Laigwanani Ole Kisongo ashindwa kumfanyia mila Lowassa

Ruwamangi

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
949
1,683
Kama ambavyo tulielezwa hapo awali

Kuwa Waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa angezikwa kimila kwa mujibu wa kabila la Kimasai.
Ambapo angepakwa mafuta ya kondoo kisha wajukuu na watoto nao kupakwa na Mwisho mwili wake kuzikwa ukiwa umekalishwa kwenye Kigoda hali hiyo imekuwa tofauti!

Lowassa ambaye ni Kiongozi (Laigwanani) wa jamii hiyo aliwaunganisha jamii ya kimaasai kwa upande wa Afrika Mashariki mpaka Ethiopia kutambuana na kushirikiana katika maswala ya maendeleo.

Jambo hilo limeshindikana kuzikwa kimila na Malaigawanani
ambao wameweka kambi kijijini Ngarash toka juzi wakiongozwa na Laigwanani wa Tanzania Izack Ole Kisongo Meijo.

Baada ya mbele ya kaburi la Lowassa akiongozana na malaigwanani wengine walimfanyia ibada ya maombi tu kwa lugha ya Kabila la kimaasai na kutamka familia imeomba waheshimu Imani ya Laigwanani Lowassa ya Kilutheri.

Na hivyo hawatapaka mafuta.

Ole Kisongo ni Laigwanani wa jamii ya Kimasai ambae makazi yake yako Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
 
Kama ambavyo tulielezwa hapo awali

Kuwa Waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa angezikwa kimila kwa mujibu wa kabila la Kimasai.
Ambapo angepakwa mafuta ya kondoo kisha wajukuu na watoto nao kupakwa na Mwisho mwili wake kuzikwa ukiwa umekalishwa kwenye Kigoda hali hiyo imekuwa tofauti!

Lowassa ambaye ni Kiongozi(Laigwanani) wa jamii hiyo aliwaunganisha jamii ya kimaasai kwa upande wa Afrika Mashariki mpaka Ethiopia kutambuana na kushirikiana katika maswala ya maendeleo.

Jambo hilo limeshindikana kuzikwa kimila na Malaigawanani
ambao wameweka kambi kijijini Ngarash toka juzi wakiongozwa na Laigwanani wa Tanzania Izack Ole Kisongo Meijo
Baada ya mbele ya kaburi la lowassa akiongozana na malaigwanani wengine walimfanyia ibada ya maombi tu kwa lugha ya Kabila la kimaasai na kutamka familia imeomba waheshimu Imani ya Laigwanani lowasa ya Kilutheri.

Na hivyo hawatapaka mafuta.

Ole Kisongo ni Laigwanani wa jamii ya Kimasai ambae makazi yake yako Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Aisee.

Sumaye naye vipi sijamsikia wakati ni mmasai mwenzake.
 
Hawa watu wakiingia kwenye Ukristo na Uislamu hizo mila kufuata inakuwa vigumu.

Wanaweza kuigiza hapa na pale kisiasa, lakini kwenye kuzikwa wanarudi kanisani au msikitini.
Kinachozipa ushindi imani hizi za kigeni dhidi ya imani zetu za asili ni fundisho la maisha baada ya kifo.

Angezikwa kimila ingefifisha matumaini ya kwenda mbinguni.
 
Kinachozipa ushindi imani hizi za kigeni dhidi ya imani zetu za asili ni fundisho la maisha baada ya kifo.

Angezikwa kimila ingefifisha matumaini ya kwenda mbinguni.
Waafrika tumekubali mila zetu ni za kishenzi kwa kiasi kikubwa.

Yani mtu anapenda ajinasibishe na Azania Front au Msikiti wa Tambaza kuliko na mila zake za Monduli au Mkuranga huko.
 
Back
Top Bottom