mema, cha muhimu ni kusema kuwa ukiwa unatoa taarifa usiwe unachanganya na mihemko yako ya chuki zikaharibu taarifa
 
Kwanza nyie watu hamna shukurani kabisa.
Mmepewa vibali vya kuingiza sukari nchini toka nje nyie wenyewe dini nyingine zote hawakupewa mbona hawakulalamika??

Mmepewa majengo ya Tanesco mkabadili kuwa Chuo chenu mbona hamkulalamika, Halafu chuo chenyewe hakitaki kujiunga TCU, wakati vyote vimeungwa TCU na hakna anayelalamika.

Punhuzeni kulia lia, jengeni mfumo
Hatutaki kusaidiwa lolote, tunataka haki tu, hivi unaweza kutuambia kwanini serikali inatoa pesa kanisa katoliki ya MOI na si dhehebu lolote nchini!?
 
Hatutaki kusaidiwa lolote, tunataka haki tu, hivi unaweza kutuambia kwanini serikali inatoa pesa kanisa katoliki ya MOI na si dhehebu lolote nchini!?
Kanisa katoliki ya MOI ndio nini we dogo acha kukurupuka?

Au ulikua unamaanisha MoU iliyosainiwa kati ya Katoliki na Serikali??
 
Kanisa katoliki ya MOI ndio nini we dogo acha kukurupuka?

Au ulikua unamaanisha MoU iliyosainiwa kati ya Katoliki na Serikali??
Huyu naye anataka kupewa uongozi?ukimuuliza hata hiyo MoU ni nini hajui ila katika kuitaja huko kwenye vikao vyao vya kahawa hadi makoo yanakauka
 
Hayo ni makundi ya wanasiasa yanayojificha kwenye mgongo wa Dini ya Kiislam.

Kwa ajili ya manufaa yao binafsi.

Uislam hautambui makundi hayo
 
Boko Haram ni jina ambalo hutumika kulitambulisha kundi lijulikanalo kama “watu waliojitolea kueneza mafundisho ya mtume na jihad

Nimeacha kusoma katika hii sentensi!...
"Boko Haram ni jina ambalo hutumika kulitambulisha kundi lijulikanalo kama “watu waliojitolea kueneza mafundisho ya mtume na jihad"

naona unaongea kwa uhakika "watu waliojitokeza kueneza mafundisho ya mtume na jihad"

- unajua nini maana ya jihad ....?

- unajua ayat ya kwanza kushushwa ni "iqra" "SOMA"

- Unaja mtume wetu alisema "katafuteni elimu japokuwa ni mbali mpaka china" >china hakuna waislam ni elimu gani tumeambiwa tukatafute"

BOKO HARAM WAPO AGAINST EACH AND EVERY TEACHING OF OUR HOLLY PROPHET !...

SO FAR WAHANGA WAKUBWA WA BOKO HARAMA NI WAISLAM

1) Wanachafua image ya waislam kwa kujiita waislam

2) kila ukisikia mtu kajitoa muhanga ni ndani ya msikiti au maeneo wanayokaa waislam wengi ..

wana agenda gani na waislam na wao wanajiita waislam...

Back
Top Bottom