LAWAMA KWA wana-CCM tu?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Nimefuatilia sana lawama zinazotolewa kwa viongozi mbali mbali wa nchi yetu Tanzania.

Kinachonipa wasi wasi ni kuona kuwa lawama hizo zinaelekezwa tu kwa wale viongozi ambao ni wana CCM.

Najiuliza haya:-
1. Ni kweli kwamba hakuna la maana wanalilifanya viongozi wana- ccm?
2. Je viongozi, Wabunge, nk. wa Itikadi nyingine za siasa hwana lawama?
Wako safi tu?
3. Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?

Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.
 
Kabla ya Kulaumu ni vizuri ukashauri,na ukitoa ushauri ikashindikana hapo ndipo unaweza kuanza kulaumu.
TUNATAKA KUJENGA TAIFA LETU NA WALA SIO KUHARIBU
 
Umenena jambo zuri Exaud.
Binafsi naona kuwa kama wangefanya inavyo paswa na kwa uzalendo wa dhati kabisa, hapana shaka kuwa Tz ingekuwa mbele sana kimaendeleo kuliko ilivyo hv sasa.
Maana yake ni kuwa nchi ambayo ina rasilimali nyingi kiasi hk halafu mwanachi wa kawaida hamudu hata milo miwili kwa ck it's a huge shame.
Nadhani kwa kuwa ccm kwa vile wameshika utamu ndo maana lawama ziko juu yao.
Hvyo ndo nionavyo mimi. Japo kwa kweli labda mazuri yapo ila kwa kweli yanafunikwa na uovu zaidi maana hayavumi kabisaaaa.
 
Kwahiyo wakulaumiwa ni wanachi siyo?

Huo mkahawa wako naona umenawiri sana, ila ukienda sehemu nyingi kunakolimwa hilo zao siku hizi limekufa, ila duniani kahawa bado inaendelea kunyweka kwa kasi kubwa kuliko juzi. Je, wakulaumiwa ni wakulima?
 
NONO,
Umeugundua mkahawa?
Wewe mchunguzi kweli kweli.

Sijui wa kulaumiwa ndugu m' bunifu.
 
Umenena jambo zuri Exaud.
Binafsi naona kuwa kama wangefanya inavyo paswa na kwa uzalendo wa dhati kabisa, hapana shaka kuwa Tz ingekuwa mbele sana kimaendeleo kuliko ilivyo hv sasa.
Maana yake ni kuwa nchi ambayo ina rasilimali nyingi kiasi hk halafu mwanachi wa kawaida hamudu hata milo miwili kwa ck it's a huge shame.
Nadhani kwa kuwa ccm kwa vile wameshika utamu ndo maana lawama ziko juu yao.
Hvyo ndo nionavyo mimi. Japo kwa kweli labda mazuri yapo ila kwa kweli yanafunikwa na uovu zaidi maana hayavumi kabisaaaa.

Big up Mkuu SABODE.
Leta hoja.
 
Mkuu wewe ni mwenyeji sana hapa JF na karibu ufikishe posts 1000.
Hivi ni kweli vyama vingine hapa havilaumiwi?
Ninavyojua hapa ni hoja kwa hoja. Wengi wanalaumu huku na kule lakini inaelekea sisi m wamebeba nyingi.
Nadhani ni haki yao na hii ni kwa kuwa kuna sababu nyingi na nyingine zimeanza kuainishwa hapa.
 
MChukia fisadi.
Hata mimi nachukia Fisadi kama wewe mkuu.
Hawa wana- CCM hawana jema jamani?
Leta hoja mkuu.
 
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Nimefuatilia sana lawama zinazotolewa kwa viongozi mbali mbali wa nchi yetu Tanzania.

Kinachonipa wasi wasi ni kuona kuwa lawama hizo zinaelekezwa tu kwa wale viongozi ambao ni wana CCM.

Najiuliza haya:-
1. Ni kweli kwamba hakuna la maana wanalilifanya viongozi wana- ccm?
2. Je viongozi, Wabunge, nk. wa Itikadi nyingine za siasa hwana lawama?
Wako safi tu?
3. Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?

Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.

Nini msingi wa maswali yako (nini kimekusukuma kuuliza)? maswali yako ni ya kijiweni mno, yamekosa pa kujishika. Nashindwa niandike vipi ili upate kunielewa.

Maybe ujiulize mwenyewe maswali yafuatayo:-

(1) Je viongozi wana CCM wanambiwa hakuna la maana wanalofanya.
Mimi nimeona na kusikia mengi mazuri hata hapa JF zipo thread hizo.

(2) Je viongozi wa vyama vingine vya siasa hawalaumiwi?
Mimi naona lawama nyingi tu kwa akina Lipumba, Mbowe, Zitto nk

(3) Je viongozi wa Taifa letu hawasifiwi kwa yale wanayotenda?
Mimi naona sifa nyingi tu zikitolewa kwenye media na forums mbalimbali

Suala la lawama kuwa nyingi kuliko sifa, ni rahisi kulijibu. Mosi ni kwasababu kero zimezidi. Kumbuka CCM ndo imeshika dola. Sasa wewe ulitaka wananchi wazipeleke wapi kero na lawama zao. Hakika nimeshindwa kukuelewa kabisa.

Unashauri mema yasemwe na mabaya pia. Kwani sasa ipoje? wewe unataka mema na mabaya tasemwe kwa kiwango sawa, Je, kwa kipimo kipi? Pole sana mkuu poor questioning. Otherwise u-substantiate wapi unakoongelea (kwenye media, JF au wapi?) kama ni general ...
 
kwani viongozi wa chama gani kingine wamewahi kuwa madarakani wakaboronga au wakafanya mema ili tuwapime? mpaka sasa nchi hii imewahi kutawaliwa na waheshimiwa wa ccm pekee na ndio tunaofahamu madudu waliyoyafanya na sina haja kuyaorodhesha hapa.
waswahili wanasema mwizi na hindi lake na hadi sasa mwizi tunayemwona na mahindi yetu yaliyoibiwa ni mwanaccm pekee. chadema, tlp au cuf alitawala lini hata tuone alivyokwiba au alivyofanya ubadhirifu?
lovulovu
 
The success or failure of a society is reflected by the current regime in power. therefore the ccm Leaders should shoulder all the blames for the mess up
 
Nini msingi wa maswali yako (nini kimekusukuma kuuliza)? maswali yako ni ya kijiweni mno, yamekosa pa kujishika. Nashindwa niandike vipi ili upate kunielewa.

Maybe ujiulize mwenyewe maswali yafuatayo:-

...

Mkuu Nziku mawazo yako ni mazuri sana.
Yanaonyesha kwamba hukujua msingi wa hoja.Kwa hiyo kwakweli hata huwezi kutoa hoja za msingi.
Lakini asante kwa mwazo japo hukujua msingi.
 
The success or failure of a society is reflected by the current regime in power. therefore the ccm Leaders should shoulder all the blames for the mess up

Wow!
Its a big task to be in power then.
 
ccm wamefulia ndugu yangu hao ndio wenye dola huwezi kumlaumu yule ambaye hayuko jikoni hata cku moja
 
Back
Top Bottom