LATRA Mwanza, Mmeongeza nauli za dalala ila imekua kero mno kwetu abiria kuulizwa kama una mia au dola wakimaanisha sh mia moja

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,377
Hili ongezeko la nauli limekuwa kero sasa na Makonda wanacheza na mziki wa viongozi wa LATRA ambao wao wana matumbo ya kushiba na familia zao

Huku Mwanza sijaona faida ya LATRA kuongeza nauli zaidi ya kero ya kuombwa shilingi mia mia " una mia hapo " ndo kauli za makondakta wa daladala za Mwanza.

Mia mia zinazoombwa na makondakta baada ya LATRA(CCM) kuongeza nauli kwa mwaka mara 2 chini ya mwenyekiti wao binti Samia Suluhu bin Hassan imekua kero mno kwa wasafiri.

Samia ongea na watendaji wako hasa wa sekta ya usafirishaji kama mmeamua kuongeza nauli za dalala muwape kabisa na chenji mia mia mnakera mno.
 
Hili ongezeko la nauli limekua kero sasa na makonda wanacheza na mziki wa viongozi wa LATRA ambao wao wana matumbo ya kushiba na familia zao

Huku Mwanza sijaona faida ya LATRA kuongeza nauli zaidi ya kero ya kuombwa shilingi mia mia " una mia hapo " ndo kauli za makondakta wa daladala za Mwanza.

Mia mia zinazoombwa na makondakta baada ya LATRA(CCM) kuongeza nauli kwa mwaka mara 2 chini ya mwenyekiti wao binti Samia Suluhu bin Hassan imekua kero mno kwa wasafiri.

Samia ongea na watendaji wako hasa wa sekta ya usafirishaji kama mmeamua kuongeza nauli za dalala muwape kabisa na chenji mia mia mnakera mno.
Kuna wengine hawajui ongezeko la 100 kwenye nauli,leo Konda nimekuta wanatukanana na Mama mmoja kule Ilalila,Bi.Mkubwa katoka Buhongwa kwenda Ilalila,analipa 1200 na Konda amekata 1400!
Nyie kwenye Daladala Mwanza kuna vituko sana,Bi.Mkubwa anadai hatambui ongezeko la nauli!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Upungufu wa 100 mtaani sio kazi ya Latra; ni jukumu la BoT kuhakikisha zinakuwepo za kutosha kwenye mzunguko. Habari njema ni kwamba zimepanda thamani ghafla. Sarafu ya 100 inatunzwa siku hizi.
 
Dsm tulishazoe kitambo mambo hayo,ila mwanza napo pa kishamba sana hadi leo hii vipanya vipo katikati ya mji.
 
Back
Top Bottom