Kwanini vyama vya upinzani alivyopitia Mh. Lyatonga Mrema vimekufa?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Huyu Makamu Pekee wa Waziri Mkuu ana jini gani maana NCCR Mageuzi na TLP viko hoi.
Pia kwenye kinyang'anyiro cha uraisi mwaka jana alikuwa akimpigia kampeni Kikwete ilhali TLP walikuwa wamesimamisha mgombea.
 
huyo ni bonge la YUDA
kumnunua ni rahisi sana na ccm wanajua bei yake
isitoshe huyo ni ccm wala sio A au B ni hiyo ya jk
 
Jamani mrema kachoka ile mbaya!!!!hana hoja bungeni yy analalamika maandamano tuuuuu!!!mm nahisi anaota zile enzi za umaarufu wake ila hajui atarudi kwa stail gani.....
 
NCCR Mageuzi sasa hivi ina wabunge wengi zaidi ya wakati wa Mrema akiwa Mwenyekiti
 
NCCR Mageuzi sasa hivi ina wabunge wengi zaidi ya wakati wa Mrema akiwa Mwenyekiti
Lakini sio chama kikubwa cha upinzani. Hii ni downfall ya umaarufu. Pia chama chao kina ushirikiano mkubwa na CCM kiasi kwamba hata wabunge wao wanaonekana ni majununi.
 
NCCR Mageuzi sasa hivi ina wabunge wengi zaidi ya wakati wa Mrema akiwa Mwenyekiti
Siamini kama hii hoja yako ina ukweli wowote, uchaguzi wa mwaka '95 NCCR ya mrema ilipata wabunge kama 15 hivi nikikosea nisahihisheni, ila ni wengi kuliko hawa wabunge wa 4 waliopo sasa
 
NCCR Mageuzi sasa hivi ina wabunge wengi zaidi ya wakati wa Mrema akiwa Mwenyekiti
Usiropoke kama hujui uliza.Unawajua hawa?Masumbuko Lamwai, Ndimara Tegambwage, Mabere Marando, James Mbatia, Augustino Mrema, Stephen Wasira, Prince Bagenda na wengineo walikuwa ni kina nani ndani ya bunge la kwanza la mfumo wa vyama vingi? Linganisha hao na wabunge watatu wa sasa ukiondoa wa VITU maalum
 
Kabla ya Wasira hajaitwa Tyson
 
Good question! Tukumbuke hizi bajeti za kikwete, Mkullo na Ndulu zinatenga posho maalumu kwa ajili ya wananchi dhaifu kama Lyatonga na wengine wanaopandikizwa na usalama wa taifa kumaliza upinzani. Kwa habari yenu ccm na kikwete, sisi cdm hatuna njaa kama hao mliowaonga. Tunajua wapo weak people cdm, mjue pia hata sisi cdm tunawatu ndani ya ccm. CDM is a movement na sio chama na tunajua hii game ... we are getting stronger and stronger while you guys are almost dead.
 
mi ni tofauti kidogo na wengine! Mrema ni mfano na funzo katika historia ya siasa za nchi hii!

Kwamba hata ukiwa kiongozi wa ngazi gani, bila kujali maslahi, kama unaona msimomo wako wa haki unabezwa na wenzako, ikibidi uachie ngazi ili mradi kuonesha msimamo wako! mrema aliweza kufanya hili, ni wachache miongoni mwa viongozi wetu wa kizazi hiki wanaoweza kufanya hivyo!

Katika hatamu zake za uongozi anakumbukwa kwa msimamo wake wa kutetea wanyonge, hata kama kulikuwa na matatizo hapa na pale, tungekuwa na viongozi 10 tu wa aina ya mrema wa enzi za mambo ya ndani, kusingekuwa na haja ya taasisi kama TAKUKURU, uadilifu na uchapa kazi miongoni mwa watumishi wa umma usingekuwa wa kiwango tunachoshuhudia leo.

Licha ya matatizo yake kama binadamu, mrema ni funzo kwa viongozi wetu, kwamba hata kama utapendwa namna gani ukitenda kinyume na matarajio yao watakupuuza.... alipendwa wakati ule sasa amepuuzwa..

kudhohofika na hata kufikia kiwango alichofikia mrema ni onyo kwa wanasiasa wetu shupavu, wajue wanapotangaza vita na viongozi dharimu wa dora wajue watashughulikiwa hadi waonekane kama wendawazimu mbele ya jamii, mbinu ni nyingi za kuwafikisha hapo, zilizotumika kwa mrema ni baadhi tu, hata hivyo wasikate taamaa kwani wakiisha kujua hatari iliyo mbele yao kwa kuangalia mifano kama mrema, watajiandaa kukabiliana nayo...

kwa jamii ya watanzania, inapomuangalia mrema inajifunza mengi, kwamba kiongozi hata awe shupavu namna gani anaweza kufanywa kama punguani hivi... baada ya kupita katika tanuri la manyanyaso na udharirishaji wa kila aina mikononi mwa watawala dharimu

Ole wao nyakati zitakapowagaekuwa, maana wao ndiyo watakuwa wendawazimu na kudhoofu kwa maradhi yanayotokana na msongo wa mawazo... na nyakati hizo haziko mbali
 
Back
Top Bottom