LHRC, Sheikh Ponda wataka uchunguzi wa kina kifo cha mtuhumiwa wa ugaidi anayedaiwa kufia kwenye mikono ya Dola

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), wametaka ufanyike uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha kifo cha marehemu Sheikh Said Mohamed Ulatule ambaye anadaiwa kufia gerezani akiwa anatuhumiwa na makosa ya Ugaidi.

Wito huo ambao umetolewa leo Machi 15, 2023 na Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Ponda Issa Ponda, wamesema kuwa uchunguzi huo ufanyike na ukawe endelevu kwa watu wote wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya Dola.

"Ufanyike uchunguzi wa kina (inquest) juu ya nini hasa chanzo cha kifo cha marehemu Sheikh Said Mohamed Ulatule na utaratabu huo uendelee kwa watu wote wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo Sura ya 24 ya mwaka 1980 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019" amesema Mkurugezi Mtendaji LHRC, Anna Henga.

Kwa upande wa Sheikh Ponda amesema kuwa taarifa za kifo hicho zinaibua maswali mengi kwa wadau wa haki pamoja na familia ya marehemu, hata hivyo amedai kuwa watuhumiwa wengine zaidi ya 100 wanaokabiliwa na mashtaka ya Ugaidi Bado wapo kwenye magereza tofauti Nchini kwa miaka sita hadi 10 na kuwa hatma yao haijulikani.

Katika wito huo wamedai kuwa ni jambo la kushangaza kuona watuhumiwa wanakaa gerezani kwa kipindi cha mika sita na zaidi bila uchunguzi wa kesi zao kukamilika kama inavyoelezwa na upande wa mashtaka.

Aidha kufuatia jambo hilo wameitaka ofisi ya Taifa ya mashtaka chini ya DPP, kuwafutia mashtaka watuhumiwa au kuhakikisha wanapeleka uchunguzi mahakamani ili haki iweze kutendeka kwa mujibu wa Sheria.

Sanjali na hoja hizo Wakili Anna Henga amesema kuwa hawaungi mkono vitendo vya ugaidi bali wanachosisitiza ni haki kutendeka kwa watuhumiwa sio kutumia tuhuma hizo kuwakosesha haki muhimu.

Ikumbukwe ilidaiwa kuwa Sheikh Saidi (80) aliyekuwa akituhumiwa kwa kesi ya ugaidi akishikiliwa kwenye mahabusu ya Gereza Kuu la Ukonga, jijini Dar es Salaam alianguka na kufariki akiwa mbele ya Mh. Jaji . Tukio hilo lilidaiwa kutokea March 4, 2023.

Taarifa ya awali iliyodaiwa kutolewa Jumanne, Machi 7, 2023 na Katibu Mkuu wa Shuraa ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, zinaeleza kuwa Sheikh Ulatule, alifariki dunia mbele ya Jaji huyo Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, tarehe 4 Machi 2023.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe huyo mlalamikaji bado yupo?! 😳😅😅😅

Mbona hakusikika awamu ya Tano?! 😅
 
Back
Top Bottom