SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,923
- 2,003
Bei Ya Ukumbi Na Vinywaji Vinaweza Kuwapa Maharusi Hata Kiwanja Huko Madongo Kuinama
huwa najiuliza mwisho wake lini watanzania wa hali ya kati na chini kimaisha, hasa mijini, wataachana na ulimbukeni wa kufanya gharama kubwa za harusi?
Tukio ambalo linachukua mamilioni halafu linafanyika within few hrs watu wanakula wanakunywa wanaondoka, bajeti ya milioni 9 baada ya honey moon maharusi wanayaanza maisha kwa taabu kulipa madeni n.k., kwanini watanzania hatubadiliki?
Wazungu miaka ya nyuma walishapita humu wakabadilika miaka mingi ilopita karne hii wakihudhuria harusi zetu wanatushangaa na kutuona ni matajiri sana kumbe hamna kitu!
Kweli hatukatai wapo wanaojiweza kifedha wacha wafanye, lakini wenzangu na miye unajikamua unafanya sherehe kubwa na mnaendelea katika circle ya kuchangiana the whole year unajikuta unachangia harusi tu, sijui kama kuna wanaopiga hesabu ya hizo kadi familia iliochanga kwa mwaka na si kana kwamba ina mwisho, no, na mwaka ujao hivyo hivyo.
Tuamke watanzania, tufanye harusi za gharama ndogo, kama ni swala la kuchangishana basi tuchangishane ada-fees-watoto wakasome vyuoni malaysia, london na us, matunda yatakuja onekana. Wakenya wenzetu waliliona hili mapema, leo wengi ni maboss ktk nchi yetu wenyewe!
Tubadilike watanzania! Harusi nacho ni chanzo cha kutiana umasikini!
bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest
Bei Ya Ukumbi Na Vinywaji Vinaweza Kuwapa Maharusi Hata Kiwanja Huko Madongo Kuinama
Kwaiyo kama mtu ana uwezo unataka asiji enjoy? Msio na uwezo jikuneni mkono unakofika
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest
hahahaaa chai maandazi duh..hiii kubwa kulikoBora kwetu Uswazi tunaweka kitu cha kigodoro tu night nzima asubuhi chai maandazi.Harusi imeisha.
Tafadharini naombeni kipimio cha kudhibitisha kuwa hii ni ndoa ya gharama na hii ni kawaida na hii ni ya chini.
Kwaiyo kama mtu ana uwezo unataka asiji enjoy? Msio na uwezo jikuneni mkono unakofika
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest
Mimi hapa nilpo nina kadi sita na nne kati ya hizo zina kiwango(single elf 30,double 50).
Hadi sendoff kadi jamani?
Mara nyingi harusi za gharama..mwisho wake ndoa haidumu..!
Unafaa kuwa Mwalimu au Doctor, mambers wote wa JF tungekuwa kama wewe basi JF ingekuwa na heshima sana asante kwa kunielimisha.Kipimo ni uwezo wa mtu binafsi. Mtu eti inaandaliwa harusi ya bajeti ya 15m halafu bwana harusi yeye ana 1m; zilizobaki zote ni wanakamati na ndugu wakunjane mashati mpaka zipatikane.
Mimi nimewahi kuwa mwanakamati mara 3 aisee ni stress tupu!! Bajeti kubwaaa, pesa hakuna bwana harusi nae anasema hana pesa.
Lakini ukifanya kitu kadri ya uwezo wako,huchangishi mtu huna stress wala huanzi maisha ya ndoa na stress, safi kabisa.
Tafadharini naombeni kipimio cha kudhibitisha kuwa hii ni ndoa ya gharama na hii ni kawaida na hii ni ya chini.