Lema na Nassari sasa toeni ushahidi uliobaki ikiwemo "print out" ya mazungumzo ya simu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,134
144,633
Mpaka sasa DC Mnyeti na madiwani wawili wamekanusha tuhuma mlizozielekeza kwao huku madiwani wawili wakiwatuhumu nyinyi kwa kutengeneza hizo video huku diwani mmoja akiziita hizo clip kuwa ni za kitoto.

Hivyo ili kukata mzizi wa fitina, nawashauri ikiwezekana hata kesho mtoe video ambazo awali hamkuzitoa pamoja na hiyo print out ya mazungumzo maana kejeli zimenza na zikisemwa sana bila nyinyi kuonyesha ushahidi wa ziada zitageuka kweli kwa baadhi ya watu hasa wale ambao sio wafuatiliaji wa mambo hivyo ni rahisi kudanganywa na hizi propaganda za baadhi ya wana-CCM.

Hatari ninayoina ni wanapropaganda hawa kuwageuzia nyinyi kibao kwa kujifanya wana mapenzi na CHADEMA na kuanza kuwazushia maneno kuwa mnakiweka chama pabaya licha ya wao mpaka sasa kushindwa kujibu tuhuma hizi pasipo kuacha shaka yoyote.

Kwa sasa hamna haja tena ya kumsitiri yoyote yule hata awe nani maana hii sasa ni sawa vita ambayo siku zote haina macho
 
Naona wanatoa ushahidi kidogo kidogo kimkakati,hii naifananisha na kumkimbiza mwizi kimya kimya bila kupiga yowe,na mwizi mwenyewe akigeuka nyuma anaona uko hatua moja kutoka alipo,

Vijana wanahakikisha pressure ya kuwawajibisha hawa watoa rushwa haishuki,hapa ni anguko la serikali hii iliyojaa watoa rushwa

Nadhani tukio hili ni mfanano wa tukio la lipumba,nadhani lipumba naye yuko kwenye payroll ya mtu fulani ili kuivuruga CUF,tukio la Arusha na la Lipumba kuisumbua CUF yanafanana sana
 
Mpaka sasa DC Mnyeti na madiwani wawili wamekanusha tuhuma mlizozielekeza kwao huku madiwani wawili wakiwatuhumu nyinyi kwa kutengeneza hizo video huku diwani mmoja akiziita hizo clip kuwa ni za kitoto.

Hivyo ili kukata mzizi wa fitina, nawashauri ikiwezekana hata kesho mtoe video ambazo awali hamkuzitoa pamoja na hiyo print out ya mazungumzo maana kejeli zimenza na zikisemwa sana bila nyinyi kuonyesha ushahidi wa ziada zitageuka kweli kwa baadhi ya watu hasa wale ambao sio wafuatiliaji wa mambo hivyo ni rahisi kudanganywa na hizi propaganda za baadhi ya wana-CCM.

Hatari ninayoina ni wanapropaganda hawa kuwageuzia nyinyi kibao kwa kujifanya wana mapenzi na CHADEMA na kuanza kuwazushia maneno kuwa mnakiweka chama pabaya licha ya wao mpaka sasa kushindwa kujibu tuhuma hizi pasipo kuacha shaka yoyote.

Kwa sasa hamna haja tena ya kumsitiri yoyote yule hata awe nani maana hii sasa ni sawa vita ambayo siku zote haina macho

Hao jama hawawezi kukwepa hii kashfa, Tanzania haikai watu wasio na akili.... hakuna haja ya kupoteza mda, wakikana ni sawa tu, maisha yanasonga, tunaelewa matatizo yao.
 
Kwa wenye akili tushasoma kuwa mchezo ulishaisha kitambo. Hakuna jipya litakalotokea hapo.

Ila tusubiri.
 
Back
Top Bottom