Lema aumbuka! Namba ya simu aliyodai ya Mulongo ilikuwa ni Uzushi

[h=3]GODBLESS LEMA AUMBUKA....VODACOM WADAI KWAMBA ULE UJUMBE WA VITISHO HAUKUTOKA KWA MKUU WA MKOA[/h]


KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amedai kuwa uchunguzi wa awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, umetumwa na mtandao wa simu wa nje ya nchi.

Kamanda alisema katika ujumbe huo ambao Lema anadai uliandikwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kutumwa kwenye simu yake Aprili mwaka huu, uchunguzi wa polisi umeonyesha kwamba haukutumwa kupitia kampuni moja wapo ya simu za mikononi ya hapa nchini.

“Katika kipindi cha mwishoni mwa Aprili mwaka huu, vyombo vingi vya habari vikiwemo radio, magazeti na mitandao ya kijamii viliandika na kutangaza habari iliyoelezea shutuma zilizotolewa na Mbunge Lema kuwa aliandikiwa ujumbe wa vitisho kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa Mulongo na ulisomeka:

“Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi inayoitaka mimi.”

Kamanda Sabas alisema ujumbe huo ulidaiwa kutumwa kutoka namba 0752960276 inayotumiwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo kwenda kwenye namba 0764150747 inayotumiwa na Lema. Alisema kufuatia tuhuma hizo, polisi walianza uchunguzi kwa kuzingatia kuwa Mulongo alikanusha kutuma ujumbe wa aina yo yote kwa Mh Lema.

Alisema uchunguzi huo ulihusisha kampuni ya simu ambayo mtandao wake ulitumika katika utumaji wa ujumbe husika. Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa chanzo cha ujumbe huo mfupi hakikuwa kampuni ya simu husika (hakuitaja) kwa vile ‘Centre Number’ iliyotumika kutuma ujumbe huo mfupi wa maneno ni 44780200332, ambayo siyo ya mtandao wa kampuni husika bali ni ya mtandao ulio nje ya nchi.

Alisema uchunguzi zaidi unaendelea kubaini chanzo cha ujumbe huo mfupi wa simu na mtu aliyehusika kutuma hatua za kisheria zitaweza kuchukua mkondo wake.
barua1.jpg
 
Bado hawajajibu swali,kama siyo Mkuu wa mkoa je ni nani?

Kwani mkuu wa mkoa hawezi kutumia namba nyingine kutuma ujumbe kwa Lema na kufikisha ujumbe alioukusudia?
 
Wakuu JF Great Thinkers Amani iwe nanyi.

Mods,
Litakuwa jambo la Mbolea sana kama hamtaiunganisha hii thread na Nyingine.
Sababu ni kuwa, Thread hii imejikita zaid kwenye Kutoa Elimu ya nini Maaana ya Free SMS Kwenye World wide web (www).
Hii inahusika kwa Namna Moja na tukio la Mbunge Lema Kutumiwa SMS na Number ambayo Mmiliki wake ni RPC Mulongo


Uwezekano Mkubwa sana kuwa RPC wa Arusha Kulishwa Maneno ya Kitu asichokielewa kuhusiana na SMS aliyotumiwa Lema kutoka kwenye Number ya Mulongo

What is SMS Centre Number???
Hii ni Number inayoonesha SMS imetokea wapi.
Hapa Ndipo RPC Huenda watu wametumia advantage ya uelewa wake wa hili suala Kumuingiza Mkenge.

Wengi wamekurupuka sana na Kuanzisha Thread eti Mh Lema aumbuka.

Mfano Mzuri wa Free SMS Services.

Hebu Kama una Google account (email ya Google), iwe gmail.com ama GOOGLEmail.com
Ukiiingia, kuna Option ya Google SMS Ambayo Requirements zake ni Lazima uingize Number yako ya Simu.
From There, you can send Free SMS From Google Account na SMS Centre Number haitakuwa ya Mtandao wako.
i.e Haitwaku +2557xxxx, Centre Number itakuwa ni Free Centre Number ya Originating Google Server.
Hii sio kwa Google tu, zipo Free SMS Services Mtandaoni Nyingi tu, we Type Free SMS in Google uone Options zaid ya 800 za Free SMS Services.
Hata JF , Mods Mkitaka, mnaweza Ku Introduce hiyo Option

Maswali Magumu Ma CCM yasiyopenda Kushirikisha Vichwa.
Ama kwa Lugha Nyingine, Yasiyojua Hii Technolojia ila yako Mbele Kishabiki shabiki na at the end of the day (Mahakamani) Always yanaangukia Pua.

Lema ali register kwenye Hiyo Mitandao Number Ya Mulongo???
Usije ukakurupuka ukasema Ndio coz, once unapoingiza Number, unatumiwa Verfication code thru SMS Kwenye Hiyo number uliyoingiza.
Hii ni Njia Moja wapo ya Ku Verify kuwa aliyeingiza Hiyo Number ndo Mmiliki Halali wa Hiyo Number.

Je Lema alikuwa na Simu ya Mulongo????


My Take

Polisi ajirini Vijana wa Ki Tanzania wasomi, wenye uelewa Mpana wa Masuala ya ICT, Otherwise mtaendela kila siku Kuingizwa Kingi


======================
Correction, kwenye Heading, isomeke kama RC Mulongo
======================
 
wadau, kutokana na kuthibitika kuwa godbless lema amelidanganya taifa, ni hatua gani anastahili kuchukuliwa mtu huyu?

Kwani Voda wamesema Mulugo hakutuma ujumbe? wamesema sms haikutoka vodacom, sasa anayetakiwa kujibu ilitoka wapi siyo aliyetumiwa ni aliyetuma, usiwe mburula!
 
polisi umebaini kua chanzo cha ujumbe huo mfupi haikua kampuni ya simu husika kwa vile Central no. iliyo tumika kutuma ujumbe huo mfupi wa maneno ni 44780200332


sasa ni kampuni na sio Magesa MULONGO??

HATUDANGANYIKI.
 
wadau, kutokana na kuthibitika kuwa godbless lema amelidanganya taifa, ni hatua gani anastahili kuchukuliwa mtu huyu?

kadanganya vipi? wenzio wanaocheza hapa ni kuondoa ukweli kuwa ujumbe umetumwa na mulongo, lakini ujumbe upo. kwa hiyo kuna mtu kamsaidia mulongo kumtishia lema? ina maana hata kampuni za simu nazo zinacheza mchezo mchafu? hata akisafishwa kiasi gani, na kwa taarifa yake mulongo, lema akipatwa na lolote tunajua ni yeye, kwa sababu katangaza kabisa na mengine kangea wazi.
kwani ccm mtu wao akikosea lazima akingwe? watakuwa na kazi ya kupangua uovu mpaka lini? wajitahidi basi kuongea kwa hekima japokuwa hekima haiwezi kuwepo penye roho mbaya. ''kimtokacho mtu ndicho kiujazacho moyo wake''
 
Bisek 09:50 Today
Jaman wana jamii nimeona barua
ya jana tar 21 May 2013 ya RPC
arusha akimkingia kifua bosi wake
RC (mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa), nikiwa
mtanzania mwenye akili timamu
nimejiuliza maswali yafuatayo;
1.Kama center namba iliyotuma
ujumbe huo ni ya nje,kwanini
namba ya simu haina country
code?mfano +254, au +256 au +44?
2.Kwanini ni ujumbe huo tuu ndio
una center number ya nje ujumbe
mwingine wote wa mulongo una
center namba halali kutoka voda
voda?
3.Kwanini jeshi la polisi liliitafuta
kwa udi na uvumba simu ya Lema?
walikuwa wanataka kufanya nini
kma kumbukumbu zote ziko peupe
pale vodacom?
4. Tutajuaje kma dikteta Mulongo
na idara kandamizi ya CCM yaani
polisi hawajaedit hiyo center
namba ionekane ni ya nje?5.Ni
kwanini taarifa hii itolewe miezi
miwili baada ya tukio kutokea?
kwanini isingetolewa immediately?
kuprint hizo calls inahitaji muda
gani?
6.Kwanini hatujaonyeshwa kwa
namna yoyote kuwa haki
inatendeka kwa mtuhumiwa
Mulongo kuhojiwa na polisi?
insteady polisi ndio wanahaha
kumtetea?
Wakati CCM na polisi wao wanaishi
jana,wanasahau watanzania sasa
wanaishi leo, uonevu na dhuruma
dhidi ya haki ipo siku itakoma......
 
Bisek 09:50 Today
Jaman wana jamii nimeona barua
ya jana tar 21 May 2013 ya RPC
arusha akimkingia kifua bosi wake
RC (mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa), nikiwa
mtanzania mwenye akili timamu
nimejiuliza maswali yafuatayo;
1.Kama center namba iliyotuma
ujumbe huo ni ya nje,kwanini
namba ya simu haina country
code?mfano +254, au +256 au +44?
2.Kwanini ni ujumbe huo tuu ndio
una center number ya nje ujumbe
mwingine wote wa mulongo una
center namba halali kutoka voda
voda?
3.Kwanini jeshi la polisi liliitafuta
kwa udi na uvumba simu ya Lema?
walikuwa wanataka kufanya nini
kma kumbukumbu zote ziko peupe
pale vodacom?
4. Tutajuaje kma dikteta Mulongo
na idara kandamizi ya CCM yaani
polisi hawajaedit hiyo center
namba ionekane ni ya nje?5.Ni
kwanini taarifa hii itolewe miezi
miwili baada ya tukio kutokea?
kwanini isingetolewa immediately?
kuprint hizo calls inahitaji muda
gani?
6.Kwanini hatujaonyeshwa kwa
namna yoyote kuwa haki
inatendeka kwa mtuhumiwa
Mulongo kuhojiwa na polisi?
insteady polisi ndio wanahaha
kumtetea?
Wakati CCM na polisi wao wanaishi
jana,wanasahau watanzania sasa
wanaishi leo, uonevu na dhuruma
dhidi ya haki ipo siku itakoma......
kila hila unayofanywa na ccm na serikali yake dhidi ya chadema ni lazima ile kwao na kuongeza umaarufu wa chadema. hila za ccm ni pembe la ng`ombe, hazifichiki tena
 
ITS ONLY A FOOL WHO WILL BELIVE THIS. Kwa nini Police CCM walipofika kwa Lema kitu cha kwanza kuulizia ni simu? na hata baadae kumtaka mke wake awapatie hiyo simu?? nia yao ilikua kuharibu ushaidi lakini walipokosa hiyo simu wamekuja na single hiyo ya kijinga kabisa.
Hata nyie Police ni wajinga sana kukubali kutumiwa kujinga hinyo.
SHAME ON YOU POLICE CCM AND MULONGO.
 
Wanafikiri watu wana akili ndogo za kufikiri kama enzi za zama zao za ujinga. Watanzania sio wakudanganyika tena inabidi wakubaliane na hali halisi kuwa ulimwengu umebadilika na watanzania wamebadilika, na matendo yao wanayowafanyia wananchi ndo yana wafanya wananchi wazidi kuamka zaidi.
 
Hatukuhitaji kujua center namba ya sms, tulichotaka kujua ni nani alietuma sms???????matope hayabebeki......
 
Wanafikiri watu wana akili ndogo za kufikiri kama enzi za zama zao za ujinga. Watanzania sio wakudanganyika tena inabidi wakubaliane na hali halisi kuwa ulimwengu umebadilika na watanzania wamebadilika, na matendo yao wanayowafanyia wananchi ndo yana wafanya wananchi wazidi kuamka zaidi.

CCM hawaoni hayo mkuu, they got different meaning.
 
Duu taifa la wadanganyika kweli.

Polisi wamefanya uchunguzi na kutupatia namba zao. Je Namba alizopokea Lema ujumbe ni za Mulongo?? kwenye simu ya Lema??

Pili Je ni mnara gani ulitumika kurusha hiyo sms ili tujue chanzo cha sms??

tatu je polisi walifanyia uchunguzi simu zote mbili yaaani ile ya mulongo na lema ili kujua kila simu iliyotuma na kupokea kweli ilipokea na kutuma sms tajwa. Hata kama simu umeitupa waniletee nitawambiwa kama sms ilitumwa wapi.

Tatu lazima sms iwe na original sasa hizo namba za kikatuni ni za kampuni gani??

Polisi hawa wamatamko wanasikitisha sana, ndio maana leo tunaaminisha njama za kulipuwa kanisa ni za bodaboda na tutaamini na kuishi nayo.

jeshi liloshindwa kuwa polisi.
 
Namba ambayo alitolewa na mheshimiwa Lema kuwa ni ya Mh. Sospeter Mulongo imeonyesha si kweli. Habari hii inaeleza zaidi.

uchunguzi wa awali wa kifo cha Mwangosi ulisema kwama alilipuliwa na kitu kilichotupwa na wafuasi wa chadema,Picha zikawaumbua. hila zozote dhidi ya chadema lazima ziwaumbue na kuongeza sifa kwa chadema. mtaangaika sana
 
Kwa hiyo zile za kina IGHONDU zilizowekwa na MWANAHALISI zilikuwa za kweli kuhusu TISS kumteka Dr. Ulimboka, manake hamkupinga au technologia hii hamkuwa nayo! Shame!
 
mulongo hatoki katika sakata hilo, hapo lema hana kosa! Watu wana haha kumuokoa mulongo! Nina wasiwasi na vodacom!
mimi sioni kosa la lema kuumbuka,maana alichosema lema katumiwa ujumbe kutoka namba fulani ilipoangaliwa kwa makini ikaonekana ni ya Mulongo sasa kosa lake liku wapi? au ilitakiwa akae kimywa bila kutoa taarifa, Je/ polisi wamemuhoji Mulongo?
 
Kama kina nchi ina watu kwenye shida na upeo mdogo TZ ina ongoza.polisi wame toa feedback ya uchunguzi wao mna question wasipotoa mna question hvi nyie ni watu gani?
wanatukumbusha walipotueleza kwamba Mwangosi alilipuliwa na kitu kilichotupwa na wanachama wa chadema
 
Kimsingi alichosema Mh.G Lema na kuudhirishia ulimwengu wote Ujumbe alioupokea ulionyesha unatoka kwa namba za simu ya mkononi ya Ndg Mulongo Mugesa,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Kuna ukweli kwamba CCM iliingiza mitambo itakayowawezesha kuziandaa na kuzituma sms kwa kusudi la kuwachafua baadhi Viongozi wa Upinzani kwa Lengo la kuidhoofisha CHADEMA,Tuliyaona hayo 2010 wakati wa UCHAGUZI Mtambo ulitumika kumchafua Dr W.Slaa Rais wa JMT aliyepokonywa kiti cha URAIS.
 
mim nafikili hamja muelewa LEMA mzee wa kulopoka ameumbuka kwa kumsingizia mkuu wa mkoa mbona ipo clear sasa mnasemaje au mnajifanya hamjui kama kaumbuka

Namba ni ya Mkuu wa Mkoa,ila center no ndio tatizo. Mbona kitu rahisi sana,RC kabadilisha center no. akatuma msg. Hapa Lema kaumbuka wapi?! Center no. inabadilishwa kirahisi tu.
 
Back
Top Bottom