Kwenye suala la Burigi nasimama na uamuzi wa waziri na Serikali, tukosoe yenye tija na tuache upotoshaji

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Katika mitandao ya kijamii kuna mjadala mkubwa unaoendelea kuhusu uamuzi wa Serikali kupindisha Poli la Akiba la Burigi na kuwa hifadhi ya Taifa, baada ya uamuzi huo kn baadhi ya wafuasi, wananchama na viongozi wa vyama vya Upinzani Nchini vimerkurupuka na kudandia sanjari na kupotosha kuhusu uamuzi huo wa Serikali!!!!!

Sitanii tangu vyama hivyo vimebaini ujinga na uvivu wa Watanzania kuchakata taarifa wanazopewa, havipati shida ni mwendo wa kupumba tu story!!! sishangai kuona wananchi wengi mitandaoni wakiamini propaganda za vyama hivyo kwamba katika eneo hilo kabla hakukuwa na wanyama wowote!!! yaani baada ya uamuzi wa Serikali ndipo iwameanza kupelekwa kutoka katika hifadhi zingine.

Sina namna zaidi ya kusema wote wanaoamini hivyo ni WAJINGA na tukiendelea na utamaduni huo wa kuamini kila jambo pasipo kulipima kamwe taifa letu haliwezi kusonga mbele. Kwanini nasema hivyo??? Kilichofanyika sasa ni kulipandisha hadhi pori la akiba la Burigi na kuwa hifadhi ya Taifa. Kwa Lugha nyingine lilikuwa tayari limeshatambuliwa na Serikali za nyuma.

Kuna wengine hoja yao ni eti limepandishwa kwa sababu linapatikana karibu na Chato ambako ni Nyumbani kwa mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI, hoja hii ni dhaifu na nyepesi sana, yaani tumefikia pahala ambapo wananchi wa maeneo anayotoka Rais au jirani kutopata huduma na shughuli za maendeleo yanayostahili kwa sababu tu Rais anatoka eneo hilo? huu ni ubaguzi mkubwa mono.

Kwa manufaa ya wengi kinyume na inavyoelezwa mitandaoni Pori la Akiba la Burigi lilikuwa tayari lina Twiga, kiboko n.k kudhihirisha wanyama waliopo bofya

 
Naunga mkono hatua ya kuyapandisha hadhi hayo mapori kuwa hifadhi za taifa

Kwangu mimi ukiacha faida za kiutalii & kimazingira, mapori hayo kwa kufanya kuwa hifadhi za taifa yana manufaa pia ya kiulinzi & usalama

Hapo mwanzo mapori hayo yalikuwa yakitumika kama mafichio ya wahalifu, wahamiaji haramu kutoka Rwanda & Burundi, pamoja na mambo mengi mabaya
 
Nikishaona mtu anachukua maoni ya mitandaoni na kuyapachika kuwa maoni ya vyama vya siasa hasa upinzani, huwa namuona mtu huyo ni mshenzi wa hali ya juu mwenye dhamira ya kuuchafua upinzani. Hii mitandao ya kijamii ni kwa ajili ya mtu yoyote bila kujali ana chama au hana. Unapogeuza maoni yoyote humu yaliyo kinyume na utashi wa serikali ni ya upinzani ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Kama mmeshindwa kutetea jambo mlilofanya huo ni udhaifu wenu. Kutaka kurushia wapinzani maamuzi yenu ni utoto kama utoto mwingi maana humu sio ofisi za chama chochote cha siasa.
 
Back
Top Bottom