Kwanini waislamu hawana imani na vitengo vinavyohusika na takwimu?



1. Kwanini ukweli usisemwe? Si Mkoloni pekee, na wale walioachiwa na Mkoloni wameendeleza, msome Sivalon, Bergen hao wote ambao wewe kwako si matapeli huyo Sheikh anatowa reference, unaweza kuwanukuu japo kidogo kuhusu elimu?

2. Huna uwezo wa kutatua tatizo bila kujuwa chanzo chz tatizo.

3. Wapo wengi tu, wala usiwe na shaka, tulibanwa zamani, sasa tunaibuwa madudu mpaka NECTA. Hujaona? basi hata hujasikia? Hata Slaa hana degree yoyote lakini ana PhD, kwi kwi kwi teh teh teh! kuta nne siyo mwisho au mwanzo wa elimu, huo ni mwanzo wa kuwa "programmed" kama unavojidhihirisha.

4. Ullipoamka wewe, wenzako ndipo walipolala, mwenyewe unaona umetowa wazo la maana? soma hapa: Tanzania Muslim Professionals

Mkuu Zomba,
Kwanza nashukuru kwa kujibu hoja zangu kwa kiasi ulichoweza. Ningependa tuendelee kuelimishana kama tu tutakuwa wastaarabu kwenye maandiko yetu maana tuko kwenye Great Thinkers Forum na hoja tunayojadili ina maingiliano na dini na hivyo ni muhimu kutojadili kwa jazba bali kwa kutumia facts.

  1. Kutoa reference haina maana unachoongea kinaukweli au kina mahusiano na hizo references. Ndio maana yule 'Shehe' hakunukuu aya yoyote kwenye hivyo vitabu alivyo-refer bali alivitumia kama viini macho (references on the fly). Ningekushauri uvisome kabla hujaweka imani yako mikononi mwake na pia usome materials nyingine kama hii thesis ya Bwana Abdin Noor Chande niliyoibandika hapo juu. Hakuna mtu mwenye umiliki wa ukweli bali facts ndio zinazotofautisha claims za ukweli wa watu wasiokubaliana.
  2. Ni kweli kujaribu kutatua jambo bila kujua chanzo unaweza usipate ufumbuzi mzuri. Lakini ni vema pia ukaelewa historia kwa kusoma wewe mwenyewe na kujua facts, na sio kwa kusikiliza na kuyumbishwa na hotuba za watu wanaojifanya wajuzi kumbe ni mbwembwe zao tu kwa ajili ya ulaji na wengine wakiwa na nia mbaya na nchi.
  3. Nafikiri pia ni kosa kuwafikiria Watanzania wenzako kama 'sisi' na 'wao'. Tuwe wamoja maana hatuwezi kuigawa nchi kwa vile tumechanganyika.
  4. Halafu sidhani kama Nyerere yule yule aliyezifungua shule za Wamisionari kwa Wananchi wote awe eti ndio huyo huyo aliyebuni mbinu ya kuwaminya waislamu elimu. Kuna msemo unosema kuwa "unaweza kumpeleka farasi mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji". Nyerere alifungua milango kwa waislamu lakini kwa sababu fulani fulani hawakusonga mbele haraka.
  5. Natumaini kuwa wewe huna fikra za kuwa kumekuwa na mbinu za serikali kuwaminya waislamu elim dunia. Kama unajua jinsi ya ku-program au hata kuandika tu formula za kawaida kwenye MS Excel au spreadsheet yoyote, utaelewa vema kilichotokea hapo NECTA. Lakini kama huelewi hizo software zinavyofanya kazi, basi inaweza ikawa rahisi kwako kukubali hizi conspiracy theories za kwamba waislam wanaonewa na NECTA. Binafsi sidhani kama idara nzima iliyojaa waislam na wakristo inaweza kufanya upuuzi wa kuwafelisha waislam tena kwenye somo ambalo ni la kwao tu na hawana ushindani nalo na wakristo.
  6. Nimeiangalia hiyo www ya TMP na nilichoona sikukifurahia. Ingawa siwajui wenye hicho kikundi, lakini sikuona chochote kinachoonyesha kuwa wana nia njema na waisalamu. Kwa mfano, nimeona wameandika kuwa wanataka kuwasaidia umma kwa kuwapatia ajira, lakini ni lazima kila anayetafuta msaada awalipe TShs 10,000. Huu ni utapeli.
Wasomi wanaotakiwa kuwaeleza waislamu ukweli ni watu kama akina Kikwete, Mwinyi, Bilali n.k., watu waliokamata madaraka ya juu kabisa nchini. Hawa wanaelewa ukweli na pia wanajua jinsi baadhi ya waislam walivyo na fikara za kuwa wanaonewa au kupunjwa, lakini kwa sababu wanazojua wao wenyewe, hawajitahidi kuelezea wananchi na hasa waislamu wenzao ili waweze kujikwamua. Na kwa vile wao hawafanyi kazi hiyo, ndio wanapojitokeza hawa mashehe uchwara na kutumia dini kuwachonganisha Watanzania.



 
Mkuu Mohammed Shossi bila shaka umesikia idadi ya watu Zanzibar wako 1.3 milioni hivi sasa sijui mwaka 1967 walikuwa wangapi ?.Ni dhahiri idadi ya wazanzibar isingeweza kuleta athari kubwa kama ulivyokuwa ukitaka kutuaminisha.

KWA NINI WAISLAMU HAWANA IMANI NA VITENGO VINAVYOHUSIKA NA TAKWIMU?

Hili ni suala muhimu kulipatia jibu na kulifahamu kwa kina sisi kama Waislamu. Wengi wana maoni kuwa kitendo cha Waislamu kuomba kushirikishwa katika Sensa na kuomba kuingizwa kwa swali la Dini ni ukorofi tu wa Waislamu.

Ukweli unafichwa na makala hii ina lengo la kuwajuza watu vipengele kadhaa juu ya hila katika sensa zilizopita. Makala hii itadhihirisha "uchakachuaji uliofanyika na ofisi za serikali katika kutangaza mgawanyiko wa watu kwa mujibu wa dini kabla ya serikali ya Mwalimu Nyerere kuamua kulifuta swali la dini katika sensa ya Tanzania iliyofanyika mwaka 1978.

Tanganyika au Tanzania imeshafanya sensa mara 6. Mara mbili za mwanzo sensa ilifanyika kama Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza yaani mwaka 1948 na mwaka 1957. Kisha sensa nne zilizobaki zilifanyika Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zikiwa zimeshaungana.

Sensa ya mwanzo ya Tanzania huru iliyoungana iifanyika mwaka 1967 na hii ilikuwa ni sensa ya mwisho kuuliza swali la dini. Sensa zilizobaki zilifanyika mwaka 1978, 1988 na 2002. Sensa ya mwaka huu, 2012 itakuwa ni ya saba katika historia ya nchi yetu na ya tano ya Tanzania huru iliyoungana.

Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.

Haya nayo ni maajabu, yaani unaweza ukadhani labda Tanzania ina tatizo la Waislamu kuwacha dini yao na kuwa wapagani. Hili nalo halina ushahidi wowote kuwa lilitokea katika kipindi hicho.

Athari kubwa ya kimabadiliko iliyotekea katika sensa hii ni kujumuishwa kwa Wazanzibari katika sensa kwa mara ya kwanza. Kwa vile Wazanzibari karibu 98% ni Waislamu tegemeo lilikuwa Waislamu Tanzania wapindukie angalau 65% (kutoka 58% ya mwaka 57 ambayo haikujumuisha Wazanzibari) ya watu wote lakini badala yake wakashuka hadi 31.4%

Tukumbuke kuwa Waislamu ndio watu ambao mara nyingi hulaumiwa kutofuata uzazi wa majira, hulaumiwa kwa kuozesha mabinti zao mapema na ni dini inayoruhusu mume mmoja kuoa wake wanne, haya yote hupelekea ongezeko kubwa la idadi, lakini ajabu ni kuwa Waislamu walipungua, si kwa asilimia 2 - 3% bali kwa 26.6%! Hivyo ni wazi Takwimu zilizotolewa na serikali ya Mwalimu Nyerere ama zilikuwa ni za uongo wa makusudi ya kupotosha au zina makosa.

Lakini cha kushangaza ni kuwa baada ya sensa hiyo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliamrisha kipengele cha dini kuenguliwa kwenye sensa bila ya kueleza Watanzania lengo la kukiondoa kipengele hicho. wakati huo tayari Tanzania ilishaanza kugubikwa na wingu la udini baada ya Mwalimu Nyerere kuamua kuivunja Jumuiya adhimu ya Waislamu East Africa Muslim Walfare Society (EAMWS) na serikali kuunda Jumuiya ambayo mpaka leo waislamu wana mashaka nayo ambayo ni BAKWATA.

Naomba sana tuzingatie nukta hii kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislamu bali iliundwa na Serikali iliyoongozwa na Mwalimu Nyerere. Kudhihirishwa kuwa mwaka 1967 udini ndio ulikuwa unaanza kushamiri Tanzania sio tu katika sensa na kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA, mwaka 1967 ndio mwaka wa Azimio la Arusha na mwaka wa kesi ya uhaini iliyojumuisha Waislamu na wengi wakawekwa rumande kwa tuhuma hizo akiwemo wanasiasa maarufu ambao waliiunga mkono EAMWS akina marehemu Bibi Titi Muhammed na Tewa Said Tewa. Hivyo leo utaweza je kuwalaumu Waislamu kwa kukosa imani na serikali katika hoja ya sensa?

Mara nyingi panapotokea badiliko kubwa kama lile ambalo linaaminika kuwa ni la kuchakachuliwa yaani Waislamu kupungua Tanzania kwa 26.6% na wapagani kuongezeka Tanzania kwa 24.3 katika kipindi cha miaka 10 (jambo ambalo mtaalamu yoyote wa sensa au takwimu hawezi kukubaliana nalo) palitegemwa pafanyike utafiti wa sababu za mabadiliko hayo, lakini hakuna aliyeamua kufanya hivyo na sababu kuu ni kuwa watu walijua wazi kuwa takwimu hizo ni za kupika.

Sisi ni great thinkers tujadili niliyoyaleta jamvini kwa hoja na tafakuri jadidi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom