Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?

Sehemu kubwa ya Kilosa/Mvomero kitunguu kinamea, nina rafiki analima Msowelo sasa hivi, ukitaka kujua vyote vilivyopo Msowelo sema nikuunganishe kwa simu akupe majibu usiku huu huu.
Mkuu kwanza ningetanguliza shukrani zangu sana tu,maana kwa wazo tu la kutaka kuniunganisha na jamaha umeonyesha wewe ni mtu wa aina gani kwa kupenda maendeleo ya jamii nzima!ningeomba uni PM namba yake huyo mheshimiwa wa Msowelo,ili niweze kupata mwanga zaidi toka kwake!againg thanks a lot mkuu!
 
Kwenu wapi mkuu Mpigaji...........na vipi kuhusu upatikanaji wa ardhi na gharama nyingine?

Mimi ni miongoni mwa wasioweza kuitofautisha miti hii..........niko Dodoma wapi hasa nikashuhudie? Je yale maeneo ya kulekea Ikulu ndogo ya Chamwino...........kuna miti mimgingi imepandwa kwenye nafasi kubwa ni mizeituni nayo maana inayo sifa ya ukijani karibu mwaka mzima.

Dodoma maharage si sana nadhani utakuwa unailenga Morogoro; kwa maeneo inayopakana na Dodoma........kwenye wilaya ya Gairo; njianai akuna aiana kadhaa za maharage nakuna nayo yakiuzwa.

Umegusa mkoa wa Lindi................mkoa huu unafaa kwa kilimo kipi ukiacha mikorosho?

Lindi hasa wilaya ya kilwa ufuta unakubali sana kilimo hiki ni cha muda mfupi wanapanda january mpaka march kuvuna jun na bei ya ufuta ipo juu mwaka huu bei imeanzia sh2500 kilo ,ekamoja unapata mpaka gunia kumi ila wanalima kienyeji hawakwatui ardhi bali wanatoa majani tu nakulima

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Kwetu tunayaita mandwenje yanapendwa sana na tembo hata binadamu ukiyala lazima ulegee

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Mwezi april nitawatika kilo nne za acrocarpus Iringa na Mby,ukizihitaji nijulishe nikupe mhusika akupe, ni Tsh 20,000/ kwa kilo,hakuna kulala.Bee farm tayari iko online, may mwaka huu mizinga kadhaa lazima itundikwe kule Kilolo.

Kwakweli leo nimefika nilikokutaka ,tafadhar naomba nipate elimu ya nyuki kwani huku nilipo kunanyuki wengi balaa watu wanarina asali porini pasipokuwafuga na asali ni nyingi sana naomba elimu wakuu ikiwa ni pamoja na kutengeneza mizinga

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Mkuu kwanza ningetanguliza shukrani zangu sana tu,maana kwa wazo tu la kutaka kuniunganisha na jamaha umeonyesha wewe ni mtu wa aina gani kwa kupenda maendeleo ya jamii nzima!ningeomba uni PM namba yake huyo mheshimiwa wa Msowelo,ili niweze kupata mwanga zaidi toka kwake!againg thanks a lot mkuu!

Nimekutumia kwa pm mkuu, kazi kwako.
 
Kwakweli leo nimefika nilikokutaka ,tafadhar naomba nipate elimu ya nyuki kwani huku nilipo kunanyuki wengi balaa watu wanarina asali porini pasipokuwafuga na asali ni nyingi sana naomba elimu wakuu ikiwa ni pamoja na kutengeneza mizinga

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

Uko mitaa gani ya Tanzania? Unaweza kuta kuna mdau namfahamu karibu yako.
 
Lindi hasa wilaya ya kilwa ufuta unakubali sana kilimo hiki ni cha muda mfupi wanapanda january mpaka march kuvuna jun na bei ya ufuta ipo juu mwaka huu bei imeanzia sh2500 kilo ,ekamoja unapata mpaka gunia kumi ila wanalima kienyeji hawakwatui ardhi bali wanatoa majani tu nakulima

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

Ndugu Usiniguse ulichosema ni ukweli kabisa. Kwa sasa nipo Ruangwa nafanya utafiti wa kulima zao hilo. Bei ya ufuta huku ni 2400 kwa kilo. Ila nimegundua Kilwa wanalima sana ufuta. Na bei huko Kilwa imefika 2530 kwa kilo. (UFUTA NI ZAO LA AJABU SANA, MAVUNO YAKIWA MENGI NA BEI INAPANDA ZAIDI KWANI WANUNUZI WANAKUJA KWA WINGI NA USHINDANI UNAKUWA MKUBWA). Kesho naelekea Kilwa kumalizia utafiti wangu. Nimegundua sehemu yenye mikorosho mingi hawalimi ufuta kwa wingi. Kilwa wao mikorosho sio mingi kama Ruangwa hivyo wanalima ufuta mwingi sana.
 
Ukifika Kilwa nishitue ili kama unahitaji mwenyeji nikupe akupe shavu, niko Kilwa mtaa wa pili napigika mkuu wangu. Ok ni kilwa Masoko au Kivinje au kisiwani au any place ndani ya Kilwa?
 
Wakuu hii document inahusika sana kwenye huu uzi
 
Attachments

  • Crop suitability.pdf
    318.9 KB · Views: 170
da ni noma vjana wa xaxa 2kijikita ktk kilimo ndio njia pekee itakayo 2toa mm nampango wa ku go mkoa wa katavi kuna jamaa yangu kafaidka na fursa hii mm niko tabora kilimo huku ni kama tabu kidogo coz place nilipo igunga kilimo kinacholipa xana ni
mpunga place ni mwanzugi blplm ni bei ya kukodi ni ndef xana kama kilo 2,3...lakn ukilma unatoka milele ndio hvyo coz maji ni miaka yote yanaflow kama unamtaj iko poa xana
 
malila ngano mbeya vp inakubali?

japo swali lilikuwa la malila naomba nimsaidie kujibu kuwa mbeya ngano inastawi vizuri sana mfano hai ni pale taasis ya utafiti wa mazao mati-uyole ila tatizo ni ardhi.
 
..
Location: Sanya Juu, West Kilimanjaro, Hai district,Kilimanjaro region

Potential agro : Vanilla

Export Market : Kenya, Europe and UAE

Seasonal crop
LAT,
Tayari Maruk Vanilla Farming and Processing Ltd tumeingia Kilimanjaro toka mwaka 2011 kukuza zao la Vanilla. Tunafanya kazi kwa karibu na Chama cha Wakulima wa Vanilla Kilimanjaro (CHAWAVAKI) chini ya Mtanzania mwenye hamasa na maendeleo ya watu-Profesa Nkya. Tunawakaribisha wakulima kujiunga nasi kukuza kilimo cha zao hili na kufaidi mapato yake.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Vannila nayo nasikia inalipa sana na inakubali Kagera na Kigoma wenyeji wa hiyo mikoa wanaweza kutoa data zaidi za hili zao na upatikanaji wa ardhi
Vanilla ni zao linakubali kwenye maeneo yenye mwinuko na mvua za wastani. Linachavua vizuri vichakani au kwenye shamba lenye uvuli na miti ya kutoa support. Ni changamoto kulima vanilla nyikani maana itakuhitaji kutafuta miti ya kutoa support kwa malando ya vanilla. Kwa Kagera na Kilimanjaro vanilla inalinwa mashambani ambako tayari kuna migomba. Tumejaribu pia kwa mafanikio kueneza zao hili Tanga-Muheza ambako mti unaotoa support kwa malanda ya pilipilimanga (black pepper) unatumika pia kutoa support kwa vanilla. Mkoa mwingine ambao tunaendelea nao vema ni Morogoro. Tuna kikundi kinaitwa TANDUSENI ambacho miaka ya nyuma kilikuwa chini ya JICA.
 
Na vp kuhusu soko lake ni la uhakika? Je sehemu kama Dodoma Vanilla inaweza kubali ukiweza fanya kwa irrigation? au ni lazima eneo liwe la miinuko?
 
Wadau kuna huu mti nimeuona upareni unaitwa MKAULIA je ndio pines au cyprus au unaitwaje kwa kitalamu
 
Naiona Tanzania mpya mbele yangu yaja kwa mapinduzi ya kijani. Kipindi kinakuja tena kilimo kitaheshimika maana ni kama tuliiacha asili watu wakakimbilia white collar jobs wakipigana majungu maofisini.
Furaha yangu ni kuwa kilimo kijacho ni cha kibiashara. Watu wamekubali kuwekeza vyakutosha mali na maarifa kwenye kilimo. Hakika WOSIA wa Baba kuwa ''kama mnataka mali mtayapata shambani'' sasa umegusa mioyo ya wenye nia.
Wenye ujuzi kwenye kilimo endeleeni kutoa maarifa bila ajizi huku mkifikiria kuwafikia walengwa vijijini ambao wanaishi na ardhi tele wasiitumie kwa manufaa yao kwa kukosa maarifa.
Mungu awabariki sana.:amen:
 
Na vp kuhusu soko lake ni la uhakika? Je sehemu kama Dodoma Vanilla inaweza kubali ukiweza fanya kwa irrigation? au ni lazima eneo liwe la miinuko?

Nasubiri hili jibu kwa hamu sana, lakini vanilla amekuwa mgumu wa kutupa feedback
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom