Kwanini wanaoshuhudia miujiza kwa Mwamposa wengi ni waislam tena wanawake?

Wewe utakuwa ni mgeni mkuu.

Mimi mwenyewe ninafuatilia hapa. Ila nikuambie tu kuwa wengi wanaotendewa hususani sisi wakristu huwa tunakuwaga kama na aibu fulani hivi kwenye kushuhudia. Ukitaka kuliamini hilo, angalia ule mfano wa kwenye biblia. Walitendewa kumi lakini ni mmoja tu alierudi kwa Yesu kushukuru.

Mpaka Yesu akamuuliza wale wenzio wako wapi? Kama sijakosea. Sasa wenzetu waislam wana ujasiri sana aisee.

Tofauti sana na sisi wakristu
Wote ambao hawakurudi kushukuru walikuwa wayahudi (jamii yake Yesu). Aliyerudi kushukuru alikuwa msamaria!
 
Na mtu mwenye kuamini kweli hasa hatakaa akafanya upumbavu kama huo.

Hawa unakuta wale wenye imani nusu nusu. Hawapo thabiti.
 
kuna dada wa kazi nyumba jirani basi anapenda hizo shuhuda atari, jana kawasha kiledio chake, eti mtu katoka tabora kaja toa ushuhuda kapona ukimwi
asee nimejikuta nacheka kutokana mkanganyiko wa maelezo yake, huku kuna mtu ana mwingoza kuongea,

Sent from my SM-S920L using JamiiForums mobile app
 
MWAMPOSA ni tapeli mkubwa,
Nna shangazi yangu anasumbuliwa na presha na kisukari, aliniomba nauli Mimi nikakataa, yaani atoke Tabora aje kuombewa na Mwamposa,eti ana amini atapona, basi bwana akauza Cha kuuza akapata nauli toka Tabora akaenda dar kwa Mwamposa, akakaa week mbili huko, alivyorudi Mimi baada ya mwezi nikampigia kujua maendeleo yake, ah wapi, kisukari kilichachamaa na presha pia,maana aliacha kutumia vidonge vya presha
Kwahiyo ulifurahi kuona presha imechachamaa..kumbuka hata Yesu aliponya ila alikua anasema imani yako imekuponya..amini kwanza...acha maovu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri anaeamini majini,kuliko anaewaamini Hawa waganga wa kienyeji kina MWAMPOSA na wengineo,eti chumvi ya upako,Mara leso ya upako,Mara sijui chukua mchanga wa pembe nne kwako akauombee, yaani uchawi mtupu na utapeli
Roho mbaya inakusumbua..njoo uombewe hayo majini na maruhani yakutoke..karibu kwa mwamposa ukanyage mafuta upate upako.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kama ni Waislamu ?

Unajua kama Waislamu wengi wanatoka katika Uislamu bila kujijua ? Mpaka mtu anaenda huko ujue huyo si Muislamu tena sababu anakuwa amekiuka mafunzo ya Uislamu na kuona aliyo kuja nayo Mtume hayatoshelezi. Sasa kwa ushahidi gani utuambie hao ni Waislamu ?
Ni wengi sana na hilo liko wazi tena wanatoka pwani!,Lindi ,Mtwara...ni waislamu pure!
Kwani kuwa muislam ndo nishindwe kuhangaika kutafuta soln napopata matatizo?
Watu sshv wamechoka kunyang'anywa uhuru wao wa,kuamua maisha yao...kila mtu anaenda kuhangaika kivyake apate soln ya shida yake!
Ni Uhuru tu
 
Inamjua Jini wewe!!?..Jini umtishie yesu atoke!!
Kwa jina la Yesu kila goti linapigwa,jini kitu gani kwa Yesu?
Sio yesu ni Yesu!

Tena huwa yanatoka bila kutishiwa mkuu ni mamlaka na nguvu na uweza!
 
Kama una uelewa wa Marketing and Sales huwezi shtuka. Ushuhuda wa mkristo hauna mvuto si ajabu wakapangiwa siku nyingine ila sio siku yenye hadhara kubwa. Ushuhuda wa mwislamu ndio unauza mahubiri.

Kama ulikuwapo....
 
Hamna ukweli wowote wale wanapewa pesa kutoa ushuhuda na sio waislamu wale wengine wakristo wanatoka mikoani ile ni marketing level ambayo ni promotion kuwa makini wali serious na magonjwa wapo hospital aende

Kama una akili timamu unashindwa kutambua kitu kidogo kama icho

Kuna wajinga wengi sana ndugu yangu....
 
Ni wengi sana na hilo liko wazi tena wanatoka pwani!,Lindi ,Mtwara...ni waislamu pure!
Kwani kuwa muislam ndo nishindwe kuhangaika kutafuta soln napopata matatizo?
Watu sshv wamechoka kunyang'anywa uhuru wao wa,kuamua maisha yao...kila mtu anaenda kuhangaika kivyake apate soln ya shida yake!
Ni Uhuru tu
Ulitakiwa uelewe kwanza nilichokiandika, kuliko kukurupuka kama ulivyo fanya.
 
Nimeangalia hapa, huyu mzee ananyomi kama ya lowasa! Sadaka pale hakosi million 100 kila wiki
 
Back
Top Bottom