Leo katika sala:Watanzania tuombee amani!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Hii ni sala maalum ya kuombea Taifa amani, na imeombwa makanisa yote leo.

Tuombe:
Mwenyezi Mungu, Baba wa milele, ulijalie Kanisa lako ulimwenguni mwote umoja na amani.
Uliimarishe linapoteswa kwa ajili ya Jina lako;na kulijalia kuwatangazia mataifa yote Injili yalo kwakusihi.

Twaitikia:
E e Bwana , Usikie kuomba kwetu.

Tuombe:
Ulimwenguni pote , uwabariki watawalao, tukae na amani, hasa tunamwombea Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete, mawaziri na wote wenye mamlaka katika nchi hii ili watawale katika haki na kweli, twakusihi.

Twaitikia :
Ee Bwana , Usikie kuomba kwetu.

Ref: Liturgia pg 349-350.

Na momi naomba wana JF michango yenu yote iwe ya kujenga amani upendo na utulivu.

AMEN
 
tatizo wengine wakijataid kujenga kule wanabomoa.. wakristo wanaitwa waoga, lakini kwa kuwa Yesu kristo ni MUNGU. ..na yeye ndo anaewapigania, na c kinyume chake. njia pekee ni sala.. napenda kusisitiza hata upande wa pil nao watafute amani...maana inapatikana..
 
tatizo wengine wakijataid kujenga kule wanabomoa.. wakristo wanaitwa waoga, lakini kwa kuwa Yesu kristo ni MUNGU. ..na yeye ndo anaewapigania, na c kinyume chake. njia pekee ni sala.. napenda kusisitiza hata upande wa pil nao watafute amani...maana inapatikana..
Ubarikiwe mkuu Mrisho.
Amani ni kila kitu, amani injenga mazingira mazuri ya kisiasa, kuabudu, biashara,maendeleo na kujiendeleza, na hata michezo.

Wakuu wa nchi tunawaombea ili wadumishe yote haya.
 
Nafarijika kusikia kuwa ni makanisa mengi waliooma sala kuombea amani.

Mch Lwakatare ameonekana ITV. Akihamasisha amani.
 
Hii ni sala maalum ya kuombea Taifa amani, na imeombwa makanisa yote leo.

Tuombe:
Mwenyezi Mungu, Baba wa milele, ulijalie Kanisa lako ulimwenguni mwote umoja na amani.
Uliimarishe linapoteswa kwa ajili ya Jina lako;na kulijalia kuwatangazia mataifa yote Injili yalo kwakusihi.

Twaitikia:
E e Bwana , Usikie kuomba kwetu.

Tuombe:
Ulimwenguni pote , uwabariki watawalao, tukae na amani, hasa tunamwombea Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete, mawaziri na wote wenye mamlaka katika nchi hii ili watawale katika haki na kweli, twakusihi.

Twaitikia :
Ee Bwana , Usikie kuomba kwetu.

Ref: Liturgia pg 349-350.

Na momi naomba wana JF michango yenu yote iwe ya kujenga amani upendo na utulivu.

AMEN
CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP
P.O. Box 55024 Dar Es Salaam Tanzania, E-mail:info@cmftz.org, website: www.cmftz.org
Tel: 0715200551, 0755200550 : Tarehe 28/10/2012
MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI NCHINI
Neno la Mungu limetuagiza katika 1Timotheo 2:1-2; kuwa, kabla ya mambo yote nataka DUA, SALA, MAOMBEZI NA SHUKURANI vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa. Ndugu zangu Watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika Katiba yetu ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba Ya 1977 Ibara 13(5). Kwa upande wa madhehebu ya Dini Tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo; Dini kubwa ni Ukristo, Uislamu na Dini za Kijadi. Wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika Nyumba moja na kufanya shughuli za Kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya miaka hamsini (50) ya uhuru Nchi yetu. Ndugu zangu wakristo na watanzania wezangu kwa ujumla napenda kuwafahamisha kuwa, hakuna nchi yeyote katika bara la Afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislam wanao ishi kwa amani na upendo kama Tanzania.Ila kwa sasa watu wasioitakia amani Nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali vurugu. Hivi karibuni, tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na Dini nyingine. Hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari; Mathalani: Redio, Magazeti na Machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa Jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika Jamii iliyokuwa imeshikamana. Aidha, mgawanyiko huu unazidi kukua na kusababisha hali ya Chuki kwa mamlaka ya Nchi, na hatimaye Dini moja na nyingine. Baada yakufanya utafiti wa kina kwanini kuwe na Chuki baina ya makundi ya Dini na Serikali tumeona kuwa, makundi haya ya Dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea Dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala. Hata hivyo, Madai ya kundi hili yanawapelekea kuwafanyia Vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na Serikali, jambo ambalo linawafanya (wanaofanyiwa vurugu) wasitumie uhuru wao wakufanya ibada ambao kimsingi wamepewa Mungu na kuandikwa katika Katiba ya Nchi Yetu. Tukiwa Kanisa la Mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za Nchi zinalindwa na kutekelezwa. Kimsingi, haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi. Hivyo, Kanisa baada ya Kumlilia Mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji usio wa maneno tu; kwani suala la kutoa matamko ya kulaani limefanywa na Dini na Serikali kwa mkazo mkubwa. Kwa upande wa Serikali, watawala wa Nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa Dini, rushwa na ufisadi katika Taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu hii ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, Kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa Shetani; hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuziopinga hila za Shetani kwa DUA, SALA NA MAOMBI ili kuleta amani ya kudumu katika Taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani Afrika na Duniani. Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini; ikumbukwe na izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu Mungu, hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na Mungu na sio siasa, na pasiwe mahali pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu. Viongozi wa dini wanaaminiwa sana na waumini wao na lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa Mungu. Aidha tukumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo. Amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika Nchi; iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa Nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kawahiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda; kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu; hii ni tunu tuliyopewa na Mungu na kuachiwa na waasisi wa Nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema Hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani. Nichukue fursa hii kumpongeza Kamanda Suleiman Kova kwa juhudi zake za kuifanya Dar-es-salaam iendelee kuwa bandari ya Amani; Kamanda Kova ameonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini na kwa watanzania wote. Kanisa la Mungu ambao tumeitwa kwa Jina la BWANA, leo hii tunaomba na kuutafuta Uso wa BWANA tukiwakilisha zaidi ya makabila 120 ya Tanzania kwa Kutumia Lugha Zetu za Makabila kama alama ya Umoja na mshikamano wetu, tukimsihi Mungu aiponye Nchi yetu. Tunaitakia Nchi yetu amani na Utulivu, katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Amini.
NDIMI NDUGU YENU KATIKA KRISTO YESU
……………………………………………….
ASKOFU MKUU DKT. MGUL
 
Back
Top Bottom