Kwann uznz syo kosa la jna Tanzana?

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Katıka nchı nyıngıne uzınzı (adultery) nı kosa la jınaı na mtu anaweza kushıtakıwa. Kwa Tanzanıa, ukımfumanıa mkeo/mmeo unachoweza kufanya nı kufungua shaurı la madaı na kumdaı mgonı fıdıa. Je kuna mtu yeyote anayejua kwanını uzınzı sıyo kosa la jınaı Tanzanıa?
 
unataka watanzania wote wahamishiwe gerezani?
Tena watunga sheria ndo watakuwa gereza first class.
 
Kama vile ni utamaduni wetu. Ingekuwa kosa la jinai watu wangeishia magerezani.
 
Katıka nchı nyıngıne uzınzı (adultery) nı kosa la jınaı na mtu anaweza kushıtakıwa. Kwa Tanzanıa, ukımfumanıa mkeo/mmeo unachoweza kufanya nı kufungua shaurı la madaı na kumdaı mgonı fıdıa. Je kuna mtu yeyote anayejua kwanını uzınzı sıyo kosa la jınaı Tanzanıa?

Kwa sababu marais, maaskofu, ma imam, ma shehe, mawakili na majaji wote ni wazinzi!
 
Inategemea jinsi utakavyowasilisha hoja yako au na mazingira ya tukio lenyewe (circumstancial evidence) lakini zaidi uzinzi umeegemea kwenye sheria za madhara (law of Torts) ambazo ni civil by nature yaani ni mlalamikaji kumdai mlalamikiwa fidia ya kosa lenyewe na hasa kwenye taratibu za kimila...................but remember - every case has its own merit!!!

However chini ya sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 na SOSPA bado unaweza kupresent case yako kama jinai as well na adhabu zake ziko chhini ya sheria ya kanuni za adhabu (penal code)!!!
 
Sherıa ya Ukımwı ınasemaje? Ufafanuzı kıdogo.
 
Sherıa ya Ukımwı ınasemaje? Ufafanuzı kıdogo.

Kifungu cha 5 kifungu kidogo cha 4 cha Sheria hii na 28 ya mwaka 2008, kinaipa malmaka mahakama kutoa ridhaa ya mazingira ya mtu kupima sero status kwa shuruti, ukijenga hoja yako vizuri baada ya kubaini uzinzi utaiomba mahakama kupitia kifungu hiki kisha nenda kifungi=u cha 21 (1) ambacho kinasema kwamba yoyote anayejijua ana maambukizi anatakiwa amtaarifu mngoni mwenzake juu ya hali yake, endapo mgoni atagunduilika na maambukizi yaani amemuambukiza mkeo kwa tendo hili huku akijua yu +, hapa kesi inakuwa ya jinai.............!!!!na adhabu yake ni faini au kifungo cha miezi 3-6 21(3)

Japo kuwa mara nyingi criminality ya kifungu hiki inaweza kuwa na utata sana akini mahakama ndiyo yenye mandate ya kutafsiri merit ya tukio..................inaangaliwa Intention, conduct and consequence.................implication, complications and repucations kwa kutumia deduactive ama inductive reasoning

Natumai umepata kidogo
 
Adultery (uzinzi) ni kosa la jinai Tanzania kwenye Kanuni ya Adhabu (Penal Code)
 
Back
Top Bottom