Great thinkers,
Katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha na wale waliokwenda vituoni siku ya uchaguzi inafikirisha sana.Watu wengi hawakwenda kupiga kura.
Tujiulize ni kwanini.
1.Rafu za wasiotaka kushindwa ambao hununua kadi za wapiga kura na kuzitupa barabarani wakishatangazwa washindi?
2.Watu wamekata tamaa na hivyo hawaoni umuhimu wa kupiga kura?
3.Watu hawajajua umuhimu wa kupiga kura?
Maswali ni mengi na majibu yake sio mepesi.Sisi tunaojua umuhimu wa kupiga kura tuna jukumu la kutafuts sababu zinazowafanya watu wajiandikishe kwa wingi,mikutano ijae wakati wa kampeni lkn idadi iwe pungufu baada ya matokeo kusomwa/kutangazwa kama tulivyojionea leo hii matokeo ya kura za ubunge wa jimbo la Igunga.
Tutafakari kwa pamoja na tuiokoe nchi yeti iliyo katika hatari ya kuporomoka kwa demokrasia maana uchaguzi bila idadi tosha ya wapiga kura ni upuuzi mtupu unaoweza kuwaweka madarakani wapuuzi na hivyo kuwatia kitanzi watanzania maskini
Taarifa ya Tume ya taifa ya uchanguzi siyo sahiii.Watu waliojiandikisha kuna majina bandia ndani ya vitabu hivyo