Kwanini wafanyabiashara wengi wa Kariakoo hawaelekezagi vizuri mahali husika?

ilishawahi nitokea hii, nilizunguka balaa, hatua ya mwisho nikaona duka nikanunua soda, nikamuuliza muuzaji akasema hapo mbelee tu Yani tena panaonekana kabisa sehem husika.
 
Yaani Kariakoo unaweza kuwa labda upo karibu na eneo unakoelekea ila ukimuuliza mtu lazima tu atakuhamisha njia au mtaa sijui kwanini?

Utasikia shuka mtaa wa pili kushoto kukia kuna jengo refu ndo hapo.

Acheni tabia hizi watu wa Kariakoo.
Hiyo ni tabia ya wabongo ujuaji na kupenda kutoonekana hawajui. Siku chache nyuma hapo nilimuuliza mlugaluga mmoja anauza nguo mkononi, nikataka aniambie kanisa la KKKT liko wapi akanielekeza barabara ya kwenda Mnazi Mmoja wakati nilikuwa China Plaza
 
Wafanyabiashara wengi wanakuja na magari kujua mitaa ya hilo jiji utawavuruga tu,
Tuulize sisi watembeza madafu na machungwa uielewe mitaa

Kwanza wanawazaga mambo lukuki mda wote usishangae siku nyingine ukajibiwa huo mtaa uko zanzibar
 
Hiyo ni tabia ya wabongo ujuaji na kupenda kutoonekana hawajui. Siku chache nyuma hapo nilimuuliza mlugaluga mmoja anauza nguo mkononi, nikataka aniambie kanisa la KKKT liko wapi akanielekeza barabara ya kwenda Mnazi Mmoja wakati nilikuwa China Plaza
Haha sijiu kwanini inakuaga hivyo
 
Hiyo ni tabia ya wabongo ujuaji na kupenda kutoonekana hawajui. Siku chache nyuma hapo nilimuuliza mlugaluga mmoja anauza nguo mkononi, nikataka aniambie kanisa la KKKT liko wapi akanielekeza barabara ya kwenda Mnazi Mmoja wakati nilikuwa China Plaza
Tujitahidi kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ndugu zangu. Sasahv unawasha Google map inakupeleka mpaka point husika, hautokaa umuulize mtu sehemu hasa kwa zile sehemu maarufu. Mfn Kanisa, Msikiti, Supermarket, Shule, nk
 
Hii ndio Point ya Msingi. Google Wamerahisisha sana maisha.

Ingawaje kuna siku nikiwasha nikafika destination sioni ofisi niliyokuwa naifwata, Bahati nzuri nikamfata mama mtu mzima fundi cherehani hapo nikamsalimia na vi stori vya uongo na ukweli kisha nikamuuliza ofisi X ilikua ipo hapa zamani, ni kiaka sasa sijapita eneo hili, leo nakuja siioni! Akaniambia ni kweli walihamia mtaa wa tatu nyuma, akanielekeza. Nadhani Kulikua na Makosa ya upakiaji Ramani Google wakasahau kuhamisha anuani ile.
 
Google hawakua na makosa. Wanaotakiwa kubadilisha anuani ni hao wenye ofisi iliyohama au hata wewe baada ya kujua imehama, unge-edit address kusaidia wengine
 
Mjini salamu ndio ya bure, tena kkoo kupewa chimbo bure utasubiri sana 😂😂
Lipa pesa upelekwe chap kwa haraka, kule watu wako busy
 
Back
Top Bottom