Kwanini Watanzania hatuamini na hatutaki kuwekeza kwenye kilimo ?

Inasikitisha jamani!
Watu tumewekeza kwenye kilimo kweli kweli!
Sasa mimi sijui ni msomali au ni muethiopia?
Acha kuwadanganya wenzio, Watanzania wengi sana awamu hii wamewekeza kwenye kilimo!
Duh jamani unatia aibu walahi!
ni vizuri kuwekeza kwenye kilimo
lakini tabu kubwa inakuja kama watafunga mipaka hivyo mazao hayatoka nje ya nchi.

hapo chungu ya kilimo utaiona
 
kilimo wengi wetu kinatushinda pia muda wa kusimamia.. ni rahisi kusimamia kiduka chako mjini kuliko kusimamia shamba mbali na unapoishi.. mwisho wa siku unanufahisha wasimamizi tu...

sio kama hatutaki shida mjini hakuna mashamba na wengi wetu tumeajiriwa huku mjini.. muda wa kwenda shambani mkoani hakuna
Tatizo siyo usimamizi, tatizo serikali, unalima unatumia gharama kununua mbegu, kuandaa samba, kulipia wafanyakazi

Halafu unavuna anatokea mpuuzi mmoja anakupangia ukauze wapi mazao yako.. WTF
 
Lakini wakati tukilia na bei ya mihogo hapa nyumbani, kuna nchi jirani ambako tunaweza kuuza kwa bei nzuri tu mfano Burundi, Rwanda, Sudani Kusini n.k
Kuna mazao yanauzwa Nje kwa sasa?
 
Hivi wakati wanajadili Bungeni kile Kikao cha mwisho kabla hawajaahirisha wewe ulikuwa wapi!? Unaambiwa Muhogo sijui Mbaazi ukiachana na Pamba na Korosho, bei imeshuka toka2000/= mpk 150/= unadhani nani atathubutu kulima zaidi ya mchicha nyuma ya Nyumba!? Sera na ushawishi wa kumshawishi Mtanzania kuingiza hela zake kwenye Kilimo ni ngumu, bado Ushuru na kodi na kipindi hicho bei wanajipangia wanunuzi na no free market
Vipi ndugu nawe umekata tamaa kwenye kilimo?
 
tatizo wakijua wewe wa town eka moja kukodi unaambiwa laki 4, vibarua ndo kabisa kwa siku anataka 5000,, bado trecta hapo si ajabu ukaambiwa laki 3 kwa heka, hizo ukilinganisha unaamua kugaili tu,,
Wapi uko Kukodi laki nne, njoo nikuuzie kwa laki mbili tu kila ekari ,ulimiliki kabisa,ardhi haiozi,atalima ata mjukuu wako
 
Kilimo ni maji ya uhakika, kama maji ya kunywa tu tunafuata km 12 vipi maji ya kumwagilia? Au unataka tuishi kwa kutegemea mvua?
 
Jibu ni kwamba hakilipi mpaka sasa ni melima mahindi na mpunga bei hazieleweki. Ni meamua kuweka stoo mpaka mwezi wa pili. Sasa hapa katikati kuna ada za watoto. Huoni wao wanafanya siasa haina hasara
 
Nikikumbuka hawa inspiration speaker wanasema tanzania tuna mkataba china eti tulime mhogo kwa wingi. Kigoma sasa hivi kilo ya muhogo ni sh. 150 alafu watu walime mengi kama mbaazi ya kwenda India wakigoma kununua inashuka tena.

Bado kahawa na korosho

nenda kaonje ladha ya umaskini
 
Mabadiliko ya hali ya hewa
Upatikanaji wa mbegu sahihi

Ukosefu wa wataalam juu ya ushauri na utaalam juu ya zao husika

Soko sio la uhakika

Mtaji duni ( jembe la mkono)

Na mengine mengi yaani kwa kifupi kuliko kupeleka hela yako shamba bora ukacheze tatu mzuka hadi hapo mifumo itakapokuwa mizuri
 
MIMI NIMEKATA TAMAA SABABU HAMNA SOKO LA UHAKIKA.NYANYA ZINAOZA TU HAPA KILOLO
Kilimo cha kusubiri mvua.miondombinu ya umwagiliaji hakuna, Mabwana shamba wa kutafuta sana. Soko la uhakika halipo, nusu ya mazao yanaozea shambani,wakulima kukopwa,usumbufu wa traffic njiani.ukosefu wa viwanda vya kusindika na matatizo mengine mengi
 
Hili ni kama tatizo sugu ama 'donda ndugu' !

Tuna maji ya kutosha.Ardhi yenye rutuba ndo usiseme. Kila kitu kipo kasoro tu tuhela tudogo twa kulipa nyapara huko shambani.

Yaani mtu anakubali ale hasara kwenye duka lake lakini huwezi kumshawishi akaweka hapo tuhela twake kwenye kilimo. Sisi ni wagumu mno kuelewa.

Kilimo hakina makodi kodi ya hovyo hovyo. Hamna usumbufu wa EFD wala TRA huko maporini. Unalima, unauza halafu unachikichia.Kiroho safi bila shida.

Na ndo kazia ambayo unaweza kupata hela nyingi sana ndani ya muda mfupi kuliko kazi yoyote ile.

Hela ya shamba tamu sana. Ni nyingi paaapu… unaweza kuacha kazi.

Ukitaka mali utaipata shambani.Na ukitaka shida shida fungua biashara yako huko mjini.
Mkuu nimeingia kwenye hiyo sekta 2017 maisha ni safi kabisa
 
Unajenga kiwanda wakati malighafi huna....

Ardhi imejaa vijana wanajazana dar es salaam kuuza soksi na mashati mitaani.
 
Kilimo ni sayansi.. huwezi kufanikiwa kama huna hiyo. Kilimo cha kibongo bongo hakifanikiwi kwa sababu kinakosa sayansi. Bila sayansi, ni vigumu kuwa na products nzuri tena zenye viwango. Eti unategemea vichungwa kama vile vya Segera uviuze Ulaya.. thubutu! Vichungwa vimejaa ukakasi balaa. Sayansi pia itafanya uzalishaji uwe wa tija.. mathalani Egypt kwa hekta moja ya shamba wanavuna tani tisa za mpunga, maana magunia 90 ya kilo 100. Bongo kwa hekta mtu akipata magunia 30 anatangaza dunia nzima.

Serikali haijawekeza katika sayansi, kilimo cha leo na mbinu zinazotumika leo katika kilimo hazina tofauti na ilivyokuwa mwaka 1900. Kelele nyingii, kila mahali iwe bungeni au wizarani. Kiini kabisa hakiguswi..
Hayo ni ya kwangu, povu sitaki ispokuwa hoja ya kuunga mkono au hoja kinzani

Shukrani sana kwa mtoa hoja
 
Back
Top Bottom