Laiti kama tungekua na ubabe wa kiarabu, hakuna timu ngeni ingetamani kuja kucheza Kwa Mkapa

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,363
9,238
Mtu mmoja aliwahi kusema huwezi kuwa Shujaa kama sio mhuni,

Huenda usinielewe yaani kua mhuni ndo kua Shujaa? sizungumzii uhuni kama ule wanaofanya wapiga ngeta mitaa ya chanika na keko. Hapa naongelea uhuni wa kua na kiu, mipango na juhudi za kupambania kitu bila uoga.

Kwa miaka mingi ligi ya Tanzania imekua ikipambwa na sifa na tambo kibao lakini haikua na ushawishi hadi pale Azam alipowekeza mamilioni ya fedha na kufanya ionekane live kwenye luninga.

Zamani ilikua ni nadra Sana watu kujaa uwanjani kushudia game ya Simba na mtibwa au Simba na Ndanda lakini sio Zama hizi, Leo ni Rahisi uwanja kutema Pale Yanga atakapocheza na Kagera sugar pale Taifa.

Kuna kitu kimeongezeka na ndio maana ligi yetu inatajwa kua na mvuto ukanda huu wa Afrika mashariki na kati. Ndio, Simba day au siku ya Mwananchi unaweza jua huenda ni Fainali ya kombe la dunia au uefa Kwa jinsi viwanja vikavotema usisahau siku ya derby Kati ya Simba na Yanga. mtoto hua atumwi dukani. uwanja utajaa Hadi kumwagika.

Kwa miaka hii timu za Simba na Yanga zimekua zikafanya poa michuano ya kimataifa hivo wageni wengi wanaifatilia Sana ligi na pia hizo mechi hutizamwa na watu wengi barani Afrika na duniani. Ni kweli watanzania tunapenda mpira ni kweli tunajaa uwanjani Ila shida yetu ni moja tu. Bado hakuna mashabiki wengi wetu hua tunaenda kuangalia mpira na tunashangilia Goli au matukio flani flani.

Hebu fikiria kwanini timu zetu zikienda kucheza mechi huko uarabuni hua tunawaza Sana?? sio kwamba wydad Casablanca wanacheza soka kama watu wa kwenye PS no.! Au Al Alhy wao ni machine za kucheza soka! Inshu kubwa ni mashabiki, wao Wana mashabiki wanaotukia uoga yaani hata kabla game haijaanza unahisi lazima tu ufungwe..

Laiti kama wabongo tungeweza kushangilia walau hata nusu ya wanavofanya waarabu basi Kwa mkapa tangekua Goligotha..
Pangekua panatisha kama Gaza pangekua ni uwanja wa vita. Lakini Kwa sasa bado ni kweli wapinzani wakiingia uwanjani hua wanaogopa umati wa watazamaji lakini baade hupata faraja baada ya kujua hamna washabiki. Laiti kungekua na mashabiki kina Raja wasingeshinda kizembe au pyramid asingemtwanga mtu bongo..

Najua Roma haikujengwa Kwa siku moja, nafurahi coz wabongo ni wepesi wa kujifunza
natamani kuona tukiiga hili Jambo. Naamini ligi yetu itakua kitu spesho hata mgeni akija kucheza tz atakua anakuja huku akijua amekuja machinjioni.

images%20(6).jpg
View attachment 2578299View attachment 2578301
 
mashabiki wa Esparance,Wydad,Raja na Al Ahly ni level zingine,wanamzingua kwanza mpinzani alafu anakutana na kipigo uwanjani.

tz kwa speed ya mpira wa bongo tuliyonayo kufika huko pia inawezekana.
 
Nidhamu ya uoga inaondoa confidence, confidence ndo inaleta morali waliyonayo wenzetu
Umaskini nadhani ndio tatizo kubwa,watu wamepigika,ela ya msosi Ni tatizo,alipe kiingilio akaangalie mechi,anawaza jioni atapiga desh.isingekua hivyo,tungekua tukijaza uwanja Sana,shagwe za kutossha,watu wanaimba kuwapa morali wachezaji vya kutosha,Sasa mtu ajala mchana ,kabana hiyo ela akalipie kiingilio,ata hiyo sauti utatoka kweli?ni kwa wachache.mtazamo
 
Ile style yao ya kuhanikiza kwa kuimba huwaga na vibe sana...kwa tz zile mgoma zetu zimepitwa na wakati...
 
Kulinganisha na uchumi wa wenzetu Morocco,wao wako mbali,mpira wa Sasa fedha pia Ina nguvu kubwa,uswahili,mishahara n.k
 
Yani nilipe kiingilio changu halafu ukanipigishe kelele Uwanjani!kuweni sirias basi..mbona kuna timu zinashinda ugenini?Mayowe uwanjani hayashindishi timu kama mnabisha hao mnaosema wanahanikiza kila siku wanachezea wakishiriki club bingwa Dunia.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
WAARABU hawamjui Mungu.

Wa kushangiliwa na kupewa Utukufu ni Mungu pekeee.....

Haya ma MIPIRA si ya kuyashangilia sana Hadi tukamsahau Mungu.
 
Umaskini nadhani ndio tatizo kubwa,watu wamepigika,ela ya msosi Ni tatizo,alipe kiingilio akaangalie mechi,anawaza jioni atapiga desh.isingekua hivyo,tungekua tukijaza uwanja Sana,shagwe za kutossha,watu wanaimba kuwapa morali wachezaji vya kutosha,Sasa mtu ajala mchana ,kabana hiyo ela akalipie kiingilio,ata hiyo sauti utatoka kweli?ni kwa wachache.mtazamo
Well said.
 
Ile style yao ya kuhanikiza kwa kuimba huwaga na vibe sana...kwa tz zile mgoma zetu zimepitwa na wakati...
Yap nazani vilabu vyetu vitunge nyimbo za hamasa ambazo shabiki watakua wanaimba uwanjazima Kwa vibe la hatari
 
Back
Top Bottom