SoC04 Leo, 1967 na Kesho

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ghettominds

New Member
May 2, 2024
4
0
Ninaandika story hii nikiwa ghetto, hivyo hii ni story ya Ghettominds. Hivi karibu kumekuwa na ongezeko la lawama kwa serikali na vijana wa nchi hii. Imekuwa ni kama mpira wa mchezo wa tennis kwani hakuna anaetaka kukaa na kitenesi hivyo basi kuishia kutupiana tuu kitenesi. Kitenesi nacho kizungumzia hapa ni suala zima la ukosefu wa ajira kwa vijana (walio na elimu na wasio na elimu). Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana kukosa ajira na kuishia kulalamika serikali kwa kutoandaa misingi bora ambayo ingewapatia vijana hawa ajira pale tuu wanatoka vyuoni, papohapo serikali nayo inawatupia lawama hizohizo kwa vijana kwani kupitia elimu waliyo nayo wanaweza kujiajiri wenyewe. Je nani wakubaki na kitensi hichi?.

Kuingia mwaka wa 2024 nilisoma na kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto kukataa kujiunga na kidato cha kwanza wakiwa na madai ya kuwa, licha ya kwenda shuleni na kukamilisha elimu yao wataishia kuwa kama dada na kaka zao waliosoma hadi chuo kikuu lakini wapo mtaani bila ajira, ndipo wapo waliodai wanataka kwenda vyuo vya ufundi kujifunza sanaa ya ufundi na kuachana kwenda kusoma kwa nadharia tuu ili waweze kupata kipato na kusaidia wazazi wao.

KWANINI VIJANA HAWAPATI KAZI WANAPOMALIZA CHUO

Nimesoma sababu nyingi tuu zilizotolewa na watu mbalimbali kuhusu sababu ya vijana kukosa ajira pale wanapo maliza elimu yao chuo kikuu. Kila mtu hufikia hitimisho na kuja na hoja mbalimbali lakini kwangu hoja kuu ni moja tuu UKOSEFU WA UJUZI KAZI.

Kila zinapotoka nafasi za ajira kigezo kikubwa huwa ni uzoefu kazini wa zaidi ya miaka 2 au 3, je kijana huyu uzoefu huo anautolea wapi na alikuwa shuleni kwa zaidi ya miaka 16 akisoma nadharia tuu?

NINI KIFANYIKE

Hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimuambia babu yangu kuhusu “Elimu ya kujitegemea”. Hii ni elimu ambayo itamsaidia kijana wa kitanzania amalizapo elimu yake basi aweze kuitumikia jamii na kulipa deni kwani alisomeshwa bure na serikali. Hivyo kijana huyu alipaswa kusoma kwa nadharia na vitendo ilimradi kumuwezesha kupata kibarua au kujiajiri pale amalizapo tuu elimu yake.

TANZANIA NIITAKAYO

Nitakachoongelea hapa ni suala lilizozungumziwa miaka 57 iliyopita ambapo Tanzania ilikuwa nyuma kiuchumi, Sayansi na kiteknolojia. Leo tunaiona Tanzania kuwa kwenye nchi zenyewe zinakuwa kiuchumi kwa kasi pia sayansi na teknolojia. Maneno SKILLED LABOR FORCE, THE FUTURE OF TANZANIA ni maneno yanayosomeka kwenye nembo ya VETA. Hivyo basi kunao umuhimu wa serikali yetu kuliangalia hili kama navyoliangalia mimi.

VETA ni chuo cha ufundi kinachomiliki vituo kwenye kila kanda ya Tanzania na kutoa kozi zaid ya 13 za elimu ya ujuzi tena kwa vitendo na nadharia. Kama zinavyofanya shule za makanisa basi VETA ningependa wafuate mfumo huo.
  • VETA waanzishe kutoa elimu ya shule ya msingi kwa watoto wadogo kuanzia miaka 7 kama alivyopendekeza Mwl. Nyerere kwenye azimio la Arusha kwani watoto hawa wataandikishwa kama wanafunzi wengine wanaoanza la kwanza. Shule hizi zitaendeshwa kama zile za binafsi kwani wazazi au walezi itabidi wachangie kidogo gharama za huduma sio kuwaachia serikali gharama zote.​
  • Masomo 4. Wawapo shuleni watoto hawa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba watatakiwa kusoma masomo ya Kiswahili, Hisabati, Kiingereza na Sayansi ya sanaa yake. Hii itasaidia kwenye kupata vijana wenye ujuzi tosha kwani watakuwa wamepatiwa ujuzi tokea wakiwa wadogo hivyo kuja kufanya kazi waliojifunza ungali wadogo.​
  • Ngazi ya pili, kama zilivyo shule nyingi za mataasisi huanzisha shule ya msingi na baadae kuwa na sekondari, basi ndivyo hivyo VETA wafanye kwani nao waanzishe shule zao za sekondari kuanzia form 1 hadi form 4, ambapo form 1 hadi form 2 wanafunzi hawa tatakiwa kusoma ujuzi wa sanaa yao kwa vitendo zaidi kwani kwa nadharia walisoma shule ya msingi. Kwa miaka hiyo miwili mengine vijana hawa waitumie kama wapo Field. Mfamo aliyosomea seremala apelekwe wanapotengeneza vitu hivyo kadhalika na mafundi magari kwenda garage.​
FAIDA YAKE
  • Tutapunguza mgomo wa wanafunzi kwenda kuanza shule kwa nadharia ya kukosa ajira kama dada na kaka zao kwani watakuwa na ujuzi wa kazi kama inavyotakiwa kwenye soko la ajira.​
  • Tutapunguza tatizo la vifaa vya miundombinu ya elimu kwani miongini vijana hawa watakuwepo mafundi fanicha, mafundi ujenzi n.k watako tumika kutengeneza vitu hivyo nakupunguza gharama kwa serikali kuwalipa watu binafsi kutengeneza vitu hivyo. Hivyo itasaidia kupunguza ukosefu wa viti na madawati mashuleni kwani tutakuwa na watalumu wengi wa kutengeneza vitu hivyo.​
  • Itampa chaguo mtoto pale amalizapo elimu yake ya sekondari kwenda kuongeza taaluma chuo kikuu amaa kuingia kwenye ajira maana atakuwa na elimu inayomtosheleza kuingia kwenye ajira moja kwa moja.​
  • Itapelekea kupunguza tatizo la ajira kwani kila mtoto atakuwa na uwezo wa kujiajiri maana amefundishwa taaluma fulani kwa vitendo na sio nadharia tu.​
  • Tutatengeneza vijana wadogo wengi wenye kuweza kulisaidia Taifa lao kwa ujuzi walio nao kwa muda mfupi tuu kutoka miaka 16 ya elimu hadi 11 na kijana huyu wa kitanzania akaanza kulisaidia taifa akiwa na umri mdogo tuu. Mfano mzuri ni mataifa ya yalioemdelea kama USA Uingereza n.k​
  • Tukuwa tumefanya kile kilichoandikwa kwenye nembo ya VETA SKILLED LABOR FORCE, THE FUTURE OF TANZANIA.
USHAURI

Kila kanda kama ilivyo kwenye vyuo vya ufundi VETA wakae waje na mpango wa shule za msingi kwani mtoto ndie kiumbe kinachoweza kunasa kila anachoambiwa na kufundishwa pia vilevile mtoto anao uwezo wa kujifunza kwa kuona na kwa kuigiza. Kwa kuzingatia hayo naona itakuwa ni wepesi kuanza na watoto kuwa fundisha fani tofauti angali wakiwa wadogo na wakaanza kuzitendea kazi angali nao wakiwa wadogo na kuja kupunguza wigo wa vijana kukosa ajira na mbadala wake ndio ujikuta kukimbilia kwenye vyuo vya ufundi. TUANZE KUWAANDAA MAFUNDI HAWA ANGALI WATOTO.

Pia VETA isiwe tena inategemea wanafunzi kutoka mashule tofauti tofauti bali wao wawe wanazalisha wanafunzi wao kuanzia ngazi ya msingi hadi ile ya sekondari na vyuo kubaki kwa wale wanaotoka kwenye mashule mengine. Hili likifanyika litaleta chachu kwa wanafunzi, wazazi na welezi ambao hawaoni umuhimu wa kupeleka watoto wao shule kwa hoja kutokuwa na ajira pale wanapomaliza elimu zao na tutajikuta tunawashawishi wazazi hawa kuwapeleka katika shule hizi za ufundi nakujifunza angali wadogo kwa maslai ya baadae.


 
Nitakachoongelea hapa ni suala lilizozungumziwa miaka 57 iliyopita ambapo Tanzania ilikuwa nyuma kiuchumi, Sayansi na kiteknolojia. Leo tunaiona Tanzania kuwa kwenye nchi zenyewe zinakuwa kiuchumi kwa kasi pia sayansi na teknolojia. Maneno SKILLED LABOR FORCE, THE FUTURE OF TANZANIA ni maneno yanayosomeka kwenye nembo ya VETA. Hivyo basi kunao umuhimu wa serikali yetu kuliangalia hili kama navyoliangalia mimi.
Skilled labor force, the future of Tanzania

And the now asee, tunahitaji hii kitu

itabidi wachangie kidogo gharama za huduma sio kuwaachia serikali gharama zote.
Nzuri sana hii


Na mpango wako wa kuzibrand shule zitoe watu skilled moja kwa moja upo njema bro sana.
 
Back
Top Bottom