Kwanini wanyama hawafanyi mapenzi kinyume na maumbile?

ungejibu swali langu, usiwe mwoga kujibu maswali kwa lengo maalum, napata mashaka pengine wewe ni victim wa haka kamchezo.
 
Then it wasnt a place to ask such a thing if someone cannot give you reasons.
Then basi mada haipo sehemu yake, sorry to say that. But thread imekua condemnation ya wanaoprefer. Without giving them a kind of environment to be reasonable of their acts. Lengo la hii thread ni nini haswa? Kupata ufumbuzi wa tatizo au kuwahukumu watendaji wa hilo jambo?

Ahsante kwa mawazo yako unayodhania kwamba ndiyo yako sahihi. Nilitegemea umesoma hii thread na kuona ilikusudia nini kumbe wapi? nilikuwa nahangaika na mtu ambaye tayari ana majibu yake kichwani, hapo unategemea nini? kama una muda unaweza ukaandika thread yenye kutaka reasons ya kwanini wanafanya hivyo sawa? lengo la hii thread ilikuwa katika mfumo wa swali ukiwataka wote wanaohusika na tendo hilo wajihoji na kuona kama kile wanachofanya ni salama? Je, watufarahi wakiona wake/dada/mama na binti zao wakifanyiwa hivyo kama wao wanavyowafanyia wengine? na akishajioji na kuona nafsi yake inamsuta katika hilo analolifanya, then achukue hatua yeye mwenyewe.

Sikuwa nimetaka sababu za kwanini wao wanashiriki huu mchezo. Na hata ukisoma thread yangu vizuri utagundua kwamba kuna baadhi ya sababu zimejitokeza hasa katika mfumo wa maswali. Hivyo, samahani kama hilo unalotaka liandikwe halijajitokeza hapa. Wewe si ulitegemea waje hapa waanze kukuambia sababu zao za kushiriki huo mchezo ndipo uridhike?

Ni mara ngapi baadhi ya wakina dada/mama wamelalamika humu JF wakionyesha jinsi wanavyoteseka na hiyo hali ambayo mara nyingi wanaume ndiyo wameonekana kuwa chanzo? wengine waliangukia huko kwasababu ya tamaa za kazi, wengine tamaa za pesa, wengine wamelazimishwa na waume/BF zao, wengine wamefanywa hivyo kwa kushawishiwa na kuwekewa vileo kwenye vinywaji, wengine wamebakwa, n.k . Wewe ni shuhuda zipi unazotegemea hao watu wakuletee hapa ndipo uone validity ya hii thread?

Nani kakuambia kwamba kuna hukumu hapa? nani katoa hukumu? mbona unakimbilia hitimisho kumbe hata thread hukuelewa lengo lake ni nini? Hivi unajua kwamba kuna mada nyingi sana unazoweza kuibua katika hii thread? je unategemea yote yanayohusiana na hii thread yajadiliwe ndipo uridhike? Ni bora ujifunze kwamba kunaweza kuwa na mada nyingi lkn mtoa thread yeye anatoa kile alichokikusudia, kwani anafanya hivyo kwasababu anazoona kwamba leo kwenye hii mada amabyo ni pana sana niiandikie katika kipengele fulani ili iwe focused katika eneo fulani tu.

Hapo kwenye Red, do you really expect me to give them a resonable environment for their acts? Do you really think that they don't know what they ared doing? and motives for their acts? forgive me for that, because these people they know for sure what they are doing and my focus/target was to remind them to have a break and think more on the impacts to victims before they act positively or negatively to anal sex.
 
Nimekusoma, nimejitahidi kukuelewa, usinihusishe na kundi lolote kati ya uliyoyapanga. tuweke wazi katika hili, hivi ufiraji ulianza lini na wapi, jamii itajadili ikijua imeanzisha mbio au imepokea kijiti. kwenye swala la hiyari ya moyo, swali la ,unajisikiaje, lina lenga kutoa mafunzo kwa wasiojua kupitia shuhuda za washiriki wa kifiro au kukemea kiaina, wadhani watajiona wajinga na kughairi, unadhani hawakatazwi na vitabu vyao vya dini? au unafikiri hawaulizwi maswali magumu juu ya nafsi zao.

naomba nikufahamishe tu kwamba mimi siyo mnafiki, hivyo siwezi kuwa sehemu ya mchezo halafu nipoteze muda wangu mwingi toka jana kufanya kazi ya kinafiki. kama ulivyoniomba hapo kwamba nisikuhusishe kwenye kundi lolote hapo juu, nilitegemea na wewe kuwa mstaarabu hivyo hivyo.

Kuhusu maswali yako;
1. haikuwa lengo la thread hii kutaka kujua hili tatizo lilianza lini na litaisha lini au lilianzishwa na nani au wapi, kwani hata bila kuuliza hayo maswali bado hakuondoi lengo la hii thread. Kama ungependa kujua hayo pia unakaribishwa kuanzisha thread nyingine ili tujadili chanzo na wapi ilikoanzia na nani mwanzilishi wa huu mchezo.
2. Sikuwa nahitaji mtu yeyote atoe ushuhuda hapa, kwani tayari hapa JF kuna watu wengi tu wameshawahi kuleta jinsi wanavyoumia kwa kitendo hicho walichofanyiwa na baadhi ya watu ktk mazingira na sababu mbalimbali.
3. Kukuemea kiaina-ndiyo (hasa ilikuwa ni kuwapa muda wahusika wajiulize maswali kadhaa kama hicho wanachoshiriki ni salama, then wafanye maamuzi).
4. wadhani watajiona wajinga na kughairi? - sidhani, isipokuwa naamini kwamba walio na utu na uchungu na familia zao wanaweza kughairi na kuachana na hiyo tabia, kwani ni suala la maamuzi ya mtu binafsi na hilo linawezekana; na hili ndilo lengo hasa ya thread hii.
5. Dini zinawakataza? - ndiyo naamini kwamba dini zote zinakataza hata dini ya asili. Kwani ni mambo mangapi ambayo dini hairuhusu lkn bado waumini wanaendelea kufanya? ni mengi tu ; lkn nilitaka hawa watu wapate muda na kujihoji kuona kama wanachofanya ni sawa hata kiimani?
6. Unadhani hawaulizwi maswali magumu juu ya nafsi zao? - yawezekana wanajiuliza au hawajiulizi maswali magumu, lkn kikubwa hapa ni kushiriki kwao katika hilo tendo. Kama watakuwa wanajiuliza maswali magumu na kufanya maamuzi sahihi nadhani tatizo lisingekuwa kubwa kama lilivyo leo. Na kama wanajiuliza, siyo vibaya kwani hata mimi nimewaongezea tu wigo wa maswali ya kujiuliza.

Ahsante.
 
HABARI ZENU WANAJAMVI,

HILI SUALA NALIANDIKA HAPA LKN NAFAHAMU KWAMBA NITATUKANWA SANA HASA NA WALE WOTE AMBAO WAMESHABOBEA KATIKA HILI TENDO CHAFU LISILO LA KIMAADILI. HATAHIVYO, NAAMINI PIA KWAMBA WAPO WALE AMBAO KWAO UKWELI UNASIMAMA SIKU ZOTE NA KUJALI UTU WAO NA WA WENZAO, HIVYO WAO WATAWEZA KUJADILI JAMBO HILI KWA NAMNA YA KUSAIDIA JAMII ILI WAONDOKANE NA HUU UFEDHULI NA UCHAFU UNAOZIDI KUSHAMIRI KILA SIKU KATIKA JAMII YETU YA KITANZANIA. NDUGU ZANGU NIPO TAYARI KWA USHIRIKIANO NA MATUSI LKN NI LAZIMA TUFIKIE KIPINDI TUKEMEE YALE MAMBO YANAYOHARIBU JAMII YETU. Maswali yangu ninayauliza katika makundi tofautitofauti ya jamii kwa wale wote wanaojihusisha na huu ufedhuli na uchafu.

a. Serikali na Watendaji wake.
Ni muda mrefu sana tumekuwa tukilaumu Ohoo Serikali yetu imeshindwa ufanisi katika mambo mbalimbali na lawama zote tumekuwa tukielekeza kwa watendaji wa Serikali bila kujali ni kwa namna gani hata sisi wananchi tunawajibika katika harakati za kuiletea nchi maendeleo, kwa kila mtu kuwajibika katika nafasi yake. Hivi, tumewahi hata kuchukua nafasi na kufikiri ni kwa namna gani nasi tunachangia serikali yetu kushindwa kufanikisha mipango yake? Hivi hizi laana tunazoziletea nchi yetu kwa kufanya huu ufedhuli na uchafu wa kufanya mapenzi kinyume na maumbile tunauchukuliaje? Hivi nchi iliyolaaniwa itaweza kufanikiwa katika mambo yake ya kimaendeleo? Hivi unaweza ukatofautisha huu ushenzi unaofanywa sasa hivi kwenye jamii yetu na dhambi za Sodoma na Gomora?

Je, kwa wale waumini wa Dini mbalimbali mnasemaje katika hili? kwamba Mungu anaweza kubariki watu na Serikali yao lkn watu hao hao wanajihusisha na laana mbaya sana ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile? Hakika tusilaumu Serikali sana kama tunavyofanya sasa, japo ni kweli Serikali inatakiwa kuwa na mipango mizuri lkn hii yote haiwezi kufanikiwa katika jamii ambayo watu wake wanafikiria kufanya mapenzi kinyume na maumbile (sehemu maalumu kwa ajili ya kupitishia MAVI, wao sasa imekuwa sehemu ya starehe kwao).

b. Dinii. Ukristo, Uislamu, Wabudha, Wayahudi, Wahindu, n.k
Swali Kwenu nyinyi Wakristo/ Waislamu/ Wayahudi/ Wabudha/ Wahindu/ n.k; Wake kwa Waume, Vijana na watoto mnaojihusisha na huu uchafu naomba niwaulize swali kwamba; Hivi huwa mnajisikiaje mnapokuwa kwenye IBADA zenu za kila siku au kila wiki na huku unajielewa fika kwamba unajihusisha na mapenzi kunyume cha maumbile? Hivi hisia na nafsi yako inakuambiaje kuhusu huu uchafu anaojiusisha nao? unajisikia tu vizuri kwamba una amani na utabarikiwa wkt unajielewa kwamba either kwenye ndoa yako au nje ya ndoa au na girl friend wako/boy friend wako mnashiriki kufanya huu uchafu? Hivi ni sehemu gani katika Maandiko Mataatifu yanayohalalisha huu uchafu? Je, Mungu unayemwamini hajakuruhusu wewe Mwanamme kufanya mapenzi kwa kutumia Uume wako kwenye Uke wa Mwanamke? ni wapi huyo Mungu unayemwamini na kumwomba amekuruhusu ufanye mapenzi kupitia kwenye sehemu aliyokupa Mungu kwa ajili ya haja kubwa?

Je na wewe mwanamke/msichana mwenye Imani, je ni wapi umepata huo ujasiri na uhalali wa kufanya na kushiriki huu uchafu na bado unajifanya kuwa muumini mzuri? Hivi mnajisikiaje pale maombi au swala inapofanywa na Mchungaji/ Padri/Askofu/Sheik, nk na wewe unashiriki huu uchafu? Hivi OLE iliyotolewa katika Vitabu Vitakatifu kuhusu WAFIRAJI NA WAFIRWA hata hamuiogopi?iii. Dini ya AsiliHivi hata wale ambao wanaamini katika Dini za Asili, je kwa Imani zenu mnaruhusiwa kufanya huu ******? je nafsi zenu zinawasuta au mnajisikia vizuri tu kwamba na wewe unashiriki huu uchafu? Je, ni kwanini tunataka laana kizazi cha leo? Hivi hatuwezi hata kujifunza kutoka kwa Mababu zetu? hivi maadili yamekwenda wapi?

C. Makundi ya watu katika Jamii yetu1. Mwanaume aliyeko kwenye ndoa + Mke wake wa ndoa
-Nina swali kwako wewe Baba/Mwanaume ambaye una ndoa na ushiriki huu uchafu na mke wako, je huwa unajisikiaje unapotembea au unapokuwa katika shughuli zako za kila siku ziwe za binafsi au za kuajiriwa? hivi inapotokea wewe ni bosi ktk ofisi fulani lkn unajihusisha na huu uchafu kwa mkeo je wewe unajisikiaje nafsi yako? je waona kwamba uko salama kwamba unamfira Mkeo mkikutana naye? Haijalishi nani alikuwa wa kwanza kumuanzisha mwenzie lkn suala hapa ni kwamba, je unajisikiaje unapokuwa unashiriki huu uchafu? Je, unapomuona mkeo anakupa hiyo sehemu ya haja kubwa, nafsi yako iko salama tu? je, unamwambia mkeo akate kiuno? Je, baadaye unamwambia kwamba mpenzi wewe ni mtamu? je, mnapokuwa mmemaliza kufanya mapenzi unamwambiaje mkeo? kwamba umefurahi kutumia sehemu ya haja kubwa na hata aibu hauoni? EBU JIHOJI NAFSI YAKO KAMA UNADHANI UNACHOFANYA NI SAHIHI?

2. Mwanaume aliyeko kwenye ndoa + Nyumba ndogo (Msichana ambaye hajaolewa)
Nina swali kwako wewe Baba/Mwanaume ambaye una ndoa na ushiriki huu uchafu na msichana ambaye hajaolewa, je unajisikiaje unapokuwa unajihusisha na huu uchafu na unapofanya naye tendo hilo huku mkeo nyumbani umemwacha? Ni kwanini wewe baba unatumia nafasi yako kumdhalilisha huyu msichana? Je, ni kwanini unamzoeza huu uchafu binti wa watu? kwako unaona ni salama? Je, umewahi kuchukua muda na kufikiria kwamba malipo ni hapa hapa Duniani? kwamba huo uchafu unaomfanyia binti ya watu nawe kuna watu watamfanyia mwanao? Je, umewahi kuwaza unavyomdhalilisha huyo Binti/Msichana kwamba hata mwanao wa kumzaa naye akifanywa hivyo (kuingiziwa Uume sehemu ya haja kubwa) utajisikiaje? Je, utajisikiaje, unapomuona msichana wa watu ****** yanatepeta kwasababu ya huo uchafu unaomfanyia sehemu ya haja kubwa? Je, unapata ujasiri wa kumwambia kwamba umefurahi kutumia sehemu yake ya haja kubwa na hata aibu hauoni? EBU JIHOJI NAFSI YAKO KAMA UNADHANI UNACHOFANYA NI SAHIHI?

3. Mwanaume mwenye ndoa + Mke wa mtu mwingine; Mke wa Mtu + Kijana ambaye hajaoa bado
Nina swali kwako wewe Baba/Mwanaume ambaye una ndoa na ushiriki huu uchafu na mke wa mtu mwingine, je huwa unajisikiaje unapofanya huu uchafu na mke wa mtu mwinigine? Je, umewahi kuwaza kwamba kuhusu uwezekano wa mtu mwingine kufanya huo uchafu na mkeo pia? au na mwanao?Je, baadaye unamwambia kwamba mpenzi wewe ni mtaalamu wa mapenzi kwasababu amekupa sehemu yake ya haja kubwa? je, mnapokuwa mmemaliza kufanya mapenzi unamwambiaje huyo mke wa mtu mwingine/jamaa yako? kwamba umefurahi kutumia sehemu yake ya haja kubwa na hata aibu hauoni?

Hivi na wewe mama mke wa mtu, unajisikiaje pale unapojihusisha na huu uchafu na mme wa mtu mwingine? unaona ni bora tu unampa mwanaume sehemu yako ya haja kubwa ili aweze kutumia na ukitoka hapo unajisikia una amani? Hivi ni kwanini wewe mama unajidhalilisha hivi? Je, hauthamini kabisa hicho kiungo na kuzingatia kazi yake ya kutolea uchafu? Hivi utaweza kupata ujasiri kweli hata wa kumkanya mwanao wk wewe mwenyewe unashiriki huo Usodoma na Ugomora? EBU JIHOJI NAFSI YAKO KAMA UNADHANI UNACHOFANYA NI SAHIHI?

4. Kijana wa kiume (Bachelor) + Msichana ambaye hajaolewa ( Girl Friend wako au wale ambao mmekutana tu kwa kipindi kifupi).
Nina swali kwako wewe kijana wa Kiume na Kike ambaye unashiriki huu uchafu na aidha GF au BF wako, je huwa unajisikiaje unapokuwa unajihusisha na huu uchafu kwa mwenzio? je wewe unajisikiaje nafsi yako? je waona kwamba uko salama kwamba unamfira Mpenzi/mchumba/GF/BF wako? Haijalishi nani alikuwa wa kwanza kumuanzisha mwenzie lkn suala hapa ni kwamba, je unajisikiaje unapokuwa unashiriki huu uchafu? Je, unapomuona mwenzio anakuomba au anakupa hiyo sehemu ya haja kubwa, nafsi yako iko salama tu? je, unamwambia mwenzio akate kiuno? Je, baadaye unamwambia kwamba mpenzi wewe ni mtamu? je, mnapokuwa mmemaliza kufanya mapenzi unamwambiaje mwenzio? kwamba umefurahi kutumia sehemu yake ya haja kubwa na hata aibu hauoni?

Hivi na wewe Msichana, Uke si unao? Je ni kwanini unampa mwanaume sehemu yako ya haja kubwa? nani kakudanganya kwamba ndiyo upendo? then, unajisikia salama tu mwenye furaha kwamba umefirwa? AIBU KUBWA KAMA HII HATA HUWEZI KUSIMAMA NA KUCHUKUA HATUA? Kwanini kujidhalilisha wewe dada? EBU JIHOJI NAFSI YAKO KAMA UNADHANI UNACHOFANYA NI SAHIHI?

NB: Soma kwa makini na uelewe ndipo utoe comment zako hasa sehemu inayokugusa. Pia MOD naomba hii thread isihamishiwe kwenye Jukwaa lolote, kwani hapa MMU ndiyo kuna watu wengi sana na Jamii yetu inaelekea kubaya, hivyo ni jukumu langu, wewe, yule na yeye katika kusaidiana katika kushauriana. Mwenye ufahamu na akili atafikiri na kuyafanyia kazi na yeye atakuwa amesaidiwa katika hili janga kubwa linaloharibu vijna wetu siku hizi.
Yote unayozungmza ni ukweli mtupu.
Naamini unasononeka sana unapoyaona yanayotokea na ni wajibu wako kukemea na huna haja kujihami kupita kiasi.
Nakushauri utafute katika dini tofauti na pia wataalamu wa saikolojia ili uweze kujua HULKA ya binadamu.
Pia utaweza kujua kwa nini kuna TOBA na pia utaweza kuelewa kitu kinachoitwa KUSUTWA NA DHAMIRA (quilty consciuosness).
Binadamu ana mapungufu mengi mno na hata pale atakapokuwa amejitahidi kumkaribia Mungu bado kuna hitilafu.
Mambo ya ngono ni mengi,kuna wanaopata furaha kwa kuumiza,kwa kuingilia watoto,kwa kuvutiwa na watu wa jinsia na hata kwa kuvaa nguo kama chupi ambazo sio za jinsia yako.
Binadamu ana mapungufu mengi na ndo maana kuna TOBA,otherwise Mungu angeangamiza tu.
 
naomba nikufahamishe tu kwamba mimi siyo mnafiki, hivyo siwezi kuwa sehemu ya mchezo halafu nipoteze muda wangu mwingi toka jana kufanya kazi ya kinafiki. kama ulivyoniomba hapo kwamba nisikuhusishe kwenye kundi lolote hapo juu, nilitegemea na wewe kuwa mstaarabu hivyo hivyo.

Kuhusu maswali yako;
1. haikuwa lengo la thread hii kutaka kujua hili tatizo lilianza lini na litaisha lini au lilianzishwa na nani au wapi, kwani hata bila kuuliza hayo maswali bado hakuondoi lengo la hii thread. Kama ungependa kujua hayo pia unakaribishwa kuanzisha thread nyingine ili tujadili chanzo na wapi ilikoanzia na nani mwanzilishi wa huu mchezo.
2. Sikuwa nahitaji mtu yeyote atoe ushuhuda hapa, kwani tayari hapa JF kuna watu wengi tu wameshawahi kuleta jinsi wanavyoumia kwa kitendo hicho walichofanyiwa na baadhi ya watu ktk mazingira na sababu mbalimbali.
3. Kukuemea kiaina-ndiyo (hasa ilikuwa ni kuwapa muda wahusika wajiulize maswali kadhaa kama hicho wanachoshiriki ni salama, then wafanye maamuzi).
4. wadhani watajiona wajinga na kughairi? - sidhani, isipokuwa naamini kwamba walio na utu na uchungu na familia zao wanaweza kughairi na kuachana na hiyo tabia, kwani ni suala la maamuzi ya mtu binafsi na hilo linawezekana; na hili ndilo lengo hasa ya thread hii.
5. Dini zinawakataza? - ndiyo naamini kwamba dini zote zinakataza hata dini ya asili. Kwani ni mambo mangapi ambayo dini hairuhusu lkn bado waumini wanaendelea kufanya? ni mengi tu ; lkn nilitaka hawa watu wapate muda na kujihoji kuona kama wanachofanya ni sawa hata kiimani?
6. Unadhani hawaulizwi maswali magumu juu ya nafsi zao? - yawezekana wanajiuliza au hawajiulizi maswali magumu, lkn kikubwa hapa ni kushiriki kwao katika hilo tendo. Kama watakuwa wanajiuliza maswali magumu na kufanya maamuzi sahihi nadhani tatizo lisingekuwa kubwa kama lilivyo leo. Na kama wanajiuliza, siyo vibaya kwani hata mimi nimewaongezea tu wigo wa maswali ya kujiuliza.

Ahsante.

Telo, inasomeka hautaki mambo ya msingi yajadiliwe, hatuwezi kuwa na mjadala unaofaa bila kuwa na malengo mazuri, ieleweke kuwa wewe ni binadamu kama walivyo wengine usijifanyizie utukufu machoni pako, muda haujawahi kupotea hata mara moja chini ya jua!
kumbe daktari anapokuuliza historia ya kuumwa kwako huwa anakupotezea muda sio? naam kwani lengo lako si kuandikiwa dawa? ya nini akuulize umeanza kuhara lini! unahara majimaji ya rangi gani, maumivu ya mgongo ulianza kuyasikia lini, umeshawahi kupata tiba popote kuhusu tatizo hili n.k,
Tuliza kichwa, bado naamini kuwa maswali yangu ni ya msingi kwenye mjadala huu ulioanzisha, uyajibu tafadhali, lau kama hujui majibu yake kwa ufasaha wana-jf watajadili. oh siyo lengo la mjadala, hii sasa itakuwa re-examination! tuwe na cross examination too.
wakati tunasubiri majibu mazuri ya maswali naliyokuuliza mapema, tafadhali tutajie neno kwa kabila ya kwenu lenye tafsiri ya "kufira"
nasubiri majibu hapa hapa jf.
 
hahahahaha.ukitaka ujue unafiki wa watu subiri siku ikitolewa thrid ya tigo.comment kibaoooooo
 
Nakubaliana nawe,siyo kitu kizuri,among many other things binadamu tunafanya..
 
Ahsante kwa mawazo yako unayodhania kwamba ndiyo yako sahihi. Nilitegemea umesoma hii thread na kuona ilikusudia nini kumbe wapi? nilikuwa nahangaika na mtu ambaye tayari ana majibu yake kichwani, hapo unategemea nini? kama una muda unaweza ukaandika thread yenye kutaka reasons ya kwanini wanafanya hivyo sawa? lengo la hii thread ilikuwa katika mfumo wa swali ukiwataka wote wanaohusika na tendo hilo wajihoji na kuona kama kile wanachofanya ni salama? Je, watufarahi wakiona wake/dada/mama na binti zao wakifanyiwa hivyo kama wao wanavyowafanyia wengine? na akishajioji na kuona nafsi yake inamsuta katika hilo analolifanya, then achukue hatua yeye mwenyewe.

Sikuwa nimetaka sababu za kwanini wao wanashiriki huu mchezo. Na hata ukisoma thread yangu vizuri utagundua kwamba kuna baadhi ya sababu zimejitokeza hasa katika mfumo wa maswali. Hivyo, samahani kama hilo unalotaka liandikwe halijajitokeza hapa. Wewe si ulitegemea waje hapa waanze kukuambia sababu zao za kushiriki huo mchezo ndipo uridhike?

Ni mara ngapi baadhi ya wakina dada/mama wamelalamika humu JF wakionyesha jinsi wanavyoteseka na hiyo hali ambayo mara nyingi wanaume ndiyo wameonekana kuwa chanzo? wengine waliangukia huko kwasababu ya tamaa za kazi, wengine tamaa za pesa, wengine wamelazimishwa na waume/BF zao, wengine wamefanywa hivyo kwa kushawishiwa na kuwekewa vileo kwenye vinywaji, wengine wamebakwa, n.k . Wewe ni shuhuda zipi unazotegemea hao watu wakuletee hapa ndipo uone validity ya hii thread?

Nani kakuambia kwamba kuna hukumu hapa? nani katoa hukumu? mbona unakimbilia hitimisho kumbe hata thread hukuelewa lengo lake ni nini? Hivi unajua kwamba kuna mada nyingi sana unazoweza kuibua katika hii thread? je unategemea yote yanayohusiana na hii thread yajadiliwe ndipo uridhike? Ni bora ujifunze kwamba kunaweza kuwa na mada nyingi lkn mtoa thread yeye anatoa kile alichokikusudia, kwani anafanya hivyo kwasababu anazoona kwamba leo kwenye hii mada amabyo ni pana sana niiandikie katika kipengele fulani ili iwe focused katika eneo fulani tu.

Hapo kwenye Red, do you really expect me to give them a resonable environment for their acts? Do you really think that they don't know what they ared doing? and motives for their acts? forgive me for that, because these people they know for sure what they are doing and my focus/target was to remind them to have a break and think more on the impacts to victims before they act positively or negatively to anal sex.

Maelezo mengi sana, just try to be precise, unakosea sana when you write with emotions. . .the wise keep their emotions aside when discussing critical matters. . .hata kama una mtu wa karibu yako amefanyiwa kitendo kama hicho, just keep your emotions aside ndipo unatoa mada, mada huwa zinaboa sana when watu wakichangia with emotions, sorry to say that.ninaposoma comment zako zote natambua una mzigo wa emotions katika mada hii. Tulia panga hoja taratibu watu watakuelewa. . .
 
Naamin ushapata majib!

Kwn ilikuwa kama research

Hvyo andika findings ktk new thread,

Eleza kwa nin watu wanafanya huo mchezo na sababu zao kwa urefu na upana!
 
kabla sijasema chochote nikuulize maswali kadhaa.....
1. umewahi kushiliki hicho kitendo majuto ni mjukuu?
2. umewaza nini mpaka ukajitoa muanga kusema haya?
3. umeoa au kuolewa?
4. unamtoto wa kike au wakiume?
5. umewahi kusikia sodoma na gomora?

nitatoa ushirikiani baada ya majibu send even in private.
 
well, it is a free world... ; and judging by what is happening in our society today, it looks like this tiGo thing is going to be around for a very very long time...
 
kabla sijasema chochote nikuulize maswali kadhaa.....
1. umewahi kushiliki hicho kitendo majuto ni mjukuu?
2. umewaza nini mpaka ukajitoa muanga kusema haya?
3. umeoa au kuolewa?
4. unamtoto wa kike au wakiume?
5. umewahi kusikia sodoma na gomora?

nitatoa ushirikiani baada ya majibu send even in private.

Karibu uendelee na mjadala.
 
1. sijawahi kushiriki huo mchezo katika maisha yangu na namwomba Mungu aniepushe na hilo.
2. Kilichonisukuma ni jinsi jamii wanavyoteseka na kuumia kwasababu ya hiki kitu. Ni mara nyingi watu wengi ambao ni victims wa hili tendo wamekuwa wakitoa shuhuda za kuhuzunisha sana na kwa kiasi kikubwa wale waliotendwa wamekuwa na matatizo ya kisaikolojia. Kwani, kuna wengi ambao hata ndoa zimevunjika hasa mume anapogundua kwamba mke wake amekuwa akishiriki tendo hilo wkt yeye hakuwahi kushiriki kamwe. Refer hasa kipindi wanapojifungua hospitalini, manesi na madokta wamewahi kutoa taarifa za namna hiyo kwa wahusika. kwa ufupi ni kwamba kilichonisukuma ni jinsi gani naumia sana ninapoona mwanadamu mwenzangu au watu wanavyoumia kama matokeo ya kile walichotendewa.
3. Nimeoa
4. Nina mtoto wa kiume.
5. Ndiyo nimewahi kusikia na kusoma habari za Sodoma na Gomora.

Nafikiri nimekujibu, hivyo karibu na wewe kama haya matendo yanakuumiza hasa yanapotokea katika jamii na baadhi ya watu kuumia (anaweza akawa ndugu/jamaa/marafiki/jirani/n.k).

Inaelekea kuna incident imekudrive kuuliza swali hili, it just did not come out of the blue. Seems like it have hurted you so much. . .i do understand the way you are feeling about this.a piece of advice, if you open more clues might come out. Seems like you are holding something just more than this thread.
 
Jamani naona badala ya kujadili hoja sasa tunahitaji taarifa binafsi za mtoa hoja. Nisichokielewa hapa ni kwamba hili siyo tatizo katika jamii yetu na watu hawaumii kwa matendo haya? Ni kweli kwamba tunafurahia haya matendo yanapotokea kwa ndugu na jamaa zetu. Mimi binafsi nampongeza mtoa hoja kwasababu hili ni tatizo katika jamii japo kuna watu hawako tayari kukubaliana na hilo. Labda nimshauri tu mtoa mada kwamba anapaswa kujua kwamba hili ni tatizo kubwa sana na wengi sana wanaathirika lakni kuna watu hasa wanaume wanaufurahia sana, hivyo asitegemee kupata msaada wa kimawazo kutoka kwa watu kama hao.

Lakini kuna watu kama mimi ambao tumefurahia hii thread kwasababu inatupa changamoto katika suala zima la kimahusiano na kijamii kwa kujaribu kuangalia au kufikiri ni kwa jinsi gani kuna watu wameumizwa sana na hii tabia ya kufanya mapenzi kupitia hiyo sehemu.
 
Don Mangi na Jogi;

Sijui unachohitaji ni kitu gani zaidi? kama maswali yako nimekujibu kutokana na nafasi yangu. Lkn inaonekana hauko tayari kupokea hayo majibu uliyohitaji toka kwangu. Naanza kuamini kwamba tayari una majibu yako kinywani na hivyo unachohitaji ni majibu kulingana na uelewa wako. Hilo inaweza ikawa vigumu kupata, kwasababu watu wanatofautiana ktk kutoa majibu. Swali inaweza ikawa 1 lkn majibu yakawa tofauti, kwasababu tu ni swali la maelezo na si la A,B, au C.

Sasa nikuulize wewe, nini position yako katika jambo hili? kwani umekuwa wa kulalamika tu lkn hakuna sehemu yoyote ambapo umejaribu kuelezea jambo linalojadiliwa hapa ukionyesha ni kwa namna gani wewe unalichukulia hili swala. Je, kwako ni tatizo au siyo tatizo? kwasababu kila wakati umekuwa wa kuuliza tu maswali ambapo kila unapojibiwa inaonekana haujaridhika na hivyo unaishia kutoa maneno mengi ya kebehi tu kwangu badala ya kuelekeza hoja zako kwenye tatizo. Naona umekuwa na visingizio vingi sana katika jambo hili. Kumbuka, toka mwanzo nilifahamu kwamba watu kama wewe watatokea tu kwenye thread, ambao kazi kulaumu lkn hawasemi nini position yao. Naomba pia ukae ukijua hili kwamba lengo langu ilikuwa ni watu wengi sana kusoma hii thread ili wale watakaoguswa na waweze kufanya mabadiliko katika mfumo wa mahusiano yao. Haikuwa lengo langu kutaka watu waje hapa na kutoa ushuhuda wao, na badala yake nilitaka watu wasome hapa na wale watakaoguswa waweze kubadili mfumo wa maisha yao.

Hivyo basi, ni jukumu lako langu, wewe, yeye na yule ambaye sehemu ya jamii kuona kama ni tatizo na kila mtu kufanya sehemu yake ili tuweze kuwasaidia wale wanaoumizwa na matendo haya.

Nafikiri utakuwa umenielewa. Naomba niishie hapo kuhusu maoni na maswali yako. Na nikuombe tu na wewe uweze kuchangia hii thread kama unaona una chochote kitakachoweza kusaidia jamii katika hili tatizo. Jamii inahitaji mchango wako ktk hili na si maswali ambayo hatahivyo hauko tayari kuyatolea majibu ya namna gani unafikiri majibu yawe.
 
Nakupongeza sana Telo kwa kupost mada kama hii, hizi ndio mada zinazotakiwa kujadiliwa ili kubadilisha fikra potofu na mtazamo wa hasi wa jamii ya sasa. Tatizo linakuja pale malumbano ya yanapochkua nafasi katika kujadili mada, sidhani kama hapa si mahali sahihi pa kunyoosheana vidole au kuonyeshana umwamba wa kudefend mada. Ushauri wangu ni kwamba kila mchangiaji achukue nafasi yake, aisome mada kwa umakini, atafakari kwa kina, aingalie nafasi yake katika kuijenga jamii,kama ni mwana dini aingalie imani ya dini yake inamhitaji afanye nini, kisha atoe suluhisho la mada na ushauri wake. Swala la kwamba unafanya au hufanyi, we ni msafi au sio msafi lisichukue nafasi katika kuchangia bali ni usahihi wa tendo hili. Mengine yajadiliwe kwa muda wake utapofika maana jamii yetu inajengwa kwa mambo mengi.Wako wanaofanya hili mengine hawafanyi na wako wasiofanya hili lakini mengine wanafanya kwa hiyo kila moja lijadiliwe kwa wakati wake ili tuijenge jamii yetu pale inapoonekana kupotea kwa mambo yasiyokua ya lazima na yanayoepukika.

SASA Nachangia mada kwa kusema kufanya ngono sehemu ya haja kubwa sio sahihi :
-Kiimani(kwa dini yoyote). Kupotea kwa hofu ya Mungu na Kumkosoa Mungu katika uumbaji wake, Kuacha miili yetu itutawale badala ya kumwacha Mungu atutawale, kupotea kabisa kwa hofu ya Mungu na kuruhusu imani za kishetani kimatendo itawale dunia.
-Kiafya (si kwa wanawake pekee hata kwa wanaume). Kwa wanawake ni kuzaa kwa taabu,kuvuja vinyesi wakati wowote,kutokwa na harufu mbaya n.k, kwa wanaume ni kuziba kwa mirija ya mkojo na uzazi, kupungua kwa nguvu za kiume n.k
-Kiakili/saikolojia(wanaofanya wanahisi ni sawa na ni muhimu na wapo tayari kwa gharama yoyote hata ikiwezekana kubaka, kufanya/kufanyiwa hivi pindi hisia zao zinapowatawala na kuacha kwao ni tabu/ugonjwa hapa hawana tofauti na wanaotumia madawa ya kulevya).
Mwisho naomba kuwashauri wale wanaofanya haya watafute sehemu tulivu,wakae chini wajiangalie wenyewe bila kuruhusu hisia zao ziwatawale, na wajihukumu wenyewe, kisha wachukue hatua, wawe wajumbe wema katika kuishuhudia jamii yetu na wajasiri wa kuijenga jamii yetu katika mambo yenye msingi na maedeleo.
Hayo ni machaache tu niliojitahidi kuchangia, naomba wanajamii wengine waongezee bila kuweka ubinafsi(selfishness) bali wajali utu wao na busara zaidi itumike. Tukumbuke kwamba mabadiliko hayatokei ghafla bali taratibu na kwa mpangilio bila kusababisha madhara.
Ahsanteni
 
nakubaliana na wewe bishanga, si vizuri kujaji watu sana.

Lakini ulipotaja kanisa katoliki umenivutia kuchangia hapa.

Je waufahamu msiamamo wa kanisa katika hili??
Nakumbuka katika mafundisho ya kanisa katoliki dhambi zimegawanywa katika makundi mawili, dhambi za kawaida na na dhambi za mauti.

Katika dhambi za mauti hii ni included kwa hiyo kwa kanisa hii ni kati ya makatazo makuu.

Padri anavyosema maneno yale naamini, ni kusihi sadaka ile ipokelewe pamoja na udhaifi wake wa kibinadamu.

Telo, katika liturgia ya misa katoliki wakati wa kubadili mkate kuwa mwili wa Yesu,Padre huwa anatamka hivi:...Ee Baba usiangalie matendo yetu bali imani ya Kanisa lako Takatifu.....'je unaelewa Kanisa linamaanisha nini hapa? Tafakari,jipime na uone wewe ni msafi kiasi gani kabla hujatoa hukumu nzito kama ulivyofanya kwenye thread yako hii.
Nahitimisha kwa kukupa ushauri wa bure:
Waislam wanasema ....'swali kabla hujaswaliwa...'
Telo.weka bidii ya kutosha katika kuokoa roho yako through prayers,kufunga,kutoa sadaka etc badala ya kuhangaika na private affairs za watu wengine ambazo kusema kweli hazikuhusu wala kukuathiri kwa lolote kwani unayolalamikia yanafanyika vyumbani na wala hujawahi kuyashuhudia kwa macho yako.Kumbuka duniani humu kila mja kaja kivyake na ataondoka kivyake.STOP JUDGING LEST YOU BE JUDGED!
 
Back
Top Bottom