Leo nimeshuhudia ajali ya bodaboda mpaka nimetetemeka

Kuna matukio hua wanafanya barabarani hadi unijuliza kwa nini serikali isipige marufuku usafiri wa bodaboda, lakini unakumbuka kwamba ujambazi utaongezeka una baki kusonya tuu, ndio maana Lema alisema bodaboda sio kazi ni laana
Serikali wangepiga marufuku bodaboda zisiingie katikati mwa mji hii itasaidia sana
 
Hii sio ajali mbaya.
Mimi nilishuhudia wamegongwa wamerushwa mtaroni, damu zinaruka juu kama bomba limepasuka, wanalia sana lkn wanaume wa dar wamezunguka wanapiga picha bila msaada,

Nilichukia mnoo na niliwatukana wote, niksmnyanyang'anya mama mmoja kanga nikashuka mtaroni kuwafunga damu na kuwatoa mtaroni.

Hiki kisa sitasahau
Una moyo wa kiungwana sana
Mungu azidi kukubariki daima ndugu yangu
 
Bodaboda wengi wanaocheza barabarani mama zao ni vijana,wao wakifa mama zao watazaa tena.
 
Aiseeh usafiri wa boda ni hatari, hawa ndugu zetu hawapo makini kabisa sheria za usalama barabarani hawazifuati kabisa.

Nimeshuhudia ajali ya hapa Chang’ombe Temeke, boda kapingwa na gari mlio umesikika mithiri ya bomu.

Huyu boda angekufa kwa uzembe wake yeye mwenyewe, taa za barabarani hazijamruhusu kupita yeye kaamua kupita kivyake kibaya zaidi mwenye gari alimuona alianza kupiga honi akiwa toka mbali.

Ashukuriwe Mungu yupo hai mwenye gari kajitahidi sana kumkwepa, ndugu zetu hembu kuweni makini mnahatarisha sana roho za watu.
Hawa jamaa hawajipendi.Ile ajali ya Kibo ,Ubungo alisababisha bodaboda

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom