Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Hakuna aliyefika hapa akawaza kurudi tena home labda awe kalogwa
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
Duh mbona wapo watu wengi tu walikuwa USA na sasa hivi wame-settle Tz? Ngoja niwaangalie vizuri labda wamelogwa!
 
Ndo JF mkuu take it easy.

I wonder unaingia chuo fall au spring maana fall shule nyingi zinafungua this week na zingine very soon. Spring ni January wanaweza kusema unawahi sana.

Naujua mziki wao hao jamaa maana niliucheza miaka hiyo mambo za rudi-go na tukatusua.

Ungesema mapema ningekushauri uende kumuona education advisor wao pale embassy hana la maana la kukwambia na sio lazima ila inakuongezea credit kwa consulars wakati wa interview. Good luck
Kuna mtu amepata Visa ya kuingia kusoma Spring Semester...amepata wiki hii, nimeshangaa, ni mapema mno.
 
Ndugu yangu watu wasikupandishe shaka visa sio ngumu as longer as huko na proper documentation . Pili Maisha ya US sikuhizi mwanzoni yamekuwa magumu sana maana ili kupata kazi unahita ID na Social security number ID kupata raisi tu ila social security number huwa hawatoi kwa wanafunzi hadi upate kazi shuleni na kazi za shule huwa ngumu kupata sababu foreign students wote wanazigombania na walio nazo hawaachi so uwe na mtu wa kukupoke au pesa ya kutosha kukuwezesha kwa muda mrefu kidogo.
Vyuo vingine vina foreign students wachache mno, unapata Social Security ID kirahisi.
 
Salamu kwenu nyote.

Awali ya yote napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha tangu naanza hizi harakati hadi leo nimefika mwisho wake na kufanikiwa.

Pili, nawashukuru wachangiaji wote hapa JF walionipa support (kwa njia ya ushauri) kuhusu jinsi gani naweza kufanikisha adhma yangu, Mungu awabariki sana (kwenu nyote mnaoamini uwepo wake na utendaji kazi wake).

Binafsi nina furaha ya pekee sana, nimefanya interview na visa yangu ime be approved, kesho saa nane kamili mchana nitakwenda kuchukua tayari kwa kuanza maandalizi ya safari hivi karibuni.

Mwisho kabisa, nawashukuruni nyote mlioniombea, mlionikejeri na kunikatisha tamaa, mmenipa nguvu kwa namna moja ama nyingine.

Nimelizie kwa kuwakaribisha nyote mlio na mlengo kama wangu, kwa ushauri namna gani mnaweza fanikiwa pia.

Wabillah tawfiq.
Hongera sana, kila la Heri.
 
Mrejesho wa nini hapa! Unadhani kwenda Marekani ni mbinguni! Huko unajipeleka utumwani tu! Nchi yako hii ni bora mara 1000 kuliko huko unakoomba na kusali! Utajua hilo utakapofika huko kama utafanikiwa interview yako! Utakuja kurudi huku mikono mitupu kama utakavyokwenda!
Niko Marekani miaka kadhaa..sijaona niko katika utumwa wowote ule!
 
Back
Top Bottom