kwanini Watanganyika wanachukia jina lao nakuita Tanzania bara?

Mandi

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
382
65
hata hapa ktk ukumbi unaposema sisi watanganyika kutakua na baadhi ya watu watatamani kutapika,wamesahau kua mkataa kwao nimtumwa wengi hufurahi kuitwa mtanzania bara,mbongo,na huchukia kuiwa mnyika.jee neno tanganyika limekwenda wapi?
 
Kizazi kipya/vijana ni wengi, nao hawajui jina la Tanganyika. Makosa yalifanywa na Nyerere, sasa kama unataka watu wabadilike na kujiita Watanganyika basi ni vyema uje na mapendekezo ya kura ya maoni. sijui kwanini tunaogopa sana kura za maoni !!!
 
hata hapa ktk ukumbi unaposema sisi watanganyika kutakua na baadhi ya watu watatamani kutapika,wamesahau kua mkataa kwao nimtumwa wengi hufurahi kuitwa mtanzania bara,mbongo,na huchukia kuiwa mnyika.jee neno tanganyika limekwenda wapi?
Mandi.

Wazee wetu wa Tanganyika walileweshwa kileo cha propaganda na Mwalimu. Wakalisahau jina la nchi yetu. Wale wachache waliokataa kileo hicho walionekana ni wahaini.

Sisi tumefungua macho tunasikia kuna nchi ya Tanzania na Zanzibar.
Nchi yetu ya Tanzania inasherehekea miaka 50 ya Uhuru wake.
Nikisoma vitabu vya historia vinasema Tanganyika kwa sasa inajulikana kwa majina mawili; Tanzania au Tanzania bara.

Hili jina Tanganyika linafanana na "Danganyika" kwa hiyo hatutaki kuitwa wadanganyika..Mwalimu alitudanganya!
 
Back
Top Bottom