Muyobhyo
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 8,149
- 6,535
anaweza akawa ni ndugu yakoyaani utambulisho wowote mitaani ushwahili au vijijini achilia mbali makanisani utakuwa haujakamilika kama mgeni hajajulikana ni kabila gani.
japo swali hilo huulizwa kwa nia njema lakini binafsi huwa naona kero kubwa.
kuna watu maofisini bila hata kugundua utajikuta wameshafanya viutafiti na kujua kila mtu pale ni kabila gani.
Madhara yake wakishajua ni kabila gani chochote utakachofanywa kitahusianishwa na kabila lako na sio wewe kama mwanadamu hai mwenye uwezo huru wa kuchagua cha kufanya.
unadhani chanzo ni nini na nini suluhisho?