jembe afrika
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,603
- 3,774
habari wajamvi, kumetokea na sinto fahamu na kampuni hii ya wahindi na madere wake. chanzo cha msuguano huu ni malipo ya makumbusho ya olduvai.anadai madereva wake wanaletarisiti bandia lakin hiyos sababu. mimi nionavyo huyu bwana anahalingumu tu ya kibiashara sasa anatafuta njia mbadala yakuzulumu haki za madereva hao na mpaka sasa watatu wako ndani kisongo. nafikiri hata hao madreva wenyewe hawana ushirikiano mzuri kiasi kwamba kila kukicha manyanyaso yanazidi.
mafuta shida,allowance mbovu.wahindi ni wanyanyasaji sana,washukuru nyerere hayupo.
mafuta shida,allowance mbovu.wahindi ni wanyanyasaji sana,washukuru nyerere hayupo.
HOW LEOPARD TOURS IS TORMENTING HIS DRIVER GUIDES !!!! YOU MUST READ THIS PLEASE
Leopard tours Mr Fazal asema Serikali iko chini yake !! HAOGOPI MTU
WATANZANIA SOMENI HII INASIKITISHA INGAWAJE NI NDEFU SANA
MATAIRI MABOVU KUTOKA INDIA:
Tunasikitika sana kuona kuwa katika kampuni hii ya Leopard mwanzoni tulikuwa tukitumia matairi aina ya Yana na hapakuwa na tatizo lolote wakati mtu unaendesha gari na ukapata flat tyre hilo tairi lilikuwa haliaribiki maana unakuta mtu uko speed 80 kisha pancha sasa mpaka usimame inakuwa kuchukua muda kidogo, ila sasa workshop manager Mr Gulam na fundi mkuu Mr Regi ambao kwa faida yao na kamisheni -wanayo pata kutoka katika kampuni ya matairi ya MRF wameishauri kampuni na sasa wamebadilisha wametufungia matairi hayo Ya MRF kutoka india ya bei rahisi, kusema kweli tunapata shida sana maana ukipata pancha ukiwa katika speed yoyote kuanzia 50 hadi 80, mpaka usimame tayari tairi halifai limekwisha,
cha ajabu unaambiwa wewe dereva wa hilo gari uwajibike kununua tairi mpya, halafu hapo hapo hilo tairi ambalo wametoa bovu workshop manager bwana Gulam anawarudishia kampuni ya matairi ili wampe lingine sasa jamani sisi tumeshalipishwa matairi mengi na cha kushangaza unakatwa laki nne kwenye mshahara wako bila hata kuandikiwa risiti yoyote wala kupewa muda wa kujitetea ajabu sana, na anaye kata hela hizi ni accountant anayeitwa Mr Mbaga huu ni unyanyasaji usioweza kuvumilika tena na muda sio mrefu tutampandisha kizimbani na tayari tumefungua kesi na muda wowote ataitwa mahakamani kujibu tuhuma na ushahidi tunao ambao tumepiga photocopy invoice zote ambazo watu wamelipishwa tokea kipindi cha nyuma huko.
Sasa tunajiuliza kuwa sisi madereva utaliii hapa leopard tours je tuna ubia na kampuni? Mbona hata hamna siku hata moja tumeshawahi kupewa bonus au kuitwa kugawana faida ya mwaka kama mtu una nunulia gari la kampuni vipuri? Tunastahili kupewa shares zetu haraka iwezekanavyo, kampuni hii inajiendesha kwa faida asilimia mia moja, bila hasara hata kidogo,kwani wear and tear zote tunazilipa sisi madereva utalii,
-Hii ni sawa kisheria? Ingawaje tunajua kwa leopard tours hakuna sheria inayo weza kuwa juu yake kwa sababu ana pesa nyingi sana na hakuna mahakama inayoweza kushindana naye na mara nyingi hata ikitokea anayo kesi na dereva mara nyingi yeye Mr Fazal wa leopard tours ndiye anayetoa hukumu kwa nguvu ya pesa alizo nazo kuwa mtu huyu afungwe au aachiliwe au apewe mdhamana. Sasa tunajiuliza ni nani mwenye nguvu Leopard tours (Fazal ) au sheria /mahakama /polisi-?
Nashangaa sana Kwa kweli kuona yeye Mr Fazal amekuwa akitugandamiza kwa miaka mingi sana kwa kulipa matairi ambayo ni mabovu utafikiri tuna ubia na Leopard tours halafu kipindi chote hicho ametulipisha hakuna aliyetulipa sisi ila leo hii hii ishu ya olduvai imetokea kaamua kutukata mishahara yetu nusu nzima na kutulazimisha kusaini kitu ambacho hakiko-!!!
MASIKITISHO YETU KWA JESHI LA POLISI
Jamani kuna sheria gani ambayo inamruhusu polisi especially RPC na OC CID kushinda Leopard tours office na kuhamishia ofisi yao hapo leopard ??? tunajua mmepewa pesa ya kutosha polisi na Mr Fazal mpaka mnatumia cheo chenu vibaya badala ya kuwa upande wa wananchi mnakuwa upande wa wenye hela inasikitisha sana maana polisi wamejua kuwa huyu mr fazal wa leopard ni mfadhili wao mkuu sasa wanatumia hiki cheo chao cha polisi ccm kututesa kwa kweli tumechoka sasa polisi tunawaomba msimamie haki na sio kusimamia upande wa watu wenye pesa, maana mnatukera polisi mmekuwa ndio sababu ya watu kusaini na kukubali vitu visivyo kuwa kweli maana hatujawahi kuona polisi mkuu kama RPC ndani ya ofisi ya mtu binafsi eti ana meza yake na wanabunduki wanalazimisha watu kusaini mikataba ambayo wanajua ni maslahi yao.
Kusema kweli inasikitisha sana hatujui sheria inasemaje kwenye hili kama polisi wanaruhusiwa maana Mr Fazal akikuita ofisini mwake anaita na gari la polisi wanakuja na bunduki wanapaki hapo leopard tours ofisini, ukiambiwa usaini mahali hata kama utaki unabebwa na gari la polisi na Fazal wa leopard anatoa tu amri kuwa peleka ndani huyu mbwa akae huko mpaka nitakaposema yaana huyo fazal mhindi mpaka atakapo amua kumtoa na cha kusikitisha anasema wazi msimpe dhamana yoyote,
yaani uwezi amini mtanzania mwenzetu Huyu mhindi akisema usipewe dhamana hupewi na hakuna wakili yeyote anayeweza kukutoa hata angekuwa anajua sheria vipi sasa sisi wafanyakazi tukiona hivyo ambao hata hatujui sheria yoyote unakubali usaini chochote hata akisema anamchukua mkeo maana usiposaini utawekwa ndani na hakuna mdhamana sasa jamani tunaomba MKUU WA POLISI TANZANIA IGP utusaidia angalau maana hii imezidi huyu mhindi anakuja tanzania kututesa watanzania kiasi hiki na inawezekana haujalifahamu hili tunaomba utusaidie ulikemee hili maana tumechoka na tuko tayari sasa kufanya kitu ambacho kila mtu mtanzania atashika kichwa ila kabla hatujafikia huko tunakuomba IGP maana tunajua wewe ni mzalendo mwenzetu na sio kama hawa polisiwako wa Arusha wenye kujaa rushwa ya wahindi, tusaidie tafadhali tusaidie hatuna hela yoyote ya kukulipa ila tumia cheo chako kutusaidia ingawaje yeye Fazal ameshasema kuwa akikuhitaji hata wewe ni ndani ya saa moja umefika ofisini kwake,
sasa jamani hii kweli ni dharau sana kwa jeshi la polisi na kwa nchi yetu kudhalilishwa na namna hii na mhindi mwenye pesa, tunajua anayo pesa ila ni za kwake na mke wake na sio hazitusadii chochote, tusaidie tafadhali IGP kama kweli unaliweza maana tumeshachafukwa na sasa tutafanya maamuzi magumu ili tuilazimishe serikali kulitazama hili jambo Fazal huyu mhindi anayetuita eti sisi ni GoLo awezi kulichafua jeshi la polisi namna hii, inasikitisha sana. Kusema kweli tumechoka tumechoka sasa Fazal maana sasa imekuwa kama fasheni ukikataa kitu ofisini kwake unawekwa ndani jamani hii kweli ni uungwana-?
watanzania tusaidieni. Yaani jinsi alivyo tuchosha kwa kututesa hata kama leo hii tukakuta Fazal kapata ajali na ajafa vizuri yaani tungechukua jiwe kubwa na kummalizia hapo hapo. Tumechoka yaani tumechoka polisi Dar tusaidieni kama mnaweza kupambana na huyu mtu hatari mwenye hela mpaka anaumwa mpaka anatukana serikali, ila tunawaomba mnapokuja hapa arusha au mnapo watuma polisi kulifuatilia tumeni polisi ambao wameridhika kidogo wenye pesa maana watamwagiwa pesa na wao wanaweza kuhamia hapo leopard kama hawa wa arusha walivyo fanya.
CHA AJABU >
Ni kwamba amegundua njia mpya ya kuwadhulumu wazee wetu aliofanya nao kazi kwa miaka 30 sasa anachokifanya nikwamba anawalazimisha kusaini kuwa walikuwa wanamuibia kisha anawalazimisha kuandika barua ya kuacha kazi ili mtu yeyote asipate haki yake jamani hii ni uonevu sana maana mpaka sisi wafanyakazi tumekosa ni wapi tunaweza kupeleka malalamiko yetu maana hatuna tena imani na vyombo vya sheria vya Arusha,
kama polisi sasa wamefanya leopard tours ndo ofisi yao basi sisi wanyonge hatuna haki ni kufungwa tu tusipokubaliana na anavyo taka maana ukikataa tu unaonyeshwa gari la polisi hapo nje kusema kweli tunarudia tumechoka kuona Fazal huyu mhindi anavyo tutesa na hatuna mahali pa kushitaki wala hakuna sasa hata mwanasheria ambaye anaweza kusimama mbele yake huyu mhindi , sasa tunarudia tutalazimika kuchukua maamuzi ambayo yatasikitisha wengi watakapoyasikia hilo inabidi Fazal ulielewe sasa nadhani enough is enough uwezi kulidhalilisha jeshi la polisi kwa pesa zako, hii haikubaliki, IGP uko wapi arusha jeshi la polisi limenunuliwa na wahindi wenye makampuni ya tours, hii ni mbaya ebu toa tamko maana sasa inatulazimu kuchukua maamuzi mabaya.
Jeshi la polisi la arusha sio la wahindi ni la watanzania walio wengi yaani tunasikitika heri mzee wetu mwalimu angekuwa hai labda- tungepata msaada maana ingekuwa vigumu kwa wahindi kumhonga,
Na pia tunaomba Serikali ingetoa pesa ya kutosha kutengeneza magari ya polisi yenyewe kuliko kumpa huyu mhindi awatengenezee maana sasa imekuwa kama Fazal wa Leopard tours ni mfadhili wa Serikali kw akuwatengenezea magari yao. Na ndo maana Fazal anadiriki kusema kuwa Serikali yote iko chini ya miguu yake na hakuna anayeweza kumfanya kitu maana kama anaweza kumpigia Raisi simu ni nani anayeweza kumwambia kitu-?????? na pia kama anaweza kumpigia RPC simu nani anayeweza kumwambia kitu-????
AJALI:
Tunasikitika sana maana baadhi ya madereva wenzetu waliopata ajali wengi wao, walilipishwa gharama zote za kutengeneza gari, unaambiwa ni uzembe wako na cha kushangaza ni kwamba hata kama aliyekugonga amekiri kulitengeneza hilo gari wao huwa wanapokea hizo pesa na bado wewe dereva wa hilo gari utawajibishwa kulitengeneza hilo gari jamani sasa sisi tunauliza je inamaana hakuna insuarance inayolinda magari au sisi madereva tumekuwa insuarance za kampuni? Tukisema kuwa Leopard tours hailipi insuarance na insuarance zake zote ni feki je tutakuwa tumekosea? Maana kusema kweli hii kampuni imekuwa ikikwepa -kulipa kodi zake katika serikali, na cha ajabu hakuna mtu yeyote anayeweza kuthubutu kuja na kukagua hapo Leopard(tunamaanisha auditors wa serikali ) maana huyo mtu ataishia kuwa tajiri maana atapewa fungu na ushaidi tunao,
kwa baadhi ya inspecta wa arusha polisi ambao walipewa jukumu la kukagua magari ya leopard alipewa fungu na kufanya ukaguzi pale pale ndani ya ofisi yake kituo cha polisi, yaani kuandika tu makaratasi maana alipewa fungu la kutosha kupotosha ukweli na huyo polisi amenunua gari jipya, pia hiyo inadhibitisha kuwa magari mengi ya leopard tours ni ya wizi na ndo maana chesis namba na kwenye kadi ya magari hayo ni vitu viwili tofauti kabisa,na hata sio mara moja au mara mbili magari ya polisi yanakuja hapo garage kufanyiwa service na kubadilishiwa matairi kwa gharama za Leopad tours kusudi wafanyakazi waendelee kuteseka wasipate haki pindi kunapotokea tatizo, na hii imejidhihirisha wazi kwani RPC wa arusha amelazimishwa na kupewa amri na Fazal wa Leopard kuwa hao watu walioko ndani wasipewe chakula wala mtu yeyote asiruhusiwe kuwaona,hapo ndipo utajua kuwa serikali hii ni dhaifu kuanzia juu mpaka chini, yenye na wahindi wachanche wenye hela.
ukweli unaweza kujulikana kama serikali ingeweza kutuma mtu ambaye hana njaa kuja kukagua hayo magari, maana kusema kweli kama unataka kuwa tajiri omba Mungu utumwe na serikali kuja kukagua magari ya leopard tours maana utaishia kuwa tajiri bilionea maana utapewa fungu kubwa kupotosha ukweli na hapo ndo maali mapolisi wengi wa arusha wamechukulia utajiri wao,
Na ndo maana magari yote ya mapolisi binafsi na yote ya polisi hutengenezwa hapo leopard tours garage bure iwe ni rangi au matairi au service huwa wanatengenezewa bure,hapo tunashindwa kuelewa serikali yenyewe haina garage yake yenyewe kutengeneza magari yake yenyewe-??? -sasa sisi tunahoji kama magari ya polisi hutengenezwa bure hapo leopard tours garage je Kuna mtu anayeweza kuishitaki leopard- tours-? jibu unalo
MAFUTA-:
Tumekuwa tunashida ambayo sasa imedumu kwa miaka kadhaa hapa Leopard tours, maana kuna mshelisheli mmoja ambaye aliajiriwa kama fundi mkuu wa garage Mr Reginald , kusema kweli amekuja na mambo mengi ambayo yametuumiza sisi kama madereva na hata kupelekea madereva wengi kuishia kujaza mafuta kwenye magari yao kwa kutumia pesa zao za mifukoni , maana unakuta gari lina miaka 25 hapo leopard yeye anacho kifanya analipiga rangi mpya na kuweka viti vipya na vioo vipya kisha consumption anasema lita moja inaenda kilomita 9 hadi 10 jamani watanzania hii ni sawa-? maana gari lina kilomita laki tatu eti linaenda kilomita 10 kwa lita 1-?! kusema kweli imekuwa ni ajabu na inashangaza sana, maana tumelalamika tunaambiwa kama utaki kazi ondoka, na masikini madereva wengi wanaamua kuweka mafuta wenyewe kwa hela zao kulinda kazi,
Sasa cha ajabu leo hii tunaambiwa eti mafuta wanatupa mengi sana mpaka eti hatuweki mafuta- mengine tunayauza sasa jamani kwa mahesabu yao wao ya kilomita 10 kwa lita 1 wanaona mafuta yatosha wakati kwa usahihi hayo magari ya leopard tours yanaenda kilomita 6 kwa lita 1, ebu watanzania angalieni jinsi huyu mhindi anavyo tunyanyasa, na kusema ukweli hatuna mahali pa kushitaki wala kulalamika maana kama ni polisi ameishikilia na siku hizi wakuu wa polisi wanashinda hapo ofisini mwake na yeye ndo anawapangia anachokitaka wakifanye, simnajua polisi wetu wanavyowanyenyekea wenye pesa-!!!! kwa jinsi tulivyo choka tutachukua hatua mkononi maana Rais wetu wa Jamhuri ya muungano alisema tuchanganye na za kwetu, kwa hiyo tutachukua hatua mkononi tutafanya maamuzi magumu kama ya alshabab,
Halafu Mr Fazal anatutisha hajui kuwa akibana mafuta wageni wake wataishia kuona miti na majani-? nani atapata hasara-???
ALLOWANCE
Kwa miaka mingi sisi madereva wa Leopard Tours tumekuwa tukilipwa shs elfu 20,000. Kwa siku kama night allowance tunapokuwa tumesafiri na wangeni porini, na cha ajabu unakuta unaposafiri kule mahotelini tunapolala tunalipa shs. 10,000 hadi shs. 20,000 kwa usiku mmoja, sasa jamani huyu mhindi ametulipa shs 20,000 ebu watanzania angalieni hapo kama wewe ndo dereva wa Leopard utabakia na shilingi ngapi hata ya kujinunulia soda ? au utawaachia familia yako shillingi ngapi nyumbani ?
Halafu cha ajabu huyu tajiri yetu hawezi kutofautisha safari allowance na Safari imprest!!! Kana kwamba yote anaita ni safari allowance, aige tu mfano wa kampuni kama KIBO GUIDES au Thomson safari wanavyo walipa wafanyakazi wao kwamba safari allowance ni ya kwako kwa ajili umetoka nje ya kituo na kuacha nyumbani kwako, na Safari Imprest utaitumia safarini kwa kulipia malazi, chakula , kuosha gari, na kulinda gari kama litapata shida yoyote kama vile pancha. Kwani kwa sasa ukitengeneza pancha ukirudi na risiti Mr Regi na Mr Gulam wanasema umeisaidia Kampuni hulipwi chochote.
-halafu cha ajabu huyu mhindi kamuajiri mmama mmoja anayeitwa AIDAH -na anamlipa kwa mwezi milioni tatu ni mfanya kazi kama sisi lakini eti -amemshauri bosi kuwa lazima tuwe tunaosha magari tukiwa porini kila siku na kusema kweli kuosha gari porini ni kati ya shs 4,000 na shs 5,000 sasa ebu angalieni hapo jamani kama umesafiri siku saba utaosha gari kwa shs 35,000 na wewe umepewa shs 120,000. Kwa siku saba, utabakiwa na shs. 105,000. Utalipia malazi shs. 105,000. Hapo umelala kwenye hoteli za shs. 15,000. Kwa siku. Na mpaka hapo hautabakiwa na kitu mfukoni kumbuka hapo haujaacha chochote nyumbani, sasa jamani na kama unalala kwenye hoteli za shs 20,000. Kwa siku basi unawajibika kutoa hela zako mfukoni ujilipie malazi na kuacha nyumbani, sasa jamani hili watanzania ni sawa? Na kama ni hivi dereva ataacha kuwa na akili ya kuiba????
Au dereva ataacha kusimama dukani?? Tunaamini hii ngoma imelia muda karibia inapasuka na pasuko lake ni balaa maana ni kubwa mno kila mtu atashangaa, -Kweli sisi tunajua hii kampuni ni ya Fazal sasa iweje leo hii mwanamke kutoka huko kwenye nchi za kifaransa aje amshauri Boss wetu ujinga na boss naye anamsikiliza , hiyo ni akili?
Ila nadhani Mr Fazal ni tajiri sana kwa sasa na akumbuke kama angekuwa ameajiri madereva ambao sio professionals asingekuwa hapo alipo na pia utajiri wake wote ni sisi madereva utalii tumemfikisha hapo alipo. Lazima alijue hilo, Ukitulinganisha na makampuni mengine wao wanalipwa vizuri sana kwa siku kati ya dola za kimarekani 30 hadi 70 na hilo Fazal analijua. Lakini kwa sababu ya tabia za kihindii za unyanyasaji walizo nazo kwetu sisi watu weusi ambao anatuita MAGOLO basi ameamua kutugandamiza mpaka mwisho.
Mishahara kapunguza, alawonce elfu 20, nssf hakuna, unasainishwa karatasi tofauti na unacholipwa, halafu wageni wote wanaambiwa wasitoe tipu, sasa huyu dereva ataacha kuwa na akili ya kuiba?
Au unatulazimisha kuwa waizi kama wewe jinsi unavyo waibia serikali? Au unafikiri hatujui? Mwisho wako unakuja, tumeamua kukuanika wazi kwa kila mtanzania ili wakujue jinsi ulivyo mbaya wewe Fazal, na mdogo wako ambaye yuko huko garage ndo manager na yeye kazi yake ni kuwapa wafanyakazi wa kike mimba na hilo sio siri maana mfanyakazi akimkataa hana kazi jamani mbona mnawafanyia hivyo wanyonge?
Cha kushangaza ni kwamba Mr Fazal -yuko tayari kutengenezea polisi magari yao yote na kuyavalisha matairi mapya na kuyapiga rangi, sasa jiulize Fazal wa leopard tours je anaubia na serikali au labda serikali iko chini yake??? Maana tunaamini serikali inatoa fungu kwa ajili ya magari yake kutengenezwa sasa iweje leo hii mtu binafsi ndo anayatengeneza kwa hela yake binafsi jamani huoni hili jambo kama ni kupofusha macho ya serikali isione uovu anaoufanya kwa wafanya kazi wake.???
Na ndio maana ukishindwana nae jambo lolote atakuambia nenda popote utakapo kushitaki maana anajua kuwa serikali yote iko mikononi mwake, na ndo maana siku zote ukimuudhi atakuambia kuwa nenda popote utakapo na mara nyingine husema kuwa hamuwezi kunifanya kitu maana serikali yote iko mikononi mwangu, na hata ndo maana kama mtakumbuka miaka ya nyuma pale Impala Hotel arusha alimtukana Waziri wa nchi na magazeti yote yaliandika lakini hakuna kilicho fanyika kwake maana serikali iko chini yake CHEZEA PESA WEWE, kilicho fanyika waziri alipofushwa macho na pesa na yakaisha juu kwa juu, jamani ni lini tutapata serikali itakayo simama imara kujali maslahi ya mwananchi wake na sio kujali maslahi ya watu wenye pesa?
SAKATA LA OLDUVAI
Kawaida katika ratiba zetu za safari unapewa pesa kupeleka wageni katika bonde la olduvai kuliangalia. Sasa mara nyingi ukienda hapo unapewa risiti ya serikali ya njano, unaleta ofisini, sasa hatuelewi inakuwaje leo hii kazi za utalii zimepungua na Fazal kichwa kimeuma afanyaje sasa ametafuta njia ya kuwabana madereva wake kuwa huwa hawaendi eti Olduvai na badala yake wanafoji risiti na kurudisha ofisini, jamani sisi tunahoji kuwa kama kweli tungekuwa hatuendi olduvai si wageni wangelalamika??!! Na iweje unarudi na mgeni anapewa karatasi ya kumhoji kuwa amefanya kila kitu na mgeni ana andika amefanya iweje leo hii anaacha wageni wote wameondoka kurudi makwao na hela imeshaingia kwenye account yake, na ndo aanze kudai eti huwa hatuendi olduvai eti anataka tumlipe hizo pesa jamani watanzania hili si kumnyanyasa mnyonge?
Au analifanya hili kwa sababu anajua kuwa yuko juu ya sheria, na kusema ukweli- leopard tours iko juu ya sheria, ndo maana kuanzia ameanzisha hizi tuhuma polisi yote ya arusha inashinda hapo ofisini kwake na kufanyia kazi zake hapo ofisini na leopard tours inawaamrisha anachokitaka na cha kusikitisha jamani jamani eti polisi wanampigia saluti mr fazal wa leopard tours jamani hii ni haki au ni kulidhalilisha jeshi la polisi,?
Kutokana na shida za polisi wetu -Inasikitisha sana jamani, Na pia inasikitisha sana maana anajigamba kuwa akitaka kukufunga anaweza maana anapiga simu anatoa ofa tu ya fungu na kisha polisi wanakuchukua kama mboga na kukutupa jela, hakuna mdhamana mpaka atakaposema, yeye fazal wa leopard tours, na haya yote anayafanya akishirikiana na RPC wa mkoa wa arusha na OC CID, anayeitwa Faustin, -jamani wanasheria wasamaria mko wapi mtusaidie kama kweli katika ulimwengu wa sasa kuna sheria ambayo inaweza kuwa juu ya Pesa?
Maana hata juzi alikiri anaweza kufanya chochote maana serikali yote iko mikononi mwake na hakuna mtu anayeweza kumfanya kitu, maana hata alimuita mkurugenzi wa Tanapa Mr Kijazi Ofisini mwake sasa tunajiuliza ninani anayetakiwa kumfuata mwenzake ofisini? !ni mkurugenzi wa Tanapa au ni leopard tours(Fazal)? Na mara nyingi anatishia kwamba na uwezo wa kumpigia simu- Rais wa Jamhuri ya Tanzania na mara moja akapanda ndege akaja kumuona ofisini mwake, huu ni udhalilishaji na anapaswa achukuliwa hatua za kisheria lakini isitoshe, tungefurahishwa sana kama mkaguzi mkuu na mthibiti mkuu wa serikali (CAG ) angetuma timu yake kuja kukagua hizo risiti maana yeye Fazal wa Leopard sio auditor wa Serikali hawezi kujua Risiti Feki na Risiti original.
Na hivi tunavyoandika hizi habari kuna wenzetu ambao anawa tuhumu kwa hizo risiti feki za olduvai alimpigia mkuu wa polisi arusha na kumpa ofa ya hela kisha kumwamrisha kuwaweka lockup hao wenzetu mpaka atakapo sema yeye Fazal wa leopard tours na wasipewe chakula na wala mtu asiwaone mpaka atakapo amua yeye Mr Fazal,na ni kweli hao watuhumiwa walikaa polisi kwa muda wa wiki nzima bila hata kufunguliwa mashitaka yeye fazal ameamua tu wawekenni ndani mpaka atakapo amua, na baada ya Fazal na polisi wake kuona ndugu wa washitakiwa wanafuatilia wakaamua kufungua mashitaka eti washitakiwa wameiibia kampuni kiasi cha milioni mia nane??!! Kwa mwezi wa nane tu?? Jamani watanzania ebu tujiulize ukimuuliza leo hii huyu Fazal aonyeshe returns za mwezi wa nane ambao anasema eti amepata hasara milioni mia nane anaweza kuwaonyesha watanzania?
Au anayafanya haya kwa sababu anajua serikali hii iko mikononi mwake na hakuna mtu wa kuweza kumfanya kitu, maana ata juzi amesema eti mnamshitaki kwa mbunge wa Arusha ?! akadai kuwa mbunge ni kitu gani kwake, awezi kumfanya chochote yeye Fazal amekiri kuwa yeye ndo RPC wa mko, Yeye ndo Mkuu wa mkoa, Yeye ndo OC Cid wa mkoa , yeye ndo jaji wa mkoa na ndo maana hakuna wa kuweza kumshitakki na hata akikushitaki huwezi kupona atakufunga tu maana anayo pesa na Serikali hii iko mikononi mwake na akakiri kuwa anaye muhitaji awe ni polisi au nani akipiga simu tu lazima waje ofisini mwake na hili tumeliona alivyo fanya maana polisi kwa muda wa wiki mbili walihamishia ofisi yao hapo polisi, na cha kushangaza akimuita Dereva wake na kumwuliza jambo kama dereva akibisha chochote ana ita polisi ambao wanashinda hapo leopard tours parking na gari lao na kuwaambia kuwa chukueni hii takataka peleka ndani mpaka atakapo toa amri, ya nini kifanyike na hakuna mdhamana, watanzania yaani kusema kweli Fazal wa leopard akisema usipewe dhamana hupewi, na akisema muachieni basi hakuna polisi wa kuweza kufanya kinyume na alicho kisema sasa jamani nauliza kweli polisi yetu tunaonyesha picha gani?
Na pia cha ajabu ni kwamba hata hao madereva wa leopard hakuna ambaye anaweza kuthubutu kumshitakki Fazal wa leopard popote maana kama magari ya polisi yote yanatengenezewa hapo leopard tours garage sasa wewe unadhani unaweza kwenda polisi kumshitaki? Au utaishia kuwekwa ndani? Na ndo maana Fazal wa Leopard tours amethubutu kuzuia mishahara ya wafanyakazi wake tangia mwezi wa Decemba mwaka jana mpaka leo na hakuna aliyeweza kumshitaki maana mahakama zote ni zake, polisi yote ni yake, serikali yote ni yake dhuuuu inasikitisha sana.
-jamani wako wapi wanasheria wasamaria watusaidie hata hawa wenzetu wapewe mdhamana???? Maana tunajua kuwa ndio pesa ni kila kitu, na ndo maana imemfanya Mr Fazal wa leopard tours kuwa juu ya sheria na kuwa juu ya mahakama na kuwa juu ya kila kitu hapa nchini , lakini ni kweli kuwa huyu mhindi na pesa zake yuko juu ya sheria????? Hata kama mapolisi wetu wanampigia saluti ? aibuuuu. Shame Shame upon our police officers and RPC.
Fazal- ona uchungu eti risiti ni feki! Unajua kuna usemi unaosema kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka sasa kama wewe ni mwizi wanao au wafanyakazi wako wataaacha kuwa wezi-? na pia kama wewe Fazal unathubutu kuwalipa wafanyakazi wako mishahara mizuri kuanzia dola mia tano mpaka elfu kwa mwezi, sasa iweje kuwa unawasainisha wafanyakazi wako kwa kuwalazimisha kusaini mshahara wa laki moja na nusu huku unawalipa milioni huoni unadhulumu-?? au wewe haumwogopi mungu ambaye ni mtetezi wa wanyonge-??
kumbuka Fazal kuwa Mungu yupo na iko siku maana kwa kawaida ngoma ambayo ina pigwa sana itatoa sauti nzuri jinsi inavyoendelea kupigwa ila ujue wakati wowote itapasuka, jaribu kuangalia kina hitla wako wapi-? waliotingisha dunia-? sasa wewe unatingisha tu Tanzania unaona umemaliza dhu masikini nakuhurumia.-
Angalia hapa wewe umewadhulumu wafanyakazi wako kwa muda mrefu, kwa kuwasainisha makaratasi ambayo ni ya mshahara usiowalipa maana kama unamlipa mtu milioni unampa dereva asaini- karatasi ya kulipwa laki na nusu sasa huoni umedhulumu au ni kwa sababu mnatuita sisi weusi magolo-:?
Na na ndoo maana unatuona kuwa hatuna maana-?! na kumbuka kuna wazee ambao umeanza nao kwa miaka 30 sasa huoni hao wazee umewaua masikini-? maana wengi wao umewalazimisha kustaafu juzi na ukumbuke kuwa wengi wao walipoenda nssf wamekuta laki tisa tu-!!! na hapo wamefanya miaka 30 nawewe na ndo wamekufanya uwe hivyo ulivyo sasa kwanini uwadhulumu-? huoni kuwa wewe ndo ulitakiwa uwe wa kwanza kuwekwa ndani na polisi-??? yaani shukuru sana maana serikali hii ya tz iko chini yako vinginevyo ukikiona cha mtema kuni.
Na tukuulize swali pia kama umeshindwa kumlipa mtu haki yake huoni umeiibia serikali kwa kutokulipa kodi-??? sasa nani mwizi wewe Fazal- au madereva wako-??? na pia labda tuhoji kama umempa mtu hela ampeleke mtu makumbusho hiyo hela umeipata wapi-? kama sio ulilipwa na hao wageni-? na kama ulilipwa na wageni wewe nawe umetoa ilipwe panapo husika sasa kama haijalipwa umepata hasara gani au unafikiria sisi watanzania ni wajinga-? hatujui kuwa umetumia njia hii kuwanyima watu haki yao.-??
Kumbuka kuna Mungu wa wanyonge iko siku tu, atasikia kilio cha wanyonge walio wengi, maana wewe siunatumia pesa kumdhulumu mnyonge basi usiogope iko siku,
Na ndo maana sisi kwa sasa tuko kimya, maana hatuwezi kukushitaki popote maana umekwisha tuonyesha kuwa unanguvu na hakuna wakukufanya kitu maana serikali yote iko chini yako-!!, ila watanzania hili la kusema serikali iko mkononi mwake Fazal inaweza kuwa kweli maana kama alimtukana Waziri Arusha na ikarushwa kwenye kila gazeti ila mwisho wake ilikuwaje? waziri alikana hakutukanwa ingawaje mwanzoni alisema katukanwa, so watanzania huyu Fazal wa Leopard ndo Serikali ya Tanzania hakuna wa kumfanya kitu na ndo maana juzi alijigamba kuwa kama anaweza kumpigia Rais wa Jamhuri ya muungano simu na yeye akaacha anachokifanya na kuja ofisini basi mbunge wa arusha nini kwake.-!!? -hii inauma sana kwa mhindi kuitukana serikali yetu kweli haikubaliki.
MISHAHARA:
Jamani kwa kawaida kila mahali katika makampuni yote duniani hata kama hawamuogopi Mungu ifikapo mwisho wa mwaka mara nyingi wengi hutoa bonus ya mwaka kwa wafanyakazi waliofanya vizuri, sasa cha kushangaza hapa kwetu Leopard tours huyu mhindi asiyemwogopa hata Mungu, tangia mwaka jana amegoma kutupatia mshahara wetu na hali akijua kuwa mwisho wa mwaka kuna sikukuu na sherehe mbalimbali wazazi hupenda kukaa na watoto wao na kusherekea na pia hata January kunakuwaga na kulipia watoto ada za shule sasa jamani ebu watanzania angalieni asivyo na huruma huyu mhindi, mpaka sasa amezuia mshahara wetu na amesema kuwa nendeni popote mnapotaka hatoi mshahara, sasa na sisi tukiangalia ni kweli hatuwezi kufanya chochote kushitaki au kumwuuliza maana polisi iko chini ya pesa zake , mawaziri wako chini yake na ndo maana aliwatukanaga hata hawakufanya chochote, sasa tutafanyaje????
Tunaombeni ushauri wenu wa kisheria je kuna sheria ambayo inamruhusu mwajiri kumnyanyasa mfanyakazi kwa kutokumlipa pesa zake??? Maana ukisema kumshitaki utamshitaki mahakama ipi au polisi ipi ? maana yeye ndo mfadhili mkuu wa kuwatengenezea magari yao bure. Sasa utamshitakije mfadhili wa polisi kwa polisi inachekesha.
Na sasa ametumia kigezo hicho kwa kuwanyima wafanyakazi mishahara yao na pia amesema kuwa atawakata mishahara kila mtu dola mia Mbili kila mwezi- kwa muda wa miaka tano ili kulipa deni walilolisababisha la milioni mia nane kwa mwezi mmoja wa nane mwaka jana tu,- dhu!! Masikini hapa si ndo madereva wa leopard wamekuwa misukule!!??
NSSF -Fazal- umeiba muda mrefu Nssf zetu, bado ukaona haitoshi umeamua kutukata dola mia kila mwezi kwenye mishahara yetu miaka 5?!! Jamani muogope Mungu plz. Muda mrefu mr fazal amekuwa akitupatia mishahara mikubwa mizuri tu ila sasa ukienda kuchukua mshahara kama unalipwa dola mia 700 kwa mwezi sasa ukienda kuchukua mshahara unapewa karatasi ambayo imeandikwa laki na nusu usaini kama ndo mshahara wako sasa cha ajabu ukikataa kusaini ni kwamba kazi hauna sasa unakuta mtu anaamua kusaini ili tu apate mshahara ingawaje unapoteza haki zako, cha ajabu huyu mhindi amekuwa akifanya hivi kwa muda mrefu sana nay eye kwa upande wake anaona yeye sio mwizi wala hajaibia serikali hata kidogo?!! Sasa sisi tunakuuliza wewe fazal mhindi huo sio wizi ? mbona unatulaumu sisi sasa? Haujui kuna usemi usemao like father like son??,
WAFANYAKAZI WAHINDI
Hapo katika ofisi ya Leopard tours kuna wahindi wengi sana wanaofanya kazi na wanalala hapo ghorofani leopard tours hawana working permit ni fresh from India, anawalinda na kuwakumbatia na hata ofisi ya Uhamiaji Arusha inalifahamu hilo na wala haichukui hatua yoyote kwa sababu ya nguvu ya pesa, na mtu yeyote haruhusiwi kuingia hapo getini ofisini leopard tours ni mpaka simu ipigwe ahojiwe sana na kama ni mfanyakazi wa serikali basi ataishia sitting room akingojea fungu lake(Mlungula) arudi alikotoka kwa kweli hii ni aibu sana kwa nchi yetu kuongozwa na wenye hela. Hasa wahindi