Nimeshasikia na kuona irresponsible governments lakini hii ya Kikwete ni mwisho.Ndugu zangu,hivi mnajua kwamba sasa watu wanamuita Kiwete badala ya Kikwete,loo, mbayaaaa.Ukiwete huu uko kwenye maeneo mengi wote tunayajua,lakini leo nitaongelea hili la mabomu ya Mbagala.
Hivi kulikuwa na sababu yeyote kweli ya wananchi wetu wale 25 au hata zaidi kuuwawa.Jamani hivi hatuna vichwa jeshini vya kuweza kujua kwamba mabomu yale katika mazingira yalipokuwa yatalipuka.Mungu wangu kweli tuamini hivyo. Na kwanini mabomu yahifadhiwe kwenye kadamnasi ya watu kule mbagala.Kwanini lakini.Mtasema jeshi ndilo liloanza kujenga kambi yake halafu wananchi ndio wakaja.Sawa lakini serikali haikuwawaona?Kama wanachi wameshakuwepo karibu kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kuyahifadhi mabomu yale Mbagala.Kwa nini hayakuhamishwa.Si kuna makambi yetu mengi yaliyopo mbali na watu,kwanini hayaku hifadhiwa huko.
Sasa wabomu ya awali yameshalipuka,lakini bado tunaona na kusikia mengine yakiendelea kulipuka.Jamani hivi ni kitu gani hasa kinaendelea.Hivi Watanzania tumefika mahali we can't do anything right.Hawa watu hasa watoto ambao wanaishi katika mazingiza ya milipuko ya mabomu kila kukicha, tunategemea wawe watu wa aina gani baadae?Serikali inapashwa kukumbuka kwamba hawa nao ni watu,na uzembe huu uliokidhiri na kuvuka mipaka una athiri maisha yao na ya vizazi vyao kwa kiwango kikubwa
Lakini katika mazingira ya kushangaza bado namuona Waziri anayehusika anedelea kupeta!Hivi nchi hii hakuna swala la uwajibikaji kabisa.Mbona Mwinyi aichukua collective responsibility kwa yale yaliyotokea magereza?Watu wamekufa kizembe,lakini Wazini na wahusika wengine wanaendelea kula kuku kwa mrija.Hivi kuna nini hasa?
Sawa tutamlilia Mungu katika hili, kwa kuwa ndiye pekee sasa aliye baki kuwa mtetezi wetu.Tukaze moyo watanzania Mungu yupo.