ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Kwa wale tunaofuata imani ya kristo , tunasoma na kuamini kuwa:
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe (Ayubu 14:1-2,14).
Mistari hii inatukumbusha kila machweo na pambazuko kuwa pamoja na taabu na mashaka mengi, au raha nk hapa duniani, ijapo siku tutakufa, tutakufa kwa kupenda au tusipopenda. Kifo kimeandikwa , iwe ni wa imani ya dini au mpagani (mtu asieamini katika dini yeyote ile).
Pamoja na kujua kuwa kifo kipo na kinatokea siku tusioijua, kuna badhii ya watu katika jamiii wanaimani pia katika mila za kuwa ukifa ni sharti ukazikwe katika udongo wa eneo la asili ya kizazi chako ( wanaita "nyummbani").
Kwa kuweka msisitizo wa kauli zao, baadhi yao wanadiriki hata kuacha wosia kwa ndugu na familia kuwa " tafadhali sana mimi nikifa, ni lazima nikazikwe nyumbani"
Pengine unakuta mtu huyu amekuwa akiishi mbali sana na huko "nyumbani "katika maisha yake yote na kabla ya umauti haujamfika alikuwa na mali na kipato kizuri sana cha kumwezesha kujenga mazingira ya yeye siku akifa "akazikwe nyumbani" lakini hakutunza hata sehemu moja ya mali zake za kuwezesha safari hiyo ya nyumbani.
Inapofika siku ya kifo cha mtu wa jinsi hii, na kwa kuzingatia baadhi ya imani za kimila na desturi za baadhi ya makabila yetu (...), inakuwa ni "lazima kutekeleza kauli ya marehemu" kwani marehemu huwa inaaminika ana nguvu kuu hata za kusambaratisha milima iwapo kauli alizohusia hazitatekelezwa (ni imani!!).,
Ikiwa familia ni maskini, na haiwezi kabisa hata kukamuana kuweza kusafirisha msiba kwenda huko "nyumbani", hali inakuwa ngumu zaidi na kama itawezekana, basi pengine inaishia kwa kuiweka katika umaskini mkubwa mno labda hata kwa kuuza mali zote ambazo zingeweza kuisaidia familia iliyoachwa na marehemu ili kutimiza "agano" na marehemu...la kumfikisha huko "nyumbani".
Ikiwa tunaamini kifo kipo na tunataka tukazikwe huko "nyumbani" ambapo pengine hata hatukuishi wala kujenga huko katika uhai wetu, kwa nini basi tusijiandae kwa hilo ili kuwatokuwaongezea umasikini na majonzi zaidi kwa wale ambao tunawaacha hapa duniani baada ya sisi kuondoka???.